Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
HABARI ZILIZOANDIKWA KATIKA MAGAZETI MBALIMBALI LEO ZINAONYESHA KUWA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KITASAMBAZA WAANGALIZI HURU NA KUJUMLISHA MATOKEO. KILA MKOA KITAKUWA NA MWANGALIZI MMOJA. KULINGANA NA HABARI HII HAPA CHINI INAONEKANA WAANGALIZI NI 1744. Swali dogo je vituo vya kupiga kura mwaka huu ni vingapi kama idadi hiyo ni sawa na ya vituo vilivyoko basi matumaini yetu ni makubwa.
Hongereni sana.
HRC kusambaza waangalizi majimboni
NA RICHARD MAKORE
16th October 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa ndani wanatarajia kuanza kusambaza katika majimbo mbalimbali kunzia Jumatatu ijayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Katemana, alisema jana kuwa waangalizi hao wanafikia 1,744 na watakuwa katika mikoa, majimbo na kwenye vituo vya kupigia kura.
Waangalizi hao wameteuliwa na mtandao wa Asasi za Kiraia (TACCEO) unaoundwa na mashirika 17 ambapo watatumia kompyuta na simu za mkononi kufanya kazi hiyo.
Kadhalika, mtandao huo umeandaa utaratibu utakaowawezesha wananchi kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa waratibu wa kitaifa watakaokuwa Dar es Salaam kupitia namba 15540 kwa mitandao ya Vodacom, Tigo, Zain na Zantel ili kutoa taarifa kwao juu ya mambo mbalimbali yatakayotokea katika vituo vya kupigia kura.
Waangalizi hao watasambazwa katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar kwenye majimbo na vituo vyote vya kupigia kura.
Katemana alisema waangalizi 270 watakuwa katika majimbo na kila mkoa utakuwa na mratatibu mmoja ambaye atakuwa anaratibu shughuliz zote za uangalizi na kutoa taarifa makao makuu ya mtandao huo yatakayokuwa jijini Dar es Salaam.
Asasi hizo za kiraia ni pamoja na Tamwa, SAHRINGON Tanzania, WLAC, TANLAP, WILDAF, ForDIA, Haki Madini, MPI, ACCORD, ZLSC, PF, Tahurifo, YPC, LEAT na LHRC.
Alisema TACCEO imepata kibali cha kufanya kazi hiyo kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwamba lengo la uangalizi huo ni kuanisha mapungufu yatakayojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010.
Kwa mujibu wa Katemana taarifa zitakazokusanywa nchi nzima na kuchambuliwa ili kuweka kumbukumbu na rejea ili ziweze kusaidia kuboresha Uchaguzi Mkuu siku zijazo.
Maeneo mengine yatakayoangaliwa na waangalizi hao ni pamoja na kiwango cha wananchi kuelewa masuala ya uchaguzi, elimu ya uria kwa wananchi, ushiriki wao, ushiriki wa wadau mbalimbali kama Nec, vyomb o vya habari, vyombo vya usalama na Asasi za kiraia zinavyoelimisha jamii.
CHANZO: NIPASHE
0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni