JAMHURI YA IRELAND
23 November 2023
Dublin, Jamhuri ya Ireland
Wananchi waingia mitaani kufanya vurugu kubwa dhidi ya serikali yao ya mrengo wa kiriberali wakidai inafungua milango na kukaribisha wahamiaji bila kwanza kusikiliza maoni ya raia wa nchi ya Ireland .
Picha : Polisi wakipambana na raia mjini Dublin, nchini Ireland.
Vurugu hizo zilianza baada ya taarifa kuzagaa ktk mitandao ya kijamii kuwa kuna shambulio la kisu lililotokea katika shule moja ambapo mwanamume mmoja alimshambulia mama mmoja na wanawe wadogo wawili wa umri wa chini ya miaka 10.
Mtu huyo aliyefanya shambulio inasemekana ametokea nchi ya Algeria na hivyo wananchi wenye hasira kali walivamia mitaa na kuchoma moto magari ya Polisi na majengo kadhaa kwa kulaumu serikali na vyombo vya dola kuwalinda wahamiaji wanaoleta tamaduni na desturi zisizokubalika Ireland kwa kuruhusu maelfu ya wahamiaji. Pia wakalaumu taarifa za awali za Polisi kutoweka wazi ni nani kutoka wapi amefanya shambulio hilo .
Waziri Mkuu wa Ireland Bw. Leo Varadkar alisifu hatua za watu waliosaidia kusitisha shambulio hilo kwa kumdhibiti mshabulizi huyo mwanamume
"Ilikuwa ni kitendo cha kutisha cha vurugu - na mawazo yetu yako kwa watoto waliojeruhiwa, pamoja na wapita njia wa kishujaa ambao walijitia katika hatari kujaribu kuwalinda, watoto pia mama yao.
Lakini waziri mkuu Bw. Leo Varadkar aliwakasirisha raia wa Ireland kwa kauli yake kuwalaani waliojitojeza kufanya vurugu ambao aliwaita ni wa mrengo mkali wa kulia, wakati watu hao waliofanya vurugu wao wanajiona ni walinzi dhidi ya wahamiaji wageni wenye ajenda ya kuua tamaduni, desturi na imani za watu wa Ireland.
Jamhuri ya Ireland ilipata mamlaka yake baada ya kupambana kwa miaka mingi takribani 100 hadi mwaka 1921, na kuzitia moyo nchi kama South African Republic huru 1910 , India 1919 kuiga vuguvugu la Republic of Ireland kujinasua kutoka kukaliwa na ma settler
Hivyo raia wa Jamhuri ya Ireland ni watu wanaojivunia utaifa na uraia wao walioupambania na kuwashutumu viongozi wenye merengue ya kiliberali kusaliti historia na utamaduni wa Ireland.
Uholanzi
Nako nchini Uholanzi nchi ambayo imekuwa kimbilio la wahamiaji wengi, kupitia uchaguzi wameamua kumchagua Bw. Geert Wilders kuwa waziri mkuu mpya baada ya chama chake kupata viti vya ubunge vya kutosha kuunda serikali ya umoja.
Geert Wilders anayejulikana kwa mtindo wake wa kipekee wa nywele wa rangi ya platinamu na kauli zake kali za kupinga Uislamu na uhamiaji, ameshawishiwa na uchaguzi wa Uholanzi hadi mahali anapopenda zaidi kuwa: katikati ya mamlaka ya maamuzi .
Katika tetemeko la ardhi la kisiasa, chama cha Wilders’s Freedom kilipata kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa wabunge nchini humo, na kumfungulia njia mwanasiasa huyo kuchukua nafasi muhimu katika kuunda serikali ijayo baada ya kampeni iliyotawaliwa na mjadala kuhusu uhamiaji.
Kutokana na kuuelezea Uislamu kama "itikadi ya utamaduni uliodumaa" na kuwaita Wamorocco "wachafu", Wilders, ambaye mara nyingi hulinganishwa na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa matamshi yake ya kichochezi na matumizi ya mitandao ya kijamii, kwa muda mrefu amekuwa mtu maarufu katika Ulaya. mandhari ya kulia.
Alizaliwa mwaka wa 1963 kusini mwa Venlo, karibu na mpaka wa Ujerumani, Wilders alikulia katika familia ya Kikatoliki pamoja na kaka yake na dada zake wawili. Aliingia katika siasa akiwa mwanachama wa Chama cha People’s Party for Freedom and Democracy (VVD), lakini akaacha kile alichokiona kuwa msimamo mpole wa chama hicho kuhusu Uislamu na uhamiaji.
Taifa la kifalme la Uholanzi nalo lina historia ya kuwa mojawapo ya mataifa makubwa yaliyotawala mapande makubwa ya nchi za mbali huko Indonesia, Marekani ya Kusini kama ilivyokuwa Portugal, Spain walipoigawa dunia ktk pande mbili yaani moja magharibi huku Bara la Marekani yote kasoro Brazil ya mashariki kuwa makoloni ya Spain na Mashariki yote ya dunia yaani bara Afrika, Asia ya Kusini, India kuwa chini ya Portugal. Ndiyo maana Brazil ni nchi pekee ya Marekani ya Kusini inaongea lugha ya Portuguese.
Kabla mataifa mengine ya Uingereza na Uholanzi kuibuka na wao kujimegea makoloni kupiti vita na mataifa hayo ya Spain na Portugal.
Hivyo manung'uniko ya raia ya Uholanzi ni kuwa sasa nchi yao kidogo kidogo imeanza kuvamiwa na wageni, hivyo wameamua kupeleka ujumbe kwa serikali na vyama vya kisiasa vya kiliberali kuwa hawaafiki kuvamiawa nchini kwao kupitia sera za viongozi wachache waliopo madarakani.