Matukio mbalimbali niliyokutana nayo kwenye usafiri wa mabasi ya mikoani

Muzine

JF-Expert Member
May 4, 2017
32,366
60,406
Habar wana Jf

Katika harakat zangu za maisha nimekutana na viroja vingi sana ndani ya mabasi ya mkoani ambayo ni

1.Kukaa siti moja na mtu anayekula njia nzima kila anachokiona ananunua anakula mpaka anakuchafua na ww yan hana ustarabu wengine unakuta hatuna hela mnafanya matumbooo yaumeeee tu mara kuku mara bugger jaman mara eggchops tutakuja tuzimie bure

2.Usiombe ukakaa siti moja na bongeee anakubana anasogea mpaka kwenye siti yako na magar yetu ya masafa marefu siti ndogoo yan unafika homee umechoka maana sio kwa kubanwa kuleee

3.Mtu aliyepuliza marashi utazani harufu ya mochwari yani harufu huingia hadi tumboni na kufanya mvurugano utatamani utapike alafu ukiwa hujala sjui utatapika utumbo hebu tuwe tunachagua marashi yenye harufu za ustaarabu

4.Madereva ambao hawatak watu wachimbe dawa yani nimeshawahi kupanda basi kutoka dar hadi dodoma ndo tukasimama kuchimba dawa mnataka watu tubast vibofuu vya mkojoo au yan dereva amejikausha kama hana akili vizur

5.Abiria wanaong'ang'ania siti za dirishani ukiangalia tiket yake ameandikiwa siti inayoanza sio ya dirishan hawa wanajifanyaga wanatapika kwenye magar unashangaa mnasafir mpaka mmefika hajatapika inaonekana ni mshamba anapenda kuangalia nyumba na miti inavyokimbia

6.Pale unapondondokewa na vibegi na mikoba inayokaa kwenye keria za ndani ya basi alafu mwenyewe anajikausha unabid unyanyuke uweke vizur

Mengine mtaongezaaa nisiwachosheeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kero yangu kubwa ni kufungulia bongo fleva au bongo muvi kwa sauti kubwa. Unafika kichwa kinauma kwa yale makelele. Nyimbo za dini siku hizi nazo zimekuwa za makelele sana. Mbaya zaidi hata ukiweka earphone zinapenya. Bora wawe wanaweka muvi za wanyama mwanzo mwisho.
 
ndio sehemu pekee ninapoangaliaga Bongo Movie (Dar-Mwanza)...
Mara ya mwisho movie ilikiwa mze KIRUNGU, yule muha wa futuhi na Majuto.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
nliwah kuwekwa siti ya watu watatu..mi katikati.dirishani kuna jamaa rasta anatafuna mirungi mkononi kashika fungu. na zile bigijii za pk. anachanganya..ilifika mda bigijii zimejaa mdomoni kam tonge la ugali..alitafuna mpk ubungo
upande wa pili masai kavaa yale mavazi yao ya mashuka..ila jasho lake harufu ile loh!!
nlikoma
 
niliwahi kusafiri na mtu kapagawa na madudu wanampeleka kwa mganga huko bush jamaa wamemtia kamba mikononi na miguuni, then jicho jekundu hatari. mie nilikaa dirishani na wenyewe wakakaa viti viwili vilivyobakia yule mtu aliyepagawa akawa mara anakojoa mara kakata gogo. aisee nachukia kupanda magari ya mkoa ule.
 
Back
Top Bottom