Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Awali wakati matrekta haya yakiletwa kwa mbwembwe tuliambiwa ni kwa ajili ya KILIMO KWANZA. Tukategemea msimu huu wa kilimo wakulima watanufaika kwa kukopeshwa zana hizo muhimu kwa ajili ya kujikwamua ki uchumi. Sasa cha ajabu, mpaka sasa matrekta haya yamekuwa mfano wa maonyesho huria, mwishowe naona nyuki wanaweza kuyageuza mizinga na kufanya maskani yao. Manaake kila nikisafiri kuja Dodoma kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitano nayakuta yako pale pale. Tena kando kando ya barabara iendayo Dar. Kwa yeyote anayefahamu kazi ya haya matrekta hebu atufumbue macho. Kwani msimu wa kilimo ndiyo huu sasa nayo yanazidi kunyeshewa na mvua bila ya kazi. Au yameletwa kwa ajili ya kazi nyingine badala ya kilimo?