Verily Verily
Senior Member
- Jan 4, 2007
- 188
- 143
Miezi michache baada ya rai ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Comredi Adulrahaman Kinana kwa jeshi la polisi kupunguza bugudha kwa magari na hasa maeneo ya mijini, hali imebadilika na taratibu inaanza kujirudia kama ilivyokuwa awali.
Ule unafuu uliokuwa umeanza kupatikana sasa unapotea kwa haraka. Mfano, jijini Dar Es Salaam barabara ya Morogoro utawakuta wanabugudhi madereva pale Urafiki, Kimara Baruti, Kimara Temboni, Kibanda cha Mkaa, kwa Yusufu na maeneo hayo hayana umbali hata wa kilometema 3-5 katikati yake. Na ukiendelea mpaka Maili Moja Kibaha ndipo wamejaa kila umabali wa wastani wa kilometer mbili Luguruni, Kibamba, Kilivya, Maili Moja nk.
Haya ni matumizi mabaya ya pesa za walipakodi kulipa mishahara wafanyakazi wasio na tija au mzigo kwa jamii.
Mdau hebu na wewe ongezea kero unazokutana nazo za hawa watu pamoja na kutakiwa kupunguza bugudha zao.
Mwisho, Je polisi na hasa hawa wa barabarini wako juu ya sheria?