Matokeo ya Serikali za Mitaa: Ni mwanzo wa mwisho wa CCM?! Au ni hasira tuu za Escrow, na Katiba?!

Mkuu naona kama ni hasira tulishakasirika sana ila hatukuchukua hatua
wengi waliishia kutukana lkn sasa tumechoka,kweli huu ni mwanzo wa mwisho wa chama tawala.
Pongezi zangu nazituma kwa m/kiti wa jumuia ya wazazi wa ccmmm aliyewakaripia kwa
jazba walioshindwa kwenye kura za maoni na hawakuvunja makundi yao,badala ya kuongea nao kwa upendo
Amesaidia sana wanaccm wengi kuunga mkono UKAWA.
Tunategemea mshikamano huu uendelee hata chaguzi zijazo.
 
Kiliangukia pale kilipowatupa chini wakulima na wafanyakazi na kukumbatia wafanyabiashara na mafisadi. Sasa hivi ndio wengi wa hawa wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanyakazi wamekuja kujua ukweli kuwa walishatupwa tangu miaka ileee! 2015 CCM hawatoki!
 
Matokeo jumla SM Tabora mjini

Mitaa 130
Ccm 86 - 66%
Cdm 14 - 10%
Cuf 28 - 21%
Nccr 1 - 0.7%
Udp 1 - 0.6%
Vijiji 33
Ccm 32- 97%
Cdm 1 - 3%
Vitongoji 130
Ccm 121- 93%
Cdm 5- 3.8%
Cuf 4- 3.07%
Ushindi jumla
CCM 85.39%
CDM 5.88%
CUF 8.22%
NCCR 0.25%
UDP 0.25%
 
Kwa sasa ninaishi mtaa unaongozwa na CHADEMA hapa Tabora Mjini kwenye kata ya Mpela, Mtaa wa Mpela....... UKAWA OOOOYYYYYYYEEEEEEEEEE!!!!!!
 
Ndoto za Alinacha HIVI ukifikiri Uchaguzi Ungefanyika Wasipate WAPONZANI KURA????
MUHIMU Tusubiri TATHMINI YA Mwisho Tuone Pamoja na Kelele zoote Je Kwa Wilaya, Mkoa na TAIFA wana Asilimia Ngapi????

kinachozungumzwa hapa wewe hukielew,kikubwa hapa ni hata kwa CCM kukosa kura kule walikokua wanashikilia,lakin pia hamasa ya watanzania katika kupiga kura,fanya tathmin ya uchaguz wa S/M uliopita na huu,kwa sasa watu wamehamasika hasaaa si kidogo,pia tilizoea CCM wapo vizuri vijiji,kwa matokeo haya imekuaje???hadi vijijin nako wamekalishwa???
 
Matokeo jumla SM Tabora mjini

Mitaa 130
Ccm 86 - 66%
Cdm 14 - 10%
Cuf 28 - 21%
Nccr 1 - 0.7%
Udp 1 - 0.6%
Vijiji 33
Ccm 32- 97%
Cdm 1 - 3%
Vitongoji 130
Ccm 121- 93%
Cdm 5- 3.8%
Cuf 4- 3.07%
Ushindi jumla
CCM 85.39%
CDM 5.88%
CUF 8.22%
NCCR 0.25%
UDP 0.25%

kwanini idadi ya mitaa iwe sawa na vitongoji wewe mjinga nini
 
Matokeo jumla SM Tabora mjini

Mitaa 130
Ccm 86 - 66%
Cdm 14 - 10%
Cuf 28 - 21%
Nccr 1 - 0.7%
Udp 1 - 0.6%
Vijiji 33
Ccm 32- 97%
Cdm 1 - 3%
Vitongoji 130
Ccm 121- 93%
Cdm 5- 3.8%
Cuf 4- 3.07%
Ushindi jumla
CCM 85.39%
CDM 5.88%
CUF 8.22%
NCCR 0.25%
UDP 0.25%

Haya ni matokeo ya uongo yaliyorushwa hewani kupitia redio uchwara ya Msomali Rage ya VOT. Nimeyasikia na wanasema eti kata ya Gongoni CUF ndo imechukua mitaa yote wakati mtaa wa Zimamoto umechukuliwa na CHADEMA. Kwa kifupi Mitaa yote iliyochukuliwa na UKAWA hapa Tabora ni mitaa wanayokaa vigogo wa CCM na ofisi zao za mkoa na wilaya kwa sasa zipo chini ya utawala wa UKAWA. Kama CCM ingekuwa inapendwa ingeweza kushinda mitaa mikubwa yenye vyanzo vya mapato na rasilimali nyingi.

Ukiangalia CHADEMA na NCCR kwa Tabora hatukuwa na mtaa hata mmoja kwa mwaka 2009 ila ilikuwa ni CUF tu hata hivyo nayo ilikuwa na mitaa michache.

Kwa sasa chini ya UKAWA tumeweza kunyakua sehemu muhimu za mitaa katikati ya mji kwa sasa CCM ni chama pinzani. Nipo nakusanaya Takwimu ili nije na taarifa sahihi sio kama hiyo iliyorushwa na Local Radio ya Msomali.

Mtaa wenye wapiga kura 1167 wa Mpela katika kata ya Mpela kwa sasa ipo mikononi mwa CHADEMA......

Stay tuned nitakuja na takwimu sahihi kesho..........
 
Wanabodi,


kushinda ni kushinda tuu hata kama ni mtaa mmoja!, hii ni sweet victory!.

Na kushindwa ni kushindwa tuu, hata kama ni mtaa mmoja, kunauma!.

The winner takes it all, the looser standing small!.

Hongereni Washinda!,

Poleni Washindwa!.

Pasco.

(Sina Chama, sina Upande!)

Jamii forums inapata heshima kwa maandiko objective kama haya. Uchaguzi huu ni bonge ya message kwa watawala,
 
Kawe ccm tumechukua

Mmechukua kihalali au mmechakachua? Mabomu yote ya jana usiku yalikuwa ya nini? Watu kuhama mitaa na kwanda kupiga kura mtaa wa pili ndio ushindi gani huo? Tena wakiongozwa na wasimamizi wa uchaguzi unaingia tu chumbani unapewa karatasi ukapige kura bila hata kuhakikiwa jina lako. Unarudi nyumbani unabadilisha gauni unarudi kituoni kupiga kura mara ya pili! Wengine walienda saloon kuseti nywele wengine kwa vinyozi kunyoa nywele na ndevu wakazungukia kupiga kura mitaa tofauti kutwa nzima. Ni aibu. Shinda kwa kupiga kura kistaarabu. Na hao wasimamizi waliowabebeba CCM walaaniwe kwa sababu hawakutenda haki. Utauliza kwani wakala alikuwa wapi. Kwa mazingira niliyoyaona walikuwa wanaingiza watu zaidi ya mmoja chumbani sasa mara huyu anatafutiwa jina kwenye daftari na huku mwingine anapewa karatasi zaid ya tatu kwenda kujaza! Ni maajabu na kweli na tulivyostuka muda wa saa sita mamluki walishapiga kura nyingi tu.
 
Uchaguzi wa mitaa ni kipimo cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,matokeo haya CCM 2015 bado wataendelea kushikilia Ikulu. Tulipo fikia sasa sio kukua kwa upinzani ni kuchukua nchi 2015 lakini kwa matokeo haya ni bahati mbaya CCM inaendelea kuwepo 2015 na kuongoza nchi
 
Maumivu ya kichwa huanza polepole......badae unaskia maumivu makali kupita kiasi.... Mwalikumbuka tangazo hili
 
Matokeo jumla SM Tabora mjini

Mitaa 130
Ccm 86 - 66%
Cdm 14 - 10%
Cuf 28 - 21%
Nccr 1 - 0.7%
Udp 1 - 0.6%
Vijiji 33
Ccm 32- 97%
Cdm 1 - 3%
Vitongoji 130
Ccm 121- 93%
Cdm 5- 3.8%
Cuf 4- 3.07%
Ushindi jumla
CCM 85.39%
CDM 5.88%
CUF 8.22%
NCCR 0.25%
UDP 0.25%
Tabora mjini kuna vijiji na vitongoji? Haishangazi hata hivyo, wanasema mzigo mzito mtwishe mnyamwezi. Wacha wabebane na liccm lao.
 
Hahahaaa, AJUZA FaizaFoxy kajificha mbali kabisa na anaingia JF bila ku-Log in.

Najua akipita hapa atacheka na kusema "**** ***** zenu leo hamnioni ng'o!!!"

Nafurahi tu kitu kimoja, hatimaye Warioba amekenua meno kwa kicheko.

Ila siyo siri, katika WATANI ninaowaheshimu, FF ni mpinzani kwelikweli. Atatumia mbinu zote kuzuia makombora huku na yeye akituma yake. Ajuza atakuwa na shule yake nzuri tu huyu maana ubishi wake huwa umetulia. RESPECT to Bi Kungwi.

Hivi akina Faiz Fox wako wapi jamani watani zetu hawa ama ndo pumu zimeshaanza.. loh!
 
Back
Top Bottom