Matokeo mabaya kidato cha 4 2012 majibu haya

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Feb 25, 2013
1,459
697
Mihtasari ya elimu na kufeli kwa wanafunzi mwaka 2012 Tanzania
Watu katika makundi mengi Tanzania wamezungumza sana na kwa kipindi kirefu sasa, kuhusu kila wanachokiita kushuka kwa elimu. Wanasema ukiona wanafunzi wamefaulu sana, elimu hiyo ni nzuri. Kwa sasa wanafunzi wamefeli, hivyo elimu imeshuka.

Chanzo kimoja cha tatizo hilo wanasema ni mihtasari wanayoiita mipya ya mwaka 2005 kuwa ni mibovu, kwa hiyo ibadilishwe. Wengine wanasema ifanywe semina ili walimu wawe na uwezo wa kuitumia shuleni vizuri. Mihtasari ya mwaka 2005 sio mipya. Kutoka mwaka 2005 hadi 2013 imepita miaka nane sasa.

Wadau wengi wa elimu kusema mihtasari hii inahitaji warsha au semina kwa walimu wanaofundisha shuleni, hicho sio kitu cha muhimu kwa sasa. Mihtasari hiyo ilipotoka mapema mwaka 2005, suala la kufanya warsha kwa walimu lilijadiliwa katika mikutano ya mwaka ya wakuu wa shule pia na katika vikao mbalimbali vya makundi ya walimu.

Katika vikao hivyo walisema mihtasari mipya ya mwaka 2005 ifanyiwe semina au warsha kwa walimu. Kipindi hicho neno upya wa mihtasari lilikuwa sahihi. Lakini leo mwaka 2013 kusema mihtasari mipya ya mwaka 2005 ifanyiwe semina ni kuonyesha kuwa bado hatujatambua tatizo. Tujue kuwa kutoka mwaka 2005 hadi mwaka huu 2013 walimu wanaohitimu mafinzo ya ualimu wanakuwa wamejifunza namna ya kutumia mihtasari hiyo. Katika kipindi hicho pia viongozi wa elimu wamekuwa wanatembelea shule na kujadili mihtasari hiyo hiyo pia. Kujadili ni mafunzo. Kwa hiyo, mawazo yanayopelekea kuona kuwa warsha au semina zitawasaidia walimu kuweza kutumia mihtasari ya mwaka 2005 sio sahihi sasa.

Matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka 2012 yamewafanya watu wengine wakubaliane na hoja zinazosema kuwa mihtasari ni mibovu na elimu imeshuka. Watu hawa wanasahau kuwa matokeo mabovu peke yake hayawezi kuwa kipimo cha elimu. Mitihani ni mke wa mihtasari. Mitihani mizuri inaweza kupima tu kama mihtasari imefundishwa. Kama mitihani inaonyesha kuwa wanafunzi wamefaulu mitihani husika, hii itaonyesha tu kuwa wanafunzi walifundishwa mihtasari hiyo na sio kuwa wanafunzi hao wana IQ ya juu. Kunahitajika pia vipimo vya elimu katika maisha ya kikazi na kijamii ili kujua uzuri wa elimu inayotumika.

Mawazo ya watu wanaosema mihtasari ibadilishwe kutokana na kushuka kwa ufaulu mwaka 2012 hayana sababu ya kuharakishwa. Mabadiliko haya yafanyike tu, pale utafiti utakapoonyesha kuwa mihtasari iliyopo haina uhusiano na maisha halisi ya watanzania. Kufeli kwa wanafunzi kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 kufanyiwe uchunguzi tu, ili kubaini yalikubwa na tatizo gani. Kwa sababu mitihani sio elimu.

Kuna tatizo la kuchanganya vitu baada ya wanafunzi kufeli mitihani ya mwaka 2012. Kama hatutachambua kwa makini na kutambua matatizo hasa ni yapi na ni kwa namna gani tutayatatua ipasavyo, itasababisha serikali kutumia fedha nyingi bila kupata ufumbuzi.
 
Acha kutudanganya wewe mihtasari ya mwaka 2005 iliacha kutumika 2009, kuna mihtasari ya mwaka 2010.
 
Tume iliyoundwa kuchunguza tatizo ndio ina majibu na sehemu ya majibu tayari yameishatolewa na sehemu ya hayo majibu yanafanyiwa kazi na serikali, nje ya hapo ni stori za vijiweni.
 
Ni kweli mkuu hajui kuna mihtasari ya mwaka 2010.kwa kuongezea ni kwamba vitabu vinavyotumika huko shuleni ni vurugu tupu mfano kidato cha 4 Geography kila shule vitabu wanavyotumiavinatofautiana.
 
mihtasari ya elimu na kufeli kwa wanafunzi mwaka 2012 tanzania
watu katika makundi mengi tanzania wamezungumza sana na kwa kipindi kirefu sasa, kuhusu kila wanachokiita kushuka kwa elimu. Wanasema ukiona wanafunzi wamefaulu sana, elimu hiyo ni nzuri. Kwa sasa wanafunzi wamefeli, hivyo elimu imeshuka.

Chanzo kimoja cha tatizo hilo wanasema ni mihtasari wanayoiita mipya ya mwaka 2005 kuwa ni mibovu, kwa hiyo ibadilishwe. Wengine wanasema ifanywe semina ili walimu wawe na uwezo wa kuitumia shuleni vizuri. Mihtasari ya mwaka 2005 sio mipya. Kutoka mwaka 2005 hadi 2013 imepita miaka nane sasa.

Wadau wengi wa elimu kusema mihtasari hii inahitaji warsha au semina kwa walimu wanaofundisha shuleni, hicho sio kitu cha muhimu kwa sasa. Mihtasari hiyo ilipotoka mapema mwaka 2005, suala la kufanya warsha kwa walimu lilijadiliwa katika mikutano ya mwaka ya wakuu wa shule pia na katika vikao mbalimbali vya makundi ya walimu.

Katika vikao hivyo walisema mihtasari mipya ya mwaka 2005 ifanyiwe semina au warsha kwa walimu. Kipindi hicho neno upya wa mihtasari lilikuwa sahihi. Lakini leo mwaka 2013 kusema mihtasari mipya ya mwaka 2005 ifanyiwe semina ni kuonyesha kuwa bado hatujatambua tatizo. Tujue kuwa kutoka mwaka 2005 hadi mwaka huu 2013 walimu wanaohitimu mafinzo ya ualimu wanakuwa wamejifunza namna ya kutumia mihtasari hiyo. Katika kipindi hicho pia viongozi wa elimu wamekuwa wanatembelea shule na kujadili mihtasari hiyo hiyo pia. Kujadili ni mafunzo. Kwa hiyo, mawazo yanayopelekea kuona kuwa warsha au semina zitawasaidia walimu kuweza kutumia mihtasari ya mwaka 2005 sio sahihi sasa.

Matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka 2012 yamewafanya watu wengine wakubaliane na hoja zinazosema kuwa mihtasari ni mibovu na elimu imeshuka. Watu hawa wanasahau kuwa matokeo mabovu peke yake hayawezi kuwa kipimo cha elimu. Mitihani ni mke wa mihtasari. Mitihani mizuri inaweza kupima tu kama mihtasari imefundishwa. Kama mitihani inaonyesha kuwa wanafunzi wamefaulu mitihani husika, hii itaonyesha tu kuwa wanafunzi walifundishwa mihtasari hiyo na sio kuwa wanafunzi hao wana iq ya juu. Kunahitajika pia vipimo vya elimu katika maisha ya kikazi na kijamii ili kujua uzuri wa elimu inayotumika.

Mawazo ya watu wanaosema mihtasari ibadilishwe kutokana na kushuka kwa ufaulu mwaka 2012 hayana sababu ya kuharakishwa. Mabadiliko haya yafanyike tu, pale utafiti utakapoonyesha kuwa mihtasari iliyopo haina uhusiano na maisha halisi ya watanzania. Kufeli kwa wanafunzi kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 kufanyiwe uchunguzi tu, ili kubaini yalikubwa na tatizo gani. Kwa sababu mitihani sio elimu.

Kuna tatizo la kuchanganya vitu baada ya wanafunzi kufeli mitihani ya mwaka 2012. Kama hatutachambua kwa makini na kutambua matatizo hasa ni yapi na ni kwa namna gani tutayatatua ipasavyo, itasababisha serikali kutumia fedha nyingi bila kupata ufumbuzi.
aaaaaa! Acha bana.
 
Back
Top Bottom