Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Biharamulo waishtukia CCM -MAJIRA
Wednesday, 08 July 2009 06:32
Na Suleiman Abeid, Kagera

SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuibuka na ushindi kiduchu katika uchaguzi
mdogo jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera, baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wamelalamika na kudai kuwa chama hicho kina ajenda ya siri ya kuua demokrasia ya vyama
vingi vya siasa nchini.

Wakazi hao wametoa kauli hiyo kutokana na kile walichodai uendeshaji wa kampeni za CCM uliofanywa maeneo mbalimbali na viongozi wake na hotuba za makada wake zilizoonesha wazi kuwa chama hicho hakikubaliani na mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

“Kwa kweli inaelekea chama tawala hivi sasa hakitaki tena nchi hii kuendeshwa chini
ya mfumo wa vyama vingi kutokana na jinsi vigogo wa chama hicho walivyokuwa
wakituhutubia katika mikutano yao ya kampeni, walieleza wazi kuwa iwapo tutamchagua
mbunge kutoka upinzani hatutapata maendeleo,”

“Hizi kauli kwa kweli zilitushitua watu wengi, na hata baadhi yetu tuliona hakuna
haja ya kwenda kupiga kura kwa maana ni wazi kuwa tuliamini iwapo tutamchagua
mgombea tunayemtaka lakini anatoka katika chama cha upinzani, basi tutakuwa
tumejinyima maendeleo,” alieleza Bi. Victoria Modest mkazi wa mjini Biharamulo.

Bi. Modest alisema Serikali ya CCM imeonesha udhaifu mkubwa katika kuvumilia mfumo
wa vyama vingi hapa nchini na kwamba haikuwa busara kutumia 'fimbo' ya kuwanyima
wananchi wake maendeleo kwa kigezo tu kuwa wamemchagua mbunge kutoka chama cha
upinzani.

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Kabindi kata ya Runazi, Bw. Steven Barikwegonza
alisema umefika wakati wa viongozi wa CCM waamue bila ya woga kufuta mfumo wa vyama
vingi nchini kutokana na kuonekana wazi kuwa wameshindwa kuvivumilia vyama vingine
vya siasa hapa nchini.

“Hebu ndugu mwandishi fikiria kauli ambazo zilikuwa zikitolewa na mheshimiwa Makamba
(Yusufu Makamba) Katibu Mkuu wa CCM Taifa, alisema wazi eti wakazi wa Biharamulo
tulifanya makosa makubwa mwaka 2005 kuchagua mbunge kutoka chama cha upinzani, na
hii ndiyo sababu ya kukosa kwetu maendeleo,”

“Alitueleza wazi kuwa safari hii tusirudie kosa iwapo shida yetu ni maendeleo, sasa
hii haiingii akilini, iweje wananchi ambao ndiyo tunaolipa kodi inayoendesha nchi
hii bila kujali mlipaji anatoka chama gani cha siasa, sasa inapofika wakati wa
kuchagua viongozi tupangiwe watu wa kuwapigia kura tena ni wale wa kutoka CCM?,”
Alihoji Bw. Barikwegonza.

Bw. Barikwegonza alishauri kuwa iwapo hivi sasa wananchi hawatakiwi kuwapigia kura
wabunge ama madiwani kutoka vyama vya upinzani ni vizuri CCM ikapeleka mswada
bungeni ili kuufuta rasmi mfumo wa vyama vingi, vinginevyo hakuna haja ya kuendelea
kuendesha chaguzi ambazo hazina tija.

“Tazama kila kinapofika kipindi cha uchaguzi serikali inatenga fungu la fedha kwa
ajili ya kuendeshea shughuli hiyo, lengo ni kutoa nafasi ya demokrasia kwa wananchi
wa Tanzania kuchagua viongozi wanaowataka na wanaoamini kuwa watawafanyia kazi,
lakini CCM wanasema mkichagua upinzani hakuna maendeleo, uchaguzi wa nini sasa?”
Alihoji.

Kwa upande mwingine wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
wamelalamikia kile walichodaiwa kitendo cha ‘kupokwa’ kwa ushindi walioupata katika uchaguzi huo na wanaamini kuwa mgombea wa chama chao, Bw. Mbasa Gervas ndiye
aliyeshinda .

Wanachama hao waliungana na viongozi wao wa kitaifa kudai kuwa CCM ilishinikiza
mgombea wake Bw. Oscar Mukasa kutangazwa kuwa mshindi japo walielewa alishindwa katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 16,682.

Walidai kuwa mgombea wao wa CHADEMA katika uchaguzi huo alipata kura
17,313 na yule wa TLP kuambulia kura 187 matokeo ambayo hata hivyo yalikataliwa na
msimamizi wa uchaguzi na kuzua mtafaruku mkubwa kutoka kwa viongozi wa CHADEMA.

Viongozi hao walidai kuwa matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi Bw. Zubeir Mbiana yalikuwa 'yamepikwa' huku wakidai kuwepo njama katika vituo tisa vya kata ya Nyarubungo.

Katika uchaguzi huo mgombea wa CCM Bw. Mukasa alitangazwa mshindi kwa kupata
kura 17,561 sawa na asilimia 50.9, wakati Bw. Gervas wa CHADEMA alipata kura 16,700
sawa na asilimia 48.46 na mgombea wa TLP aliambulia kura 198 sawa na asilimia 0.6.
 
Hiyo ndo ccm bwana, ukiishinda kwa kura inakaa mezani. Hapo bwana huna ujanja lazima itakutoa k.o (knock out) tu. Mimi bado siamini kama ccm ilishinda jimbo la busanda na pia sishangai kuiona imenyakua jimbo la biharamulo kwa sababu ni wezi wa kura.
 
Hiyo ndo ccm bwana, ukiishinda kwa kura inakaa mezani. Hapo bwana huna ujanja lazima itakutoa k.o (knock out) tu. Mimi bado siamini kama ccm ilishinda jimbo la busanda na pia sishangai kuiona imenyakua jimbo la biharamulo kwa sababu ni wezi wa kura.
Mkakati huo ulipangwa mapema mara mahakama kuu ilipotengua ubunge wa Marehemu Kabuye.Mkakati ni hivi watumishi wa idara ya usalama wa Taifa wakishirikiana na Tume ya Uchaguzi, walianza kuvuruga majina ya wapiga kura na kuhakikisha kuwa watakaopiga kura wawe ni wale wenye muelekeo wa kupigia CCM.Hiyo idadi ndogo inayojitokeza isikushangaze wapanga mikakati wa CCM ndio walitaka wapige kura.Majina ya wale wenye msimamo usiotabirika, majina yao yalikuwa hayaonekani kwenye vituo walivyojiandikisha.
 
Back
Top Bottom