Matokeo Arusha sio mazuri kwa mabadiliko

chadema ni chalenger tu si champion bado hawajakubalika na watanzania bali ni wanywa viroba na waendesha bodaboda tu
Hizi kauli wenzako ndani ya CCM washaona hazina maana,huoni wale vijana mliokuwa mnawaita wahuni na si wapigaji kura siku hizi munawanyenyekea mpk munawapunguzia ushuru katika bodaboda,wewe bado unawaita wanywa viroba?inawezekana kweli wanakunywa viroba lkn likifika suala la kupiga kura hawakosei kudumbukiza karatasi zao upande stahiki na CCM wanabaki wameduwaa......acha kebehi mambo ndani ya Tanzania yanabadilika kila kukicha.
 
mbona umeshindwa kutwambia kuwa hali ya kila chema kabla ya kwenda kwenye uchaguzi? umesahau kuna vitu vina sababisha mtu marks zake zipungue hata kama akiwa kajiandaa vipi kwa mtihani.

Kwakweli kwa haraka huu ni ushindi mkubwa sana kwa chadema kwa magumu na hujuma walizopitia. hakika na kuhakishia kuwa kwa hujuma walizo fanya ccm kwanza kwa watu walio jitokeza ni wazi jamii uoga umeanza kuisha kabisa.

Ulitakiwa ufanye mlingano wa mambo walio pitia hao watahiniwa wawili kabla ya mtihani.
 
ulichokisema ni kweli hata mimi nimeliona hilo kuwa tofauti imekuwa ni ndogo sana tofauti na tulivozoea na matarajio ya watu wengi, lakini point ya msingi uchaguzi wa arusha kwa mda huu umekubwa na misukosuko mingi ambayo ilipelekea akina nchemba kuwatoa kafara watu kadhaa ili washinde na bado hawajafanikiwa, lazima ujue katika huu mtanange kuna challenger , l eader na follower , kwa mtazamo huu naona nikupe kazi ya kuendelea kufikiria nani alikuwa katika position gani. a single drop can lead to colour change.
 
nikiwa kama mmoja wa wapenda mabadiliko nashangazwa sana na matokeo ya Arusha muda huu'tulitegemea ccm kupata chini ya asilimia 10 ya kura zote'nikienda kwenye point moja kwa moja ni kwamba kama Arusha yenye watu walioamka kiasi hiki wameweza kupigia ccm kura nyingi kiasi hiki je mikoa ambayo bado imelala itakuwaje?
Sijui kama unaweza kutafakari na kuelewa ninachojaribu kuweka hapa'nafikiri kazi ni kubwa mno iliyo mbele yetu kwani kama Arusha ccm wameweza kupata kura nyingi hivi je 2015?itakuwaje'natoa wito kwa wapenda mabadiliko wote tuungane kwa hali na mali kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwa mikoa yote'kwa kweli 2015 kuongozwa tena na ccm ni kuleta maangamizi zaidi kwa taifa letu
Unaweza kuwa na wasiwasi lakini si kama unavoona kwa kura hizo walizopata CCM unataliwa ujue ni kwamba wameiba kwa nguvu zote lakini hazikutosha
 
nikiwa kama mmoja wa wapenda mabadiliko nashangazwa sana na matokeo ya Arusha muda huu'tulitegemea ccm kupata chini ya asilimia 10 ya kura zote'nikienda kwenye point moja kwa moja ni kwamba kama Arusha yenye watu walioamka kiasi hiki wameweza kupigia ccm kura nyingi kiasi hiki je mikoa ambayo bado imelala itakuwaje?
Sijui kama unaweza kutafakari na kuelewa ninachojaribu kuweka hapa'nafikiri kazi ni kubwa mno iliyo mbele yetu kwani kama Arusha ccm wameweza kupata kura nyingi hivi je 2015?itakuwaje'natoa wito kwa wapenda mabadiliko wote tuungane kwa hali na mali kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwa mikoa yote'kwa kweli 2015 kuongozwa tena na ccm ni kuleta maangamizi zaidi kwa taifa letu
Katika analysis yako ungeweka na idadi ya waliojitokeza kupiga kura kama asilimia ya wapiga kura wote.

CCM ilijenga hofu miongoni mwa wana Arusha kwa namna nyingi, IKIWEMO YA MLIPUKO WA BOMU, na uwezekano mkubwa ni kuwa watu kujitokeza kwa uchache kumepunguza gap la ushindi wa mshindi.

Lakini pia kuna kundi linalofaidi uwepo wa hawa CCM. Watu kama akina Mulongo na kikosi chake, mafisadi wakubwa na nguvu yao ya fedha ya hata kuhonga watu. Hivyo mimi bado naona ushindi huu ni mkubwa sana kwa Chadema.

Hata hivyo nashkuru kwa angalisho na kutobweteka na ushindi na kukaza buti kuendelea na kazi.

All in all, Ushindi wa zaidi ya 70% ni ushindi wa kishindo kwa kigezo chochote kile.
 
this is fallacy argument....unapokutoa analysis ya jambo lazimu utazame context....CDM katika uchaguzi huu imepita katika majaribu ambayo naweza sema hawajawahi pina na hawakuwahi fikiria kama pana siku wanaweza pitia. kitendo cha mlipuko wa bomu kwenye kampeni zake kitazamwe kwa jicho la tatu kwani kuna watu waliamini kuwa yawezekana ni CDM ndiyo wamefanya hili.....fikilia kampeni chafu za ccm mpaka jana wakiwa na lengo baya zaidi ambalo yamkini halijawahi tokea pia la kuwahamasisha malwaigwana kutoa matamuko kuwa wachaga wanatuaribia jiji letu.....kumbuka hawa wazee wanaheshimika sana arusha....tamko lao limeathri mambo mengi.......mkuu think twice before u twite:yield:

There is no fallacy at all! Anachokisema mwenzako kuna mantiki! Kwa nguvu ya CDM Arusha, hata hicho kidogo cha CCM hakikupashwa! Anatahadhalisha kufanya nguvu zaidi from today to 2015. Nadhani ana nia njema na mageuzi!
 
nikiwa kama mmoja wa wapenda mabadiliko nashangazwa sana na matokeo ya Arusha muda huu'tulitegemea ccm kupata chini ya asilimia 10 ya kura zote'nikienda kwenye point moja kwa moja ni kwamba kama Arusha yenye watu walioamka kiasi hiki wameweza kupigia ccm kura nyingi kiasi hiki je mikoa ambayo bado imelala itakuwaje?
Sijui kama unaweza kutafakari na kuelewa ninachojaribu kuweka hapa'nafikiri kazi ni kubwa mno iliyo mbele yetu kwani kama Arusha ccm wameweza kupata kura nyingi hivi je 2015?itakuwaje'natoa wito kwa wapenda mabadiliko wote tuungane kwa hali na mali kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwa mikoa yote'kwa kweli 2015 kuongozwa tena na ccm ni kuleta maangamizi zaidi kwa taifa letu

Nahisi kama huyu ni Juliana Shonza !
 
UMEANGALIYA HAYA KABLA YA KUANDIKA.
1.vijana wengi ni washabiki na wanachama wa chadema.
2.wengi wa vijana wakereketwa wa chadema walikuwa chini ya umri wa mpiga kura 2010 hivyo hawakujiandikisha(si wapiga kura mpaka sasa)
3.vijana wengi waliokuwa na sifa ya kupiga kura 2010 hawakujiandikisha kwa sababu ya mwamko mdogo(mpaka sasa pia si wapiga kura)
4.vitambulivyo vingi vya kupigia kura vimeharika ama kupotea.
5.chadema hawahongi(wanatumia ushawishi wa kidemokrasia)
6.mwigulu+ccm+polisi+serikali=ubinyaji na ukiukaji wa demokrasia,(no balanced game)
7.vtisho vya ccm,siasa ovu juu ya amani inatupunguzia kura kwa kinamama wengi na wazee ambao kimsing ni rahisi kutishika na ni ngumu kuwashawishi.
8.umeangalia kama tunapiga hatua ama laa?Mfano uchaguzi wa darajambili(arusha) mwaka jana 2012,ccm ilipoteza kata yake iliyoshinda 2010,cdm=zaidi ya 1800,ccm=900,cuf=200.
9.zaidi ya 90% ya wapiga kura wa sasa walikuwa wanachama ama washabiki wa ccm miaka 3 iliyopita,hivyo hata ccm wanabadilika na wanatupa kura.
 
Nikiwa kama mmoja wa wapenda mabadiliko nashangazwa sana na matokeo ya Arusha muda huu'tulitegemea ccm kupata chini ya asilimia 10 ya kura zote'nikienda kwenye point moja kwa moja ni kwamba kama Arusha yenye watu walioamka kiasi hiki wameweza kupigia ccm kura nyingi kiasi hiki je mikoa ambayo bado imelala itakuwaje?

Sijui kama unaweza kutafakari na kuelewa ninachojaribu kuweka hapa'nafikiri kazi ni kubwa mno iliyo mbele yetu kwani kama Arusha ccm wameweza kupata kura nyingi hivi je 2015?itakuwaje'natoa wito kwa wapenda mabadiliko wote tuungane kwa hali na mali kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwa mikoa yote'kwa kweli 2015 kuongozwa tena na ccm ni kuleta maangamizi zaidi kwa taifa letu
Unaweza kuwa sahihi lakini kulingana na joto la Arusha lilivyokuwa Chadema walihitaji kushinda hata kwa tofauti ya kura 1 tu kama wewe ni mgeni kwenye siasa za Arusha CDM wana next step inayotakiwa kufuatwa baada ya kushinda viti vyote 4 (i.e issue ya meya feki) Aidha ukumbuke kuwa kwa siasa zilivyokuwa Arusha na mashambulio ya mabomu wapiga kura wengi hawakujitokeza zaidi ya wale wenye roho ngumu. Jaribu kujiridhisha walioandikishwa kila kata ni wangapi na waliopiga kura ni wangapi. Inshort CDM wako strategic na smart zaidi ya magamba katika mambo yao. Japo ieleweke kuwa sidharau ushauri wako uliotoa.
 
Nikiwa kama mmoja wa wapenda mabadiliko nashangazwa sana na matokeo ya Arusha muda huu'tulitegemea ccm kupata chini ya asilimia 10 ya kura zote'nikienda kwenye point moja kwa moja ni kwamba kama Arusha yenye watu walioamka kiasi hiki wameweza kupigia ccm kura nyingi kiasi hiki je mikoa ambayo bado imelala itakuwaje?

Sijui kama unaweza kutafakari na kuelewa ninachojaribu kuweka hapa'nafikiri kazi ni kubwa mno iliyo mbele yetu kwani kama Arusha ccm wameweza kupata kura nyingi hivi je 2015?itakuwaje'natoa wito kwa wapenda mabadiliko wote tuungane kwa hali na mali kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwa mikoa yote'kwa kweli 2015 kuongozwa tena na ccm ni kuleta maangamizi zaidi kwa taifa letu

Unasahau kuwa kuna
1. hofu ya bomu
2. Mabalozi kuandikisha namba za kadi za kura
3. Wapiga kura kuyakosa majina vituoni.
4. Daftari la wapiga kura kutoboroshwa toka 2010, hivyo kimsingi wale wote waliopokea mabadiliko toka 2010 hd leo, maelfu ya vijana, hawapigi kura.

Hivyo usitarajie tofauti kubwa ya ushindi.
 
Nikiwa kama mmoja wa wapenda mabadiliko nashangazwa sana na matokeo ya Arusha muda huu'tulitegemea ccm kupata chini ya asilimia 10 ya kura zote'nikienda kwenye point moja kwa moja ni kwamba kama Arusha yenye watu walioamka kiasi hiki wameweza kupigia ccm kura nyingi kiasi hiki je mikoa ambayo bado imelala itakuwaje?

Sijui kama unaweza kutafakari na kuelewa ninachojaribu kuweka hapa'nafikiri kazi ni kubwa mno iliyo mbele yetu kwani kama Arusha ccm wameweza kupata kura nyingi hivi je 2015?itakuwaje'natoa wito kwa wapenda mabadiliko wote tuungane kwa hali na mali kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwa mikoa yote'kwa kweli 2015 kuongozwa tena na ccm ni kuleta maangamizi zaidi kwa taifa letu

Subiri daftali la wapiga kura liboreshwe na tume huru ya uchaguzi ndiyo utajua hii tathmini yako kimeo!!
 
Naendelea...
10.toka uchaguzi 2010,hakuna kata tuliyopokonywa na ccm
11.si watu wote ni wapenda mabadiliko
12.si watu wote wanaupeo wa kuelewa na kufanya maamuzi sahihi,mfano mpaka leo kuna wav walishaapa kutopiga kura,wapo wanaopanga foleni kwenda kuharibu kura zao makusudi
13.rusha na hongo wanaihimili wachache,ndio mana kwa kutambua hilo tunafanya kila liwezekanalo kutotoa mwanya kwa ccm kuhonga wapiga kura mana wakifanikiwa hata washabiki wetu wengi watachagua kupigia rushwa,na tambua mtego huu kuna watu umewanasa,
14.mpaka sasa wapiga kura wanaopiga kura ni chini 40%.
SASA MAAJABU UNAYOYATAKA NI BAADA YA DAFTARI LA KUDUMU KUFANYIWA MAREKEBISHO,na kujiridhisha kuwa waliopiga kura ni wachache mno chini ya watu 10,000 katika kata nne zenye population ya malaki ya watu.
Angalia population detail za sensa
 
Ba hapo Hamna marekebisho ya daftari la wapiga kura.waliovote 2010 ndo haohao.mwanZisha mada aone hili
 
Mleta thread,bado una hofu baada ya kusoma maelezo ya wadau wengi?Nasubiri majibu,
Ushauri wako na matokeo ya leo ni kitu ambacho nakijua toka mwaka jana,na ushauri wangu kwa sasa CHADEMA walekeze nguvu zao kubwa kuwaandaa vijana walio wengi wakae tayari kujiandisha pindi TENDWA atakapoanza kurekebisha daftari la kudumu,I AM CONFIDENT 2015 ccm will score less than 38% of total votes under balanced game,if not a balanced game still ccm is going to lose the battle.
 
Ni mtazamo mzuri CDM ijipange kukabiliana na nguvu ya dola na uwizi wa kura na mbinu chafu. Naamini hilo limeonekana ndio maana Mwema na Kikwete wameanza kupiga mayowe CDM isijipange kujilinda.
 
Back
Top Bottom