lyinga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2013
- 2,496
- 1,035
Huwa natatizika sana naposikia viongozi wetu wanasafiri all the way kutoka Tanzania mpaka Marekani au nchi nyingine yoyote ya Ulaya kwa ajili tu ya kuchunguzwa afya. Huwa najiuliza hivi madaktari wetu wa waliosomea hapahapa nchini hawawezi kufanya hiyo kazi? Kama hawawezi basi kwa maoni yangu ni wakati muhimu wa kuwawezesha ili waweze kuifanya hiyo kazi na ili kupunguza gharama za kwenda nje ya nchi.
Wala usisikitike kwanza ngoja nikutoe tongotongo kwanza unajua ni nani aliziuwa zile shule za vipaji maalumu?
Na nisababu zipi wakati wale viongozi na maprofesa, ma dr , mainjinia wa enzi hizo sio hawa wa dot.com ndio hizo shule ziliwatoa?
Pili unajua kuanzishwa kwa hizi shule binafsi ambazo kwa asilimia kubwa hakuna kiongozi wa sasa awaye yeyote mtoto ama mjukuu au kitukuu ndio wanaosoma shule hizo?
Na hizi za hali ya chini ukiunganisha za kata na hizi za serikali ambazo hazina tena nuru ile iliyokuwako miaka ya 90 kushuka chini ndizo wanazosoma watoto wa makabwela? Sasa hapo unataka kuniambia kuna kiongozi gani anayeweza kuzithamini hizi shule zetu makabwela wakati hapa kati pameshawekwa tabaka jibu unalo.
Tatu twende mahospitalini asilimia kubwa ya viongozi tuliokuwa nao sasa wengi wanatibiwa nje na familia zao , atakuwaje na uchungu au kizithamini hizi zetu huku makabwela tunazo lala kitanda kimoja wagonjwa wawili ?
Hapo jibu unalo sasa wapendwa nanukuu kwenye maandiko Matakatifu imeandikwa unapoona mmoja wenu anawakwaza ni heri kumfunga jiwe kubwa shingoni na kumtosa baharini ,
Na jiwe lenyewe ni hili kwa wale ambao hamjajiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura siku ikifika shime tuende wote kuhakiki na kujiandikisha kwenye hilo daftari,
Ili ifikapo october tuweze kwa umoja tuweze kuwafunga jiwe kubwa hawa waliotukwaza mpaka tukawa kama yatima na kuishi kama wakimbizi kwenye nchi yetu wenyewe , yenye kila neema na baraka za Mungu tuwatupe baharini nayo ni kura yako ndio mkombozi wako na kizazi kijacho leo tupo kesho hatupo,
Shime wapendwa hakuna linaloshindikana chini ya jua na kwa pamoka twaweza Mungu ibariki Tanzania.