Matibabu ya viongozi nje ya nchi - Aibu kwa Tanzania!

Aliyekuwa awe mrithi wa kiti cha ufalme Saudi Arabia alifia hospitalini New York.

Kwahiyo ukiwa kiongozi ni lazima ukatibiwe nje nchi? Mimi na wewe je? Kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa karibia viongozi wote wa nchi yetu hakukusikitishi wewe?
Hasa ukiangalia huduma za afya zilivyodorora?
Sijui mwenzetu unaishi hapa au uko wapi?!
 
Tatizo hilo ni la kujitakia na ni la kihistoria. Fikra hata za waasisi wetu ambo kwao uhuru ni pamoja na kurithi vyeo, tabia, na hulka za watawala wa kikoloni...tofauti ni rangi tu! hata nyerere enzi zake licha siasa yake ya ujamaa na kujitegemea, alikuwa anakwenda majuu kupata huduma za uchunguzi na tiba. Ufumbuzi ni wananchi kukomaa ili kuwashinikiza viongozi wajione kuwa ni sehemu ya jamii hii, na hivyo wanapokumbwa na matatizo wayatatue kwa kutumia raslimali hizihizi ambazo wengi tunazitegemea..km rufaa basi iwe ya haki. Tabia ya viongozi kwenda ulaya kutibiwa hata mafua tu inakera sana!
 
Kwa mwendo huu kuboresha huduma za afya ni vigumu maana viongozi wana uhakika wa kupata huduma bora nje ya nchi, sisi wananchi tutaishia kwa akina kalumanzila
 
Guys we reap what we sow. Hatukuona sababu ya kujari na kuendelea vile vilivyo vya kwetu. Leo tumekosa karibu yote na tumekuwa wageni wa watu wengine. Imagine tuna Lugalo,muhimbili, KCMC na nyingine nyingi. Twendeni tukaone kwenye hizi hospitali zetu kuna nini. Hii hela tunayolipa India tungeweza kuziboresha hizi hospitali zikasaidia watu wengi zaidi.
 
inabidi muwe kwenye system ya afya kuelewa haya maamuzi.kiukweli tupo nyuma kwa vitu vingi kuanzia vipimo mpaka dawa.unaweza ukaleta vifaa vya kisasa ukakosa mtu wa kuvifunga,mtu wa kuvitumia na hata kuvifanyia ukarabati.itachukuwa muda kuwafikia wenzetu
 
uKIJARIBU KUANGALIA KWA MAKINI UTAGUNDUA
KWAMBA VIONGOZI WATANZANIA WANAPENDA
SANA KWENDA KUTIBIWA NJE.
HATA KWA MAGONJWA AMBAYO YANGEFAA KUTIBIWA
HAPA NCHIONI WANAKIMBILIA NJE KWA MATIBABU SASA
SIJUI NJE KUNA HOSPITALI KWA AJILI YA VIONGOZI WA
TANZANIA AU NI KASUMBA WAMEJIJENGEA ..
Itafikia sehemu serikali itaongoza Nchi ikiwa india kama ya
somalia ilivyofanya ikiwa Kenya hivyo ni kazi kwao
kurekebisha mambo mapema il kila kitu kikae vizuri.

nawasilisha.,,,,.,,,,,,,,,,,,.................
 
Huu ni ushauri wangu naomba maoni yenu. Kwa sasa matibabu katika hospitali za Tanzania kidogo ni nzuri katika hospitali za binafsi. Kati ya madai ya madaktari nchini uboreshaji wa vifaa vya tiba katika hospitali za umma. Hospitali ya rufaa kama Muhimbili kama hospitali ya rufaa haina vifaa vingi muhimu kama T-Scan na vingine kama ambavyo watu wengi wakiweno viongozi kutibiwa nje ya nchi. Ili viongo wetu waamke waboreshe hospitali zetu tuwakatalie kutumia kodi zetu kutibiwa nje ya nchi. Watakapoona maisha yao nayo yako hatarini wataacha siasa na kuboresha hospitali zetu. kwa kweli tuamue kweli kuwakatalia na tuwe na msimamo kwani hawawezi kushinda nguvu ya umma. Ngoja niishie hapa niwapishe kwa maoni.
 
Ili tuweze kuboresha hospitali za tanzania tukatae viongozi kutibiwa nje ya nchi
Huu ni ushauri wangu naomba maoni yenu. Kwa sasa matibabu katika hospitali za Tanzania kidogo ni nzuri katika hospitali za binafsi. Kati ya madai ya madaktari nchini uboreshaji wa vifaa vya tiba katika hospitali za umma. Hospitali ya rufaa kama Muhimbili kama hospitali ya rufaa haina vifaa vingi muhimu kama T-Scan na vingine kama ambavyo watu wengi wakiweno viongozi kutibiwa nje ya nchi. Ili viongo wetu waamke waboreshe hospitali zetu tuwakatalie kutumia kodi zetu kutibiwa nje ya nchi. Watakapoona maisha yao nayo yako hatarini wataacha siasa na kuboresha hospitali zetu. kwa kweli tuamue kweli kuwakatalia na tuwe na msimamo kwani hawawezi kushinda nguvu ya umma. Ngoja niishie hapa niwapishe kwa maoni.​
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Siyo hospital tu. Ili kuboresha shule ni lazima watoto wa watumishi wote wa Serikali kusoma shule za serikali. Na tuweke kwenye katiba.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nakubaliana na hoja 100%. Kama kiongozi anataka kutibiwa nje ya nchi afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe lakini si kwa hela ya watanzania.
 
Nilimaanisha: Ili tuweze kuboresha hospitali za tanzania tukatae viongozi kutibiwa nje ya nchi.
 
Mkuu nakupa 100/100. Mimi nilishasema hapa JF hata shule tusipozua watoto wa Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na viongozi wengine serikalini kupeleka watoto kwenye private school, shule zetu za kata zitakuwa vichekesho siku zote
 
Huu ni ushauri wangu naomba maoni yenu. Kwa sasa matibabu katika hospitali za Tanzania kidogo ni nzuri katika hospitali za binafsi. Kati ya madai ya madaktari nchini uboreshaji wa vifaa vya tiba katika hospitali za umma. Hospitali ya rufaa kama Muhimbili kama hospitali ya rufaa haina vifaa vingi muhimu kama T-Scan na vingine kama ambavyo watu wengi wakiweno viongozi kutibiwa nje ya nchi. Ili viongo wetu waamke waboreshe hospitali zetu tuwakatalie kutumia kodi zetu kutibiwa nje ya nchi. Watakapoona maisha yao nayo yako hatarini wataacha siasa na kuboresha hospitali zetu. kwa kweli tuamue kweli kuwakatalia na tuwe na msimamo kwani hawawezi kushinda nguvu ya umma. Ngoja niishie hapa niwapishe kwa maoni.

Kenya pamoja na uhujumi uchumi; Wanatibiwa Nairobi Ukienda Hospitali za Nairobi zote zina Mashine za kisasa na Safi

na Bora Waziri wao Mkuu Odinga aliugua akafanyiwa Operation ya Ubongo pale pale Nairobi hakukimbizwa - India

Na Odinga kapona na yuko salama sisi Madaktari wetu wakitaka Vyombo vya kisasa always serikali inasema haina pesa

Lakini utasikia Rais kaenda nje na kundi la watu 40; Mwai Kibaki hajawahi kwenda kuhutubia UN haoni sababu ya

kupoteza pesa; alikwenda ya Mwaka Jana sababu Kenya ilikuwa inachaguliwa kwenye SECURITY COUNCIL

SISI ni WAGONJWA TUNAJIFANYA WAJAMAA MBELE YA UMATI; lakini ni MABEPARI UCHWARA
 
Huu ni ushauri wangu naomba maoni yenu. Kwa sasa matibabu katika hospitali za Tanzania kidogo ni nzuri katika hospitali za binafsi. Kati ya madai ya madaktari nchini uboreshaji wa vifaa vya tiba katika hospitali za umma. Hospitali ya rufaa kama Muhimbili kama hospitali ya rufaa haina vifaa vingi muhimu kama T-Scan na vingine kama ambavyo watu wengi wakiweno viongozi kutibiwa nje ya nchi. Ili viongo wetu waamke waboreshe hospitali zetu tuwakatalie kutumia kodi zetu kutibiwa nje ya nchi. Watakapoona maisha yao nayo yako hatarini wataacha siasa na kuboresha hospitali zetu. kwa kweli tuamue kweli kuwakatalia na tuwe na msimamo kwani hawawezi kushinda nguvu ya umma. Ngoja niishie hapa niwapishe kwa maoni.
Huu ni mtambo gani aisee? Tangu mchana naona unatajwatajwa au ndio CT-Scan
wabongo kwa ujuaji!!!!!!!!!!!!
 
Viongozi wetu hawaoni kama mgomo wa dadakitari ni tatizo kwani wao huwa hawatibiwi hapa muda wowote wana ndege standby(pesa za kodi) tayari wakijisikia vibaya kuwapeleka India na Ulaya kutibiwa kuanzia mafua makali,malaria hadi kupasuliwa.Wanaelewa bongo vifaa havipo na wao ndio wanaostahili kuishi.Kwani Sajuki msanii huyu,dr ulimboka,mwakyembe,na wengineo wangebaki hapa siku za kuishi zisingekuwa hivyo.Madaktari bingwa tunao vifaa hakuna.CHUKUA NUSU TU YA MAGARI YA KIFAHARI YA SERIKARI VINGEKUWA VIFAA HADI HOSPITARI ZA WILAYA ZINGEPASUA NA KUTIBU MAGONJWA YOTE.Fikiria hivi ingekuwa ni risasi,bunduki za polisi,uchaguzi ,mwenge,magari,yaani pesa isingekuwa issued.
 
Wakati ndugu zetu wakisumbuliwa na kukosa vifaa na madaktari kugoma Tanzania viongozi wamekuwa wakienda kutibiwa na kufanya uchunguzi wa kiafya nchi za nje!! wakati Hospitali hazina hata vifaa vya kutosha. Sasa hawa viongozi wanaosema wanawapenda ni wakati wa kuangalia je maisha yao na maneno yao ni ya kweli!!
 
We waache wadunde wakifikiri watanzania badowamelala.
 
Ni aibu ya hali ya juu kwamba viongozi wa Africa hawawezi kutibiwa kwenye nchi zao! hadi check up ni nje. Ukweli ni kwamba Ombaomba wa USA anapata matibabu bora kuliko Millionaire wa Tanzania!.
 
Huwa natatizika sana naposikia viongozi wetu wanasafiri all the way kutoka Tanzania mpaka Marekani au nchi nyingine yoyote ya Ulaya kwa ajili tu ya kuchunguzwa afya. Huwa najiuliza hivi madaktari wetu wa waliosomea hapahapa nchini hawawezi kufanya hiyo kazi? Kama hawawezi basi kwa maoni yangu ni wakati muhimu wa kuwawezesha ili waweze kuifanya hiyo kazi na ili kupunguza gharama za kwenda nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom