Mateso ninayopitia hayabebeki wala kuzoeleka

Upwiru

Member
Mar 27, 2022
15
50
Salaam wakuu

Hii ni stori yangu ya kweli kuhusu jambo linalonitesa na kuniumiza kwa muda wa mrefu sasa. Nitaweka kila kitu wazi katika angle zote ili niweze kupata msaada. Tafadhali sana, naomba kwa yeyote atakayeweza kunipa mawazo ya kunisaidia asisite kufanya hivyo. Natanguliza shukrani zangu za dhati. Sasa twende moja kwa moja kwenye Mada. Tatizo langu hasa ni UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka chini ya 30. Mkasa wangu unaanzia mbali sana wakati nasoma shule ya sekondari. Mimi ni mmoja wa wale vijana ambao aibu ilikuwa inatutawala na tulichelewa sana kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi licha ya mara kwa mara kuwa na tamaa za kimwili kama binadamu wengine.

Kama nilivosema awali, nilichelewa kujihusisha na mapenzi sio kwamba sikuwa na matamanio, bali ni uamuzi wangu binafsi niliokuwa nao. Katika kipindi chote hicho, kuna mambo yaliyokuwa yananitokea ambayo nilikuwa nayaona ni kawaida tu. Mfano, unajikuta labda uko kwenye mziki unacheza na binti yupo mbele yako. Katika hali ya kucheza nae unashangaa umepata msisimko wa ajabu na kujikuta ukijipiga bao. Hii hali ilikuwa ikinitokea lakini sikushituka kwasababu nilihisi kabisa labda kwakuwa sijawahi kushiriki tendo la ndoa, basi vile vitu vinakuwa vimejaa sana. Nilikuwa nachukulia kawaida. Mfano wa pili ni ile hali inakutokea upo kwenye mtihani au unafanya shughuli yoyote ya haraka na muhimu. Mara ghafla unaambiwa muda umekaribia kuisha. Unajikuta napata msisimko wa hatari na kujipiga bao. Hii ilinitokea huko nyuma wala sikujali kwa sababu niliamini chupa kimejaa kwa sababu sijawahi shiriki tendo la ndoa.

Lini sasa niligundua kuwa nina tatizo?

Baada ya kumaliza kidato cha sita nikiwa na miaka 22, hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kushiriki tendo la ndoa. Kabla ya hapo sikuwahi kushiriki tendo hilo na wala sikuwahi kuwa na hofu yoyote juu ya tendo hilo wala upungufu wa nguvu kwasababu sikuwahi kuona weakness yoyote kwenye mwili wangu.

Naikumbuka jioni moja ya mwezi Mei miaka 7 iliyopita. Nilikuwa na miadi na mtoto ambaye nilikuwa kwenye mahusiano naye. Ile tumefika guest, shauku ikawa juu sana na katika kuandaana pale pale nikajikuta namwaga...kabla hata sija penetrate. Ile hali ilinishangaza sana kuona uumea umesinyaa na kuwa kama wa mtoto. Nikajiuliza kwa kupanic hiki ni nini? Kwasababu sikuwahi kuelewa chochote kuhusu kujamiiana na wala sikujua kama halia ya kusinyaa uume huwa inatokea kwahiyo nilipanic. Mtoto alikuwa mzoefu hivyo alinituliza pale na kuniambia ni hali ya kawaida. Basi shughuli ikawa imeishia pale. 15k yangu ya chumba ikapotea.

Nakumbuka siku ile sikulala vizuri. Nilikuwa na mawazo sana na niliwaza maisha yangu yatakuwaje kama niko vile. Mtoto aliendelea kunifariji na kunipa moyo na maisha yakaendelea.

Baada ya pale niliendelea na mahusiano na yule binti. Na tulikutana kimwili mara kwa mara. Lakini katika mara zote nilizokutana nae bado bao la kwanza lilikuwa linanitoka hata kabla sijamuingia. Ni ile katika kupeana romance na maandalizi najikuta nimemwaga. Nakaa muda wa dakika kadhaa uume unasimama na najaribu kupenetrate ila simalizi dakika namwaga. Sio kwa raundi ya pili au ya tatu. Sijawahi kuzidi sekunde 30. Siujui huo utamu na inaniumiza sana

Kama walivyowanaume wengi, matamanio ni maisha yetu. Hivyo nilikuwa na mahusiano na mabinti wengine pia. Lakini kote huko niliishia kuumbuka. Nikijitahidi sana basi lile bao la kwanza litakuja baada ya kupiga takle mbili tatu. Na hapo nafanya bila kumuandaa mwenza wangu maana nikisema nimuandae tu namwaga hata kabla sijavua nguo. Ni mateso sana. Naumia na inaitesa sana hii hali.

Kiufupi sijawahi kufurahia sex. Kwangu mimi kwenda dakika moja bila kumwaga ni muujiza sana achilia mbali kwenda nusu saa. Sijawahi kuzidi sekunde 30. Sio kwa bao la kwanza, la pili au mia moja. Inaniumiza sana.

Napata hamu ya ngono ila sina uwezo wa kufanya ngono. Huniumiza sana kimoyomoyo nikikaa na wenzangu wakiwa wanafurahia faragha zao. Natamani wangejua mateso ninayopitia kijana mwenzao. Nina kila kitu ila sina furaha ya mapenzi. Na kinachoniumiza zaidi ni kuwa nipo katika age anbayo natakiwa kuwa na familia. Kuna binti nampenda sana, nayeye ameonesha kunipenda ila huwa namkimbia. Sitaki kuaibika. Hata kununua malaya siwezi kwasababu nisawa na nitapoteza hela yangu bure. Kuperform chini ya nusu dakika ni zaidi ya showtime. Ni fedheha na maumivu makubwa sana.

NB:
1. Asilimia kubwa ya maisha yangu nimekulia mkoani ambako vyakula vya asili ndio vyakula vyetu. Maisha yangu hayana uzungu kusema labda aina ya vyakula ninavyokula.

2. Katika maisha yangu sijawahi kujichua.

3. Mi ni kijana ninaecheza soka. Kwahiyo mazoezi yamekuwa ni sehemu ya maisha yangu toka enzi hizo.

4. Sidhani kama ni swala la kisaikolojia maana kama confidence ninayo. Siku ya kwanza nakutana na mwanamke nilikuwa niko sawa kimwili na kiakili. Sikuwa na hofu yoyote. Hata baada ya yaliyotokea. Yalinitesa mwanzoni ila badae nikajijenga kisaikolojia na kujiamini lakini bado.

5. Katika kukua kwangu nimesumbuliwa sana na gesi tumboni. Nimekuwa mbovu wa tumbo toka enzi za utoto.

6. Kipindi fulani cha maisha yangu nilikuwa na fungus sehemu za siri kwa muda mrefu sana.

7. Hadi leo bado nateswa na wet dreams, kuna muda hata bila kuota naamka najikuta nimechafuka.

8. Kuna muda uume wangu unasinyaaa na kuwa mdogo sana kama wa mtoto wa primary. Ila kikawaida nikiwa katika full erection, uume wangu ni inch 6.

9. Nina hisia zote za kimwili. Inshu kubwa ni perforamce. Naweza nikiwa nimekutana na mwanamke namtongoza au mtoto yeyote mzuri ambaye sijamuweka katika kundi la marafiki. Basi huwa nasimamisha uume. Niko active sana. Mtu akiniona anaweza sema huyu jamaa hatari maana uume unasimama active sana ila kimbembe nikifika room. Nusu dakika haizidi. Hiyo ni kwa kila round.

10. Sijawahi tumia mkongo wala viagra.

Nimeweka NB hapo juu ili kwa mtu mwenye nia ya dhati ya kunishauri aweze kujua kila kitu na kuondoa assumptions. Niliwahi kumfungukia baba yangu mzazi ambae hadi leo anaumia kwa ajili yangu. Amepambana sana kwa ajili yangu lakini bado. Anaumia sana kama mzazi.

Imefikia hatua nimekata tamaa ya kupona. Sielewi tatizo ni nini. Mateso ninayopitia ni zaidi ya kusimulia. Najua kwa mwanamme yeyote anajua thamani ya uanaume wake. Kwangu mimi ni tofauti.

Naumia, nateseka na ninahangaika sana. Nimekuja kwenu nikiamini kwenye wengi kuna mengi. Naomba kwa yeyote mwenye kuwa na mawazo namkaribisha sana.

Mimi ni binadamu ambaye sijapenda kuwa hivi. Kwa yeyote atakaekuja na comments za kejeli na dharau ajue kabisa kuwa zitaniumiza na kunipa machungu sana kwasababu sikuchagua kuwa katika hii hali. Najua watu wa aina hiyo hawakosekani ila ni vema tu ukihisi unataka kunikejeli ufikirie mara mbili kabla ya kuniumiza kwa maneno ya dhihaka. Mpaka nakuja hapa nimefikia kiwango cha mwisho cha kukata tamaa. Sihitaji kingine zaidi ya msaada na faraja. Nitawasamehe wote watakaonidhihaki ila sitawasahau kwa jinsi watakavyokuwa wameniumiza sana.

Ndugu zanguni, hili tatizo lisikie kwa mwingine. Ni tatizo kubwa sana. Linatesa na kuumiza sana. Watu wana familia zao, wana mademu zao na wanaenjoy maisha yao ila nipo mimi ambaye kwa nje ni furaha ila kwa ndani ni huzuni kubwa sana. Sio uongo, ni kweli nakimbia wanawake. Nakimbia kuficha aibu yangu. Sifurahii hii hali ila nitafanyaje???

Naamini panapo uhai nitarudi na ushuhuda wa kupona hapa mbele yenu. Imani hiyo ni kubwa sana. Karibuni sana kwa msaada ndugu zangu.
 
7. Hadi leo bado nateswa na wet dreams, kuna muda hata bila kuota naamka najikuta nimechafuka.

Nimejaribu kusoma sehemu zote sijaona kasoro isipokuwa hapa nambari 7 nimejikuta napata mawazo tu, isijekuwa una ile kitu waamini waliodeep kwenye mambo ya kiroho wanaita "spiritual wife"...

Ambayo kuna watu wa kike na kiume imekuwa inawasumbua kwenye maisha yao ya kingono na wenzi wao kiasi kwamba wanajikuta wanaishi wenyewe tu bila mahusiano au ndoa...
 
Salaam wakuu

Hii ni stori yangu ya kweli kuhusu jambo linalonitesa na kuniumiza kwa muda wa mrefu sasa. Nitaweka kila kitu wazi katika angle zote ili niweze kupata msaada. Tafadhali sana, naomba kwa yeyote atakayeweza kunipa mawazo ya kunisaidia asisite kufanya hivyo. Natanguliza shukrani zangu za dhati. Sasa twende moja kwa moja kwenye Mada. Tatizo langu hasa ni UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
Pole sana kwa hilo tatizo mkuu, labda nijaribu kushauri, kama kwa sasa uko kwenye mahusiano basi fanya siku moja moja mkae wote tu ndani (wewe unaweza kuvaa boxer tu na yeye kanga moja) bila kufanya tendo.

Unaweza ukaweka movie mkaangalia wote au mkafanya usafi, kupika etc kama ratiba za kila siku. Point yangu ni hii: nahisi akili/saikoloji yako inahitaji mazoea ya kuona mwili wa mwanamke kama ni kitu cha kawaida na wala sio kitu hadimu.

Ukishakuwa na "chemistry" wewe na mwanamke especially huyo ambae uko nae kwenye mahusiano naamini confidence ya tendo itaongezeka na utakuwa sawa kwake na hata kwa wanawake wengine.

Experience ya kutokuwa na wanawake huko nyuma inaweza ikawa ndo sababu.
 
Pole sana kwa hilo tatizo mkuu, labda nijaribu kushauri, kama kwa sasa uko kwenye mahusiano basi fanya siku moja moja mkae wote tu ndani (wewe unaweza kuvaa boxer tu na yeye kanga moja) bila kufanya tendo.

Unaweza ukaweka movie mkaangalia wote au mkafanya usafi, kupika etc kama ratiba za kila siku. Point yangu ni hii: nahisi akili/saikoloji yako inahitaji mazoea ya kuona mwili wa mwanamke kama ni kitu cha kawaida na wala sio kitu hadimu.

Ukishakuwa na "chemistry" wewe na mwanamke especially huyo ambae uko nae kwenye mahusiano naamini confidence ya tendo itaongezeka na utakuwa sawa kwake na hata kwa wanawake wengine.

Experience ya kutokuwa na wanawake huko nyuma inaweza ikawa ndo sababu.
Asante sana mkuu
 
Pole sana ndugu, nimeumia pia kwa ajili yako hasa nikifikiria kuna wakati napiga show mpaka naamua kuahirisha bila kumwaga,
Jaribu kuwa unatumia mizizi ya mtulatula unatoa maganda ya juu unakwangua na kisu kisha unatafuna,naamini inaweza kukusaidia na pia hata isipotatua tatizo bado haina madhara yoyote kiafya,pole sana
 
Mkuu kunywa maji mengi ,fanya mazoezi ,relax , job changanye na wanawake mpaka hiyo mbususu uione ya kawaida tu ...muda mwingine ni mihemko mikali unayokuwa nayo unapokuwa na mwanamke kwa bed...
Asante mkuu kwa ushauri wako. Ila kiukweli kabisa mimi ni mtu wa mazoezi sana. Kuhusu kuiona mbusus ya kawaida naiona sana kwasababu nimeshakuwa na wanawake wengi kwa mara nyingi. Sina presha ya mbususu wala kimuhemuhe na kuhusu maji mimi kama mtu wa mazoeazi natumia sana. Ila sielewi shida ni nini lakini nakushukuru sana
 
Pole sana ndugu,nimeumia pia kwa ajili yako hasa nikifikiria kuna wakati napiga show mpaka naamua kuahirisha bila kumwaga,
Jaribu kuwa unatumia mizizi ya mtulatula unatoa maganda ya juu unakwangua na kisu kisha unatafuna,naamini inaweza kukusaidia na pia hata isipotatua tatizo bado haina madhara yoyote kiafya,pole sana
Asante sana ndugu yangu kwa kuyahisi maumvi yangu. Bahati mbaya huo mtulatula siufahamu. Pengine naufahamu kwa jina jingine na nitashukuru ukinifafanulia zaidi au hata picha.
 
Pole sana ndugu,nimeumia pia kwa ajili yako hasa nikifikiria kuna wakati napiga show mpaka naamua kuahirisha bila kumwaga,
Jaribu kuwa unatumia mizizi ya mtulatula unatoa maganda ya juu unakwangua na kisu kisha unatafuna,naamini inaweza kukusaidia na pia hata isipotatua tatizo bado haina madhara yoyote kiafya,pole sana
Mtulatula tena?
 
Back
Top Bottom