Matatizo ya mfupa wa kati wa kifua (sternum/breast bone)

badshah

Member
Mar 16, 2013
51
32
Habri zenu wana JF,

Ningependa kwa yeyote mwenye ujuzi wa hili anipe ushauri... miaka 6 iliyopita nilikuwa nacheza mchezo wa karate, katika hali ya kurusha ngumi nikasikia mshutuko katika mfupa wa kifuani (Stermun) hali hiyo ikanifanya nisiweze kuendelea na mchezo tena. nilitumia dawa za kupunguza maumivu.

Tatizo ni kwamba mfupa huu umekuwa ukinipa tabu kwani nikijinyonga upande wa kulia au kushoto nahisi maumivu ingawa ni ya mbali sana pamoja na sauti za mbaaaali kama vile mtu akivunja vjiti, na wakati wa baridi huwa nahisi maumivu ya mbali sana. lakini tatizo hili halinifanyi nishindwe kupumua, kufanya kazi ngumu, kusikia homa au tatizo lolote kiafya lakini ni ile kero inayotokana na kutokuwa katika hali ya kawaida kama wenzangu.

kuna wakati nikikaa sana nikijisomea muda mrefu, nikiinua kichwa kama hali ya kunyoosha mgogo nasikia kama sauti ya click katika sehemu hiyo iliyoathirika, hali hii inanifanya nihisi kama kuna mifupa imekatika au kuachana kidogo. nimepiga X-ray lakini imeonekana iko poa tu.

Sasa naombebi ushauri wenu kama kuna anayefahamu alternative way ya kuondoa tatizo hili au kama kuna dawa ya kurekebisha. Nice Day!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom