Matapeli sugu wa mtoni Mtongani akina ntunyungu

stineriga

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
2,172
886
utapeli upo wa kuchukua pesa zako cash na utapeli wa kuchukua vitu/bidhaaa unazouza,
hawa wajamaa wamebobea kwenye utapel wa aina zote na wanatumia uchawi, usipokuwa makini au kama huna taarifa hao ni matapeli unalizwa,

nasikia hawa matapeli wa mtongani walishatolewa hadi kwenye tv na RPC lakini si wote waliobahatika kuona hiyo taarifa na hawa na mtandao wao wanaendelea kuwaliza watu, juzi jumatatu tumelizwa milioni 2 na hawa mbwa, inauma sana,

kama wewe ni mfanyabiashara, jihadhari nao watakupigia simu na kusema wana vitu/vifaa vya bei rahis wanauza kisha watakutapeli bila huruma milions/laki zako ulizotolea jasho lako,

ukiwa unauza vifaa/vitu watakupigia simu na kusema kuna mzee/kaka/baba yao anataka na kisha kusepa navyo na kubaki unashangaa

watakupigia simu watakuambia ushuke mtonngani, ukishuka watakuambia uchukue pikipiki hadi msikiti wa kichangani, hapo utapelekwa kwenye nyumba moja fulani hivi amabayo ni nzuri kidogo kulinganisha na nyumba za jirani,

nasikia ukiingia tu humu ndani lazima ulizwe, nasikia wameweka dawa hapo mlangoni, na hii nyumba wanaitumia kama ofis yao ya kuwatapeli watu hawaish hapo wala kulala hapo, kwahiyo kuwapata ni ngumu sana,

Hii ndio nyumba ambayo ukiingizwa tu lazima ulizwe, ipo mtongani kichangani ndani ndani,

attachment.php

attachment.php

attachment.php

NB
1. kama wewe ni mfanyabiashara unayetoa matangazo kwahiyo mtu yeyote anaweza kuwa na namba yako, kuwa makini na wanaokupigia na ujiridhishe kweli ni wateja,
2. kuwa makini sana kutotoa pesa bila kuona bidhaa unayouziwa na kuridhika nayo,
3. kuwa makini vitu/vifaa vyako unavyouza kutoka machoni mwako na hujui vinakwenda wapi na pesa hujapokea,
4. tafuta mwenyeji wa sehemu husika na uulizie kuhusu biashara uanyotaka kufanya kabla ya kuingia kichwa kichwa,
5. sali au jilinde unavyoweza kabla ya kukutana na watu usiofahamiana nao kwa lengo la biashara kwani matapeli wengi ni wachawi
 
Attachments

  • IMAGE_012.jpg
    IMAGE_012.jpg
    251.2 KB · Views: 17,083
  • IMAGE_014.jpg
    IMAGE_014.jpg
    227.9 KB · Views: 17,283
  • IMAGE_013.jpg
    IMAGE_013.jpg
    186.2 KB · Views: 16,844
Hawa jamaa si walikamatwa kwa kutapeli mamilioni kwa kujifanya mapadre? Ina maana weshaachiwa tayari? Mwe!

Hii nchi imeoza, kama mtu alihukumiwa maisha jela afu kakutwa kitaa tena anamiliki SMG unatarajia nini, ndo maana sisi huku kwetu watu wa namna hiyo tunamalizana nao wenyewe kwa kiberiti na petrol, wakija watu wa haki sijui za binadamu, sijui vibaka wanakuta tulishakamilisha kazi kitaambo.Ndo dawa pekee
 
Huku Kichangan, Soweto, Azimio na Tandika kw ujumla ni jambo la kawaida kukuta nyumba/jengo imeandikw kwa maandish makubw USIKUBALI KUTAPELIW, NYUMBA HAIUZW, ni MTUNYUNGU na kundi lake wamewatapeli watu weng kw style hiyo ya kuuza nyumba za watu!
 
Tunaomba vyombo vya habari wafanye investogative journalism wawaanike hawa matapeli na hiyo nyumba itaifishwe na iwe chini uangalizi wa serikali,au hata iwe kituo cha polisi...kwani hawa ia maana serikali imewashindwa kabisa?au nao wanapata commission hapo?wanatisha sana hawa watu...jeshi la polisi nao wanafanya kazi kwa matukio,ile intelijensia iko wapi?
 
Hawa jamaa si walikamatwa kwa kutapeli mamilioni kwa kujifanya mapadre? Ina maana weshaachiwa tayari? Mwe!
Ndio jeshi letu la polisi ukimkamata mwizi atawekwa ndani baada ya siku 2 yupo mtaani, kwa hali hii wale wanaowakamata wezi na kuwachoma moto wana makosa?
 
Tunaomba vyombo vya habari wafanye investogative journalism wawaanike hawa matapeli na hiyo nyumba itaifishwe na iwe chini uangalizi wa serikali,au hata iwe kituo cha polisi...kwani hawa ia maana serikali imewashindwa kabisa?au nao wanapata commission hapo?wanatisha sana hawa watu...jeshi la polisi nao wanafanya kazi kwa matukio,ile intelijensia iko wapi?

kama unamaanisha serikali na jeshi la polisi la tanzania nakupa pole
 
Hawa jamaa si walikamatwa kwa kutapeli mamilioni kwa kujifanya mapadre? Ina maana weshaachiwa tayari? Mwe!

wana mtandao mkubwa hawa mbwa, nasikia kuna wengine wamekamatwa, lakini wengine waliopo mtaani wanaendelea kutapeli, nasikia pia wanatumia uchawi hata wakikamtwa huwa wanatoka na kurudi mtaani na kuendelea kutapeli,
 
Hawa jamaa wameliza sana watu mimi mwenyewe walishanipigia simu wakaniambia wana madawa ya mifungo kutoka shirika la afya duniani.

Nikawatengezea mtego nikapanga vikosi vyangu niwapelekee pesa airport nafika airport napiga simu walete mzigo wachukue niwape pesa wakatuona wakanistukia wakakimbia

Jamaa hatari sana wana vituo vingi tu vya kuumizia watu, Sinza, Airport, Shoprite kamata, Kinondoni, Mwenge, Magomeni.

Wakati mwingine wanajifanya wafanyakazi wa TIGO wanakupigia wanakuomba namba ya siri.
 
Washajua udhaifu wa vyombo vyetu vya dola,ndio maana wanafanya watakavyo!
 
Tunaomba vyombo vya habari wafanye investogative journalism wawaanike hawa matapeli na hiyo nyumba itaifishwe na iwe chini uangalizi wa serikali,au hata iwe kituo cha polisi...kwani hawa ia maana serikali imewashindwa kabisa?au nao wanapata commission hapo?wanatisha sana hawa watu...jeshi la polisi nao wanafanya kazi kwa matukio,ile intelijensia iko wapi?

mkuu nimefikiria sana unachosema, ni kweli nashangaa intelejensia za polisi inakuwa wapi kwenye kudhibiti mitandao kama hii ya kitapeli, na ile nyumba nimefikiria hivyhivyo ibomolewe au itaifishwe na kugeuzwa kituo cha polisi. au ningekuwa nafahamiana na samu mahela au na mtu kama zembwela waanikwe hawa watu hadharani .
 
utapeli ni mwingi sana dar es laam hatari yake unashinda ujambazi, polis nao ndio wa kulaumiwa, kupenda kwao rushwa, polis kutokua siriaz kikaz mtu anakata tamaa hata kwenda kuripoti, anabaki analia tu mwenyewe.

Washajua udhaifu wa vyombo vyetu vya dola,ndio maana wanafanya watakavyo!
 
Mimi nilikutanana na wale wa kuvunja nyumba, waliniumiza mchana kweupe...ile narudi toka kibaruani jioni, nakuta geti wamevunja, milango ipo wazi na vitu ndani hamna, dah natamani kweli kuwakamata niwauzie kesi ...
 
Back
Top Bottom