Matajiri walioko nyuma ya ccm waanza kustuka!

MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,258
274
Niko hapa cmanjiro wazee 'wanene' kifedha wanasemezana 'eti nasikia hawa jamaa wamechukua hata udiwani kata karibu zote..Sasaa' anasema mmoja wakiwa wameegemea gari lililochafuka na matope ya mvua. Labda wametoka Arumeru. 'itabidi nimuhimize mwanangu mmoja aisee aingie kwa hawa majamaa "cdm" manake hii yetu imeshavurugwa na manyang'au'
 
Hao ndio wanaochelewesha ukombozi wetu, jitahidini kuwafahamu kadri inavyowezekana, ikibidi iwe kama mapinduzi ya Ufaransa nyakati hizo.
 
Hatutaki matajiri tunahitaji wazalendo wa kuijenga nchi yetu. kama utajiri wao ni halali na wanalipa kodi wanakaruibishwa sio kuficha ufisadi wao. Miaka 10 tu itatutosha kuibadili nchi yetu kutoka maskini mpaka bajeti ya kujitosheleza sio ombaomba.
 
Niko hapa cmanjiro wazee 'wanene' kifedha wanasemezana 'eti nasikia hawa jamaa wamechukua hata udiwani kata karibu zote..Sasaa' anasema mmoja wakiwa wameegemea gari lililochafuka na matope ya mvua. Labda wametoka Arumeru. 'itabidi nimuhimize mwanangu mmoja aisee aingie kwa hawa majamaa "cdm" manake hii yetu imeshavurugwa na manyang'au'
wasije wakahamia tu CDM kuleta ufisadi wao
 
They are very clever... watakula huku na huku.

By the way, why putting their eggs in one busket wakati CDM inawasha indicator?
 
They are very clever... watakula huku na huku.

By the way, why putting their eggs in one busket wakati CDM inawasha indicator?

kumbe hawa Wazee siku moja tu wameishaanza kukonda! Wangekuwa very clever wangeweka mayai yao ktk vikapu viwili tofauti! No Longer at Easy!
 
ili mradi wapo katika mstari sawa lakini kama biashara zao hazieleweki wasijaribu,i think chadema need smart business people n wealthy,pengine wapo kwa shda 2 ccm bt wanatamani mabadiliko,chadema must be able to win the wealthy n the poor,skilled n unskilled in short all type of people
 
Jamani hata songi za kapteni mlala usingizi hazikusaidia?ama kweli siku ya nyani kufa miti yoooote huteleza
 
CHADEMA wawe makini. Matajiri ndio waliokiponza CCM, na kuwaweka mfukoni.
 
Tusiingie kwenye mtego. Wafanyabiashara wengi siyo mafisadi. tatizo ni wanasiasa wanaotumia jukwaa na nyadhifa hizo kujineemesha wao moja kwa moja au kwa kutumia wanafamilia. kuepusha kujikana mbele ya umma wanajificha nyuma ya wafanyabiashara pamoja na kusafisha fedha haramu na hivyo kutoa mwanya kwa wafanyabiashara kukwepa kodi au kupewa tenda za kiujanjajanja wakati wakilindwa na wanasiasa dhidi ya mkono wa sheria. Haki inawekwa kando. wanasiasa wakiwa waadilifu wafanyabiashara hawatapata upenyo wa kutugeuza madondocha. Dawa ni kuwabana wanasiasa. Kwa vipi? Hicho ni kitendawili. Labda tuanzie kwenye katiba mpya. Lakini mchakato wake umeanza kufinywangwa na wanasiasa kiasi kwamba utakuwa muujiza kama itapatikana katiba yenye kulinda maslahi ya wananchi na kubana wansiasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom