Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,660
- 46,350
Naamini Waziri Mkenda au msemaji wa Serikali wanaona mjadala mkubwa kuhusu combinations mpya za masomo ya kidato cha tano na sita kujumuisha masomo ya kidini. Sasa wasikae kimya, kama wanaona jambo hili lina maslahi mazuri ya nchi basi wajitokeze hadharani kutoa ufafanuzi, kujibu maswali na kuwaeleza wale wanaohoji.
Waziri aeleze,
1. Kwanini waliona ni vyema kuunda tahasusi rasmi za kidini badala ya kuyafanya masomo ya dini kuendelea kuwa options tu au masomo ya ziada ambayo mwanafunzi anayependa anaweza kuongezea?
2. Kwanini ni dini mbili tu ndizo zimeundiwa tahasusi maalumu? Kwa nini dini za Uhindu, Uhamadiya, Ubudha, za Asili n.k hazijaundiwa tahasusi zao?
3. Kwanini hakuna tahasusi mahususi ya dini inayojumuisha dini mbili? Yani tahasusi ya wale wanaotaka kusoma Divinity na Islamic Knowledge kwa pamoja.
4. Kwanini haikuundwa tahasusi ya "religious studies" kutoa fursa ya wanafunzi kusoma kwa upana zaidi kuhusu dini na imani nyingi zaidi za duniani kadri ya uwezo wao?
5. Walimu watakaokuwa wanafundisha haya masomo ya kidini watakuwa waajiriwa wa serikali wanaolipwa kwa kodi za raia? Upatikanaji wao utazingatia nini hasa tukizingatia dini zote mbili kubwa zina madhehebu mengi yenye muelekeo tofauti?