denoo JG
JF-Expert Member
- Oct 27, 2023
- 1,780
- 6,013
Hapa umegusa pazito sana.Nimemshangaa sana anavyohoji uwepo wa Prof Janabi kwenye matibabu ya JPM ambaye tuliambiwa alikufa kwa ugonjwa wa moyo. Alitaka nani awepo?
Angejiongeza kifdogo tu hata kwenye google asome cv za huyo tuliyeambiwa ndiye alikuwa daktari binafsi wa JPM akijulikana kama Prof Mabula Mchembe. Kwenye google cv yake inasomeka kama ifuatavyo:
Dr. MABULA DAUD PAUL MASALU MCHEMBE
MD, M.Med(Surgery)(UDSM),FCS(ECSA),Cert.Cardiothoracic Surgery.
Kwa hiyo daktari binafsi wa JPM ni surgeon, bingwa wa upasuaji. Ugonjwa tulioambiwa umemuua ni ugonjwa wa moyo, ambao bingwa wa fani hiyo ni Prof Janabi. Hivyo ilikuwa muhimu na lazima kumshirikisha Janabi katika jopo la kumtibia mkuu JPM.