mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 543
- 1,875
Wakuu habarini za mida,
Leo nataka niwahabarishe baadhi ya fursa za masomo huku ughaibuni na njia rahisi yakuzifikifikia.
Zifuatazo ni baadhi ya full funded scholarships zisizohitaji GPA ya 3.7 ili uweze kuzinyakua isipokua hata wew GPA ya 2.5 unaweza kuibuka nayo bila matatizo yoyote.
-NAWA scholarships kutoka kwa serikali ya Poland
-DAAD scholarships toka kwa serikali ya Ujerumani
-ITALY GOVERNMENT scholarships kutoka kwa serikali ya italia
-SWEDISH INSTITUTE scholarships kutoka kwa serikali ya sweden
Mimi nikiwa mmoja wa wanufaika wa SWEDISH INSTITUTE scholarships kwa mwaka 2020/2021 kwa leo nitajikita zaidi kuielezea SI scholarship licha ya kuwa na taarifa makini na sahihi kuhusu scholarships zote nilizotaja hapo juu.
Ili kupata Swedish institute (SI) scholarshipa nilazima uwe raia kutoka mataifa yapatayo 42 Tanzania ikiwa miongoni mwao.
Scholarship hii inalenga zaidi kuwapata watu wenye sifa za uongozi huku wakiwa na uzoefu wa masaa yasiyopungua 3000 katika kazi zao husika .
hivyo baadhi uzoefu wako kazini na namna ambavyo uzoefu huo unaendana sambamba na sifa ya uongozi katika program yako ya Masters uliyoomba ndio kigezo kikuu Cha kuibuka kidedea katika maombi hayo bila kujali ushindani wa ufaulu yaani GPA.
Hivyo basi hatua ya kwanza kabisa ya mchakato huu ni kufanya maombi ya chuo katika website yao www.universityadmissions.se
Katika website yao hiyo utafungua account yako huku uliwa na passport yako na kujaza taarifa zako zote muhimu kisha utalipia online kulingana na maelekezo yao ada ya maombi ya chuo ambayo ni krona za kiswedish 900sek sawa na shilingi laki mbili na arobain na tano za nyumbani .
Baada ya hapo huku utachagua programs zako za Masters zisizozidi 4 kutoka vyuo uvipendavyo Kisha kuweka viambatanisho vyako ambavyo ni original copy za passport yako, certificate ya degree, transcripts ,pamoja na requirements zingine kulingana na mahitaji ya chuo ulichoomba,.
KUMBUKA MAOMBI HAYA HUFANYIKA October 16 na deadline ni January 15 admission results hutoka mapema April.
Baada ya kumaliza mchakato wa maombi ya nafasi ya chuo ndipo utaanza mchakato wa maombi ya scholarships ambayo HUFANYIKA katika kipindi Cha siku kumi tu.
Mfano mwaka huu yalifanyika kuanzia tarehe 8 February mpaka tarehe 18 February.
Katika kipindi hiki utaingia katika website yao ya www.si.se ambako nako utafungua account yako ,utajaza taarifa zako na kufanya maombi yako bila malipo yoyote na huko ndipo utakapotakiwa kuwasilisha form zao za maombi ambazo ni Motivation letter, CV, reference letters, leadership and work experience form na hizi zote utazi download toka katika website yao.
Ukikamilisha hayo yote kwa umakini mkubwa hakika Mungu Alie hai atakutendea muujiza kama alionitendea Mimi na hakika utakuja ughaibuni walau kuongwza ujuzi na kusafisha macho na kurudi nyumbani kuwainua watz wenzetu wanaohitaji maarifa zaidi ili kujikwamua.
NB.: application number yangu ilikuwa 13594475 Kama itakavyoonekana hapo pichani na nmeziambatanisha ili kuonyesha uhalisia wa jambo hili.