Mastaa wa Nigeria wanakimbiza kila Charts za AfroBeats popote duniani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,122
FvYfe-NWYAMfLwR
Wasanii wa Muziki kutoka #Nigeria wanaendelea kushika nafasi nyingi na za juu kwenye kiwanda cha Muziki Afrika na Nje ya #Afrika ambapo katika orodha ya nyimbo 10 zilizosikilizwa zaidi kupitia #Spotify, kuna Mastaa 8 wa Nchi hiyo.

Nafasi mbili pekee zimebaki kwa Mastaa wa Nchi nyingine ikiwemo namba 5 ya #Amaarae kutoka #Ghana na nafasi ya 9 ikishikwa na #Libianca kutoka #Cameroon.

Mdau wa Muziki unadhani ni nini kinakwamisha Wasanii wa #Tanzania kufikia viwango hivyo hadi sasa?.
 
Halafu pia kumbuka wanatumia lugha iliyo sambaa zaidi duniani
Kwa hili me ntakupinga ila ni kwa mtazamo wangu tukisingizia lugha tutakuwa tunakosea kwa mfano navy kenzo wanatumua lugha ya kingereza na wanaiba vizuri lakini utashangaa fan base yao sio kubwa sana na kuimba wanajua kabsa hapo utaona kuwa promoters ni jambo la msingi haya Asake anatumia kiyoruba lkn mziki wake mkubwa san unasambaa me naona shida ipo kwy promotions,brand,sound,melody etc ila sio lugha wangapi wanapenda nyimbo za kispanish ila hawaijui hiyo lugha vp kuhusu despacito?? Waliimba kiingereza mule???

Sorry uandishi mbovu ila ndo haya kwa upande wangu
 
Wanaijeria ni wajanja sana. Nyimbo zao nyingi ni za furaha furaha. Ndicho watu wanapenda. Kingine kikubwa ni wajanja sana katika vionjo hasa melody kwenye chorus na bridge. Hapo ataweka %90 kuhakikisha anabamba. Wasikilize wote wanaovuma. Hatujui hata wanaimba nini pamoja na pidgin yao ila tunajikuta tunarukaruka tu. Wasanii wetu wawekeze huko pia. Ila nawakumbusha, soko la muziki limeshikwa sana na vijana. Wakumbuke kuna watu wazima pia ambao hawana burudani. Wanabakia kusikiza kwaya na zilipendwa. Vijana hao wajitahidi kwenye natumizi sahihi ya lugha na ujumbe
 
Back
Top Bottom