Masoko ya HISA ya US yaanza kuporomoka kufuatia utabiri wa Trump kuibuka mshindi wa Urais

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
Masoko ya hisa duniani yameanza kulegalega na yale ya Marekani yakielekea kwenye anguko kubwa kutokana na matokeo ya Urais wa nchi hiyo yanayoendelea kutoka, kuwashangaza wawekezaji duniani.

Donald Trump anaongoza dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton.

Hadi sasa hisa za Dow Jones zimeshuka kwa pointi 800 au 4.4%. Hiyo inalifanya soko la hisa la Marekani kushuka kwa asilimia kubwa tangu August 2011 liliposhuka kwa 5.5%.

Wawekezaji wengi duniani wanaamini kuwa kutotabirika kwa Trump na msimamo wake kibiashara, kutasababisha anguko na hasara kubwa iwapo akishinda.

1478682369343.png
 
Trump alisema atarudisha viwanda vyote USA kutoka Asia. Ushindi wa Trump ni pigo kwa nchi za Asia kuliko Europe. Africa viongozi wengi wakae mkao wa mshangao. Huyu bwana atawapa mbivu na mbichi. Kwa wale wa kuoana jinsia moja huu ni mwanzo mgumu. Huyu bwana hakubaliani na upuuzi huu. Uhamiaji hana mambo na wahamiaji halali. Swala la Imani hapo pana mtihani. Ubaguzi utakomaa. Ni mawazo yangu.
 
Umesema wewe utafiti utabili sijui nn weka pembeni haya hata anguko la utabiri wa tb joshua chali nn wewe unaongea anguko lako hapa ujaliona ulione la marekan ndani ya siku wakat mwaka mzima unashangilia eti tumepiga hatua kwel nguzi nyeusi sisi shida
 
Wanahabari ni mwaka wao wa kuadhirika wanapotosha umma wa ulimwengu badala ya kuwahabarisha ukweli ....ona sasa walisema Bi Clinton anaongoza katika kura ya maoni yu wapi sasa ..waandishi ni wafitinishaji wakubwa walaghai ...aibu na fedheha ni yao sasa hakuna namna...wabebe lawama ya upotoshaji...
 
Umesema wewe utafiti utabili sijui nn weka pembeni haya hata anguko la utabiri wa tb joshua chali nn wewe unaongea anguko lako hapa ujaliona ulione la marekan ndani ya siku wakat mwaka mzima unashangilia eti tumepiga hatua kwel nguzi nyeusi sisi shida
Heeeeee!!
 
Waandishi wa habari wengi akili yao ni moja yani uongo uongo mwingi.
 
Trump alisema atarudisha viwanda vyote USA kutoka Asia. Ushindi wa Trump ni pigo kwa nchi za Asia kuliko Europe. Africa viongozi wengi wakae mkao wa mshangao. Huyu bwana atawapa mbivu na mbichi. Kwa wale wa kuoana jinsia moja huu ni mwanzo mgumu. Huyu bwana hakubaliani na upuuzi huu. Uhamiaji hana mambo na wahamiaji halali. Swala la Imani hapo pana mtihani. Ubaguzi utakomaa. Ni mawazo yangu.
Suala la viwanda si la kisiasa lipo kwenye cost of production. China gharama za uzalishaji zipo chini
 
Trump alisema atarudisha viwanda vyote USA kutoka Asia. Ushindi wa Trump ni pigo kwa nchi za Asia kuliko Europe. Africa viongozi wengi wakae mkao wa mshangao. Huyu bwana atawapa mbivu na mbichi. Kwa wale wa kuoana jinsia moja huu ni mwanzo mgumu. Huyu bwana hakubaliani na upuuzi huu. Uhamiaji hana mambo na wahamiaji halali. Swala la Imani hapo pana mtihani. Ubaguzi utakomaa. Ni mawazo yangu.
Kwa nini alivihamisha mwanzoni? Yeye ndiye mwenye viwanda huko Asia na Australia
 
Masoko ya hisa duniani yameanza kulegalega na yale ya Marekani yakielekea kwenye anguko kubwa kutokana na matokeo ya Urais wa nchi hiyo yanayoendelea kutoka, kuwashangaza wawekezaji duniani.

Donald Trump anaongoza dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton.

Hadi sasa hisa za Dow Jones zimeshuka kwa pointi 800 au 4.4%. Hiyo inalifanya soko la hisa la Marekani kushuka kwa asilimia kubwa tangu August 2011 liliposhuka kwa 5.5%.

Wawekezaji wengi duniani wanaamini kuwa kutotabirika kwa Trump na msimamo wake kibiashara, kutasababisha anguko na hasara kubwa iwapo akishinda.

View attachment 431496
Wanamwogopa mfanyabiashara mwenzao?
 
Back
Top Bottom