Maskini Mtoto Huyu......

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Leo ni siku ya Mtoto wa Afrika....mtoto ambaye amekosa matumaini.....mtoto ambaye unamkuta anaombaomba pembezoni mwa barabara,mtoto ambae anaikosa elimu japo ni haki yake....mtoto ambaye Konyi anamtumia kwenye vita....mtoto ambaye anabakwa na kunajisiwa pamoja na kufanyiwa ukatili wa kila aina.....mtoto ambaye hata akienda shule anaenda na njaa yake,konda anamnyanyasa,na akiwa darasan anakaa chini.....mtoto asiye na mtetezi....mtoto anayesakamwa na magonjwa ya kila aina,malaria,utapia mlo,ukimwi,pepopunda,surua,na kadhia tele......Mtoto ambae hakuna mwanasiasa anayependa kumkadili.....mtoto ambaye baadhi ya watu humtumia ili kupata pesa kwa wafadhili........
Mtoto wa Afrika lini atatabasamu?????
nini lengo la siku ya mtoto wa Afrika?????
 
Back
Top Bottom