Elections 2010 Maskini Mbatia, aunga mkono tafiti za REDET na SYNOVATE!

March 2010.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akitoa tamko la chama chake juu ya ufisadi nchini. Ramadhan Semtawa

SPIKA wa Bunge Samuel Sitta ambaye amejijengea umaarufu kutokana na msimamo wake wa kupambana na ufisadi, ametakiwa kujitoa kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuonyesha utashi wake wa dhati katika kupambana na uovu huo.

Kauli ya Mbatia inakuja baada ya Spika Sitta kunukuliwa akisema huenda Mwenyekiti wa TLP Agustine Mrema anapewa fedha kupigia debe CCM ambayo ni chama cha spika huyo.

Akingumzia kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia alisema Spika Sitta ameonyesha dhamira njema kuanika dhambi za CCM za kununua watu ili wakipigie debe chama tawala jambo ambalo, limekuwa likipigiwa kelele siku zote.

Hayo yalisemwa na Spika Sitta wakati akijibu tuhuma za Mrema kwamba spika huyo anakiuka taratibu za uongozi kwa kuzungumzia suala la Richmond nje ya Bunge.


Spika Sitta alisema; “kinachoshangaza yeye ni mwenyekiti wa TLP, lakini ni wa kwanza kuzungumzia matatizo yaliyomo ndani ya CCM, kama ameshindwa huko ni bora arejee CCM ili tupambane huku.

“Kuna uwezekano huyu bwana anapata fedha ili kuipigia debe CCM,” alisema Sitta.

Mbatia kwa upande wake alisema; “"namshukuru sana Spika Sitta, amesema ukweli yeye ni mjumbe wa Kamati na Halmashauri kuu ya CCM, alipotoa kauli hii tulistuka sana".

"Lakini tunakwenda upande wa pili, kama Sitta anakiri mfumo huo ni wa kifisadi, CCM ina nunua thamani ya utu kwa fedha kitu ambacho ni dhambi kwanini na yeye asitoke CCM," Mbatia alihoji.

Mbatia alienda mbali na kufafanua kwamba Spika Sitta kama atashindwa kutoka CCM basi na yeye atakuwa ni sehemu ya ufisadi huo ambao umekuwa ukiivuruga nchi.

"Kwa kuwa Spika Sitta amejivika joho la kupambana na ufisadi tunampongeza. Tunampongeza kweli, lakini swali la kushangaza ambalo tunakosa majibu ni kwamba mheshimiwa huyu anafanya nini kwenye chama hicho, ambacho amekiri mwenyewe ni chama cha kifisadi?" alihoji Mbatia.

Mbatia alisema NCCR-Mageuzi kina ushahidi wa kutosha kwamba katiba ya nchi, sheria za nchi na sera mbalimbali za nchi ambazo zimekuwa zikitekelezwa chini ya uongozi wa CCM, ni za kifisadi.

"Hivyo ufisadi umejengeka ndani ya dola na dola yenyewe sasa inatekeleza ufisadi huo," alisema Mbatia.

Alifafanua kwamba, aina hiyo ya ufisadi hauwezi kupigwa vita kwa kutoa matamko tu wala kutunga sheria moja moja na kwamba mfumo kama huo, haurekebishwi kwa kupigwa viraka.

"Mfumo unarekebishwa kwa kuubadili na kuweka mfumo mwingine mahali pake, sasa taifa limefika pabaya sheria zinatungwa kuhalalisha ufisadi kwa njia moja au nyingine.

Katika kuonyesha dhamira ya kufumua mfumo huo, Mbatia alitangaza vigezo saba vya kiongozi bora anayepaswa kuchaguliwa na Watanzania kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Alivitaja vigezo hivyo kwamba ni pamoja na mgombea awe mcha Mungu, mzalendo na mwenye uchungu na nchi yake.



Pia awe na ushujaa kutetea maslahi ya taifa, awe mwadilifu awe na moyo na uwezo wa kufanyakazi na aweze kukubali kukosolewa na kuthimini muda.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18492
Source: Mwananchi

My Take:

If you read between letters you will for sure understand what kinda dude he's, very sad.
 
Sasa pata picha ya huo upupu aliouongea leo ndo kajimaliza kabisaaa!!!

naamini kuna ccm dam ambao hawako kwenye core na wanaumia sana kuona chama chao kinayeyuka mbele yao.
he is lunatic (sory mods). jamaa hana tofauti na Dr. Bana
 
Any body around to see James Mbatia on TBC? Nimeamini kweli kuwa huyu jamaa ni Kibaraka wa RA na Sisiem yake. Zile taarifa kuwa anafadhiliwa na Rostam ni za kweli mpaka amediriki kusema kuwa si NCCR au chama kingine chochote kitakacho shinda CCM kwenye uchaguzi huu!

Kweli huyu jamaa hana akili tena maana anasema anacho ambiwa. mwangalie kwenyeTBC sasa

NI KWELI Kabisa vibaraka wa CCM sasa hivi tunavyoelekea 31 oct HAWAJIFICHI maana muda huu ndio wakuthibitisha kazi waliyotumwa wanaifanya barabara. Ukweli ni kwamba baada ya uchaguzi tutakuwa tumewajua waganga njaa wengi ktk siasa za BONGO
 
Mbatia ni kibaraka wa CCM kama tu alivyo Mrema.

Fuatilia matamko na hotuba za Mbatia utajua kabisa jamaa ni mtupu kwenye uwanja wa Siasa.
Yeye alikuwa wa kwanza kuunga mkono tamko la Shimbo kuwa NCCR-Mageuzi wanaukubaliana na upuuzi huo wa kina Shimbo. Halafu amekurupuka tena na kuwa-support REDET na Synovate.

Siku zote ni mtu wa kukurupuka na kudandia mada kama alivyo Mrema. Mrema na Mbatia ni walewale.
Wazungu husema,''Birds of the same feather flock together''.

Mbatia hana lolote hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi sembuse umwenyekiti wa Chama!!!!
 
Kuna WAPUUZI wachache walifanya kampeni kuchelewesha uhuru wetu nyakati za nyerere, lakini uhuru ulipokuja wakabadilisha chorus na kujiunga na furaha ya kuwa huru.
Mbatia siyo tija kwa kipindi hiki na sidhani kama tunamhitaji sana kwenye historia na ramani ya mageuzi nchini.
ndo mana nafahamu sasa kwa nini Marando kajiondoa huko.

nasikia ana mke na watoto. aliwapataje hao?

Taratibu jamani haya, tutaonana wabaya haya ......!!!
 
Jamaa ninamfahamu anamatatizo ya kisaikolojia si anagonga skuli hapa netherlands groningen university yani huwezi amini hata ushirikiano na wabongo wa hapa hana, halafu vidonda vya tumbo huwa vina mzinguo sana... yeye na mkewe pia hawako katika good terms....yote haya yakichangnyikana anakuwa full lunatic...
 
Niliwahi ambiwa kuwa Mbatiani pandikizi kikakataaa, ila baada ya kuona mazungumzo yakeTBC niliamini na alinitia kinyaa. Mimi kwangu mtu yeyote ambaye umeenda shule lakini shule yako ikawa haitafisiriki kwa MATENDO au MANENO yako kutokana na sababu yeyote ile, either kuwa blinded na pesa au ahadi ya wadhifa, nakutambua kuwa sio MSOMI BALI bali ni mtu uliye maliza vidato au levels tu. Mtu yeyote MSOMI lazima usomi wake utafisirike kwa matendo yake. Kuelimika ni kuwa na uwezo wa kuchambua kwa kina na kutenda mambo mbalimbali kwa mujibu wa taaluma na uhalisia wake.
 
Nae ka epa kamemtembelea na anajuta kwa nini amegombea na mdee kawe.............ccm wameanza kumsonga arudi na anaonesha yukop tayari njaaaa.....itamuua km mrema
 
Kwa Maneno haya ya Mbatia!! Baada ya Dr. slaa kutinga Ikulu kwa kura yangu na Watanzania wote wenye uzalendo kwa nchi yetu, mimi nitahamia NCCR kwenda kuanzisha vuguvugu na mageuzi mapya katika chama hicho maana hii siyo NCCR niliyopigia kura 1995!! kuanzia January 2011 nitatuwa mwanachama wa chama hiki na nitapambana na huyu mpumbafu kugombea nafasi ya mwenyekiti na nina uhakika nitamshinda!!!! Amedhihirisha upuuzina njaa zake si kwa wana NCCR- mageuzi bali kwa kila aliyemuona akibwabwaja pale TBC
 
Mbatia ana homa ya uchuguzi baada ya Halima Mdee kumfunika Kawe naona kachanganyikiwa na baada ya uchaguzi chama chake hakipo tena atarudi CCM kuganga njaa
 
So unataka nisijiunge nacho, niacha kife au niende huko huko kumvulumisha huyu Kipepeo? Mi nataka niende nimkabe kabali na kumuondoa kwenye huo uenyekiti anaosemea! Sisiem ikitoka madarakani haitakuwa na maana tena na kuvutia watu.
 
Tunaomba REDT wafanye kira za maoni tujue nani yuko mbele kati ya Dkt.Magufuli na Lissu
 
Back
Top Bottom