Masikini Kanumba...

gmwansasu

Member
Apr 23, 2008
43
5
Sikuwahi kuwaunga mkono waliokuwa wanamzogoa Kanumba wakati alipolazimika kuongea kiingereza huko BBA, lakini hii baada ya kuingia kwenye tovuti yake kwa kweli imebidi na mimi niongee kitu.

Hivi kwani huyu dogo kama angeandika biography yake kwa kiswahili angepungukiwa nini? maana hicho kiingereza alivyokichanganya kwa kweli mpaka kinatia kichefuchefu.

Nakumbuka wakati anawalalamikia waTz kwa kumsema vibaya nakumbuka alisema kuwa mbona kuna wasanii wengi wakubwa hawajui kiingereza na hakuna mtu yoyote anayewasogoa, ingawa dogo kuna kitu alisahau, kuwa hao wasanii wakubwa wasiojua kiingereza huwa hawa pretend kujua kiingereza hata kidogo, kila wanapohojiwa na vyombo vya habari vya kimataifa wataongea lugha waliyoizoea na hicho chombo cha habari kitakuwa na jukumu la kutafuta namna ya kutafisiri hayo mazungumzo.

Sasa yeye amevuruga kila kitu kwenye hiyo tovuti, eti "I originate from Shinyanga region in Tanzania" au "I was given birth on january 8th 1984"

Nisimalize utamu, bonyeza hicho kiunganisho cha tovuti hapo chini tusaidiane kulalamika

HugeDomains.com - KanuMba.com is for sale (Kanu Mba)
 
sikuwahi kuwaunga mkono waliokuwa wanamzogoa Kanumba wakati alipolazimika kuongea kiingereza huko BBA, lakini hii baada ya kuingia kwenye tovuti yake kwa kweli imebidi na mimi niongee kitu.

hivi kwani huyu dogo kama angeandika biography yake kwa kiswahili angepungukiwa nini? maana hicho kiingereza alivyokichanganya kwa kweli mpaka kinatia kichefuchefu.

nakumbuka wakati anawalalamikia waTz kwa kumsema vibaya nakumbuka alisema kuwa mbona kuna wasanii wengi wakubwa hawajui kiingereza na hakuna mtu yoyote anayewasogoa, ingawa dogo kuna kitu alisahau, kuwa hao wasanii wakubwa wasiojua kiingereza huwa hawa pretend kujua kiingereza hata kidogo, kila wanapohojiwa na vyombo vya habari vya kimataifa wataongea lugha waliyoizoea na hicho chombo cha habari kitakuwa na jukumu la kutafuta namna ya kutafisiri hayo mazungumzo.

sasa yeye amevuruga kila kitu kwenye hiyo tovuti, eti "I originate from Shinyanga region in Tanzania" au "I was given birth on january 8th 1984"

nisimalize utamu, bonyeza hicho kiunganisho cha tovuti hapo chini tusaidiane kulalamika

http://www.kanumba.com/Biography.html
Swali je umemuelewa?if yes then tatizo ni nini?
Kanumba nampa tano hadi hapo alipo ameworkhard sana.Je wewe unaeijua vizuri lugha ya mkoloni umefanya nini,imagine unakufa leo utakumbukwa kwa lipi?
Kanumba anapiga shule sasa.mwacheni kama kumzodoa mmemzodoa sana na naamini akijifunza kutokana na makosa
 
kaka,
mbona unamrekebishia kanumba huku jamii?
huku huwa haingii kabisa, wee mcheki kwenye global publisher na michuzi,
huko utamkuta kisha utamwambia ni wapi akarekebishe kwenye ukurasa wake huo wa wavuti
 
Hili lilisha jadiliwa sana huko awali.... nadhani before unaileta hii tena unge search for the old threads..
 
Nafikiri Kanumba alisikiliza mawaidha ya watu wanampenda kweli na si kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa au kumkashifu. Wale wote wanaomtakia mema walimwambia wazi kabisaa kuwa "Ngosha gani unalialia kama mwanamke (mwana nkima)? Acha kulialia hapa na nenda shuze ya Kiingereza."

Mie napendekeza pia ajifunze somo linaloitwa Comunication Skills. Huwezi kuwa unaongea KISWAENGLISH wakati uko kijijini. Kama unaongea Kiswahili basi jitaidi kuongea Kiswahili na kama Kiingereza, basi ongea kiingereza hasa. Kama ni Kisukuma basi kimwage haswaa kama huna akili nzuri..........

Kila la kheri Kanumba huko shuleni.....
 
kaka,
mbona unamrekebishia kanumba huku jamii?
huku huwa haingii kabisa, wee mcheki kwenye global publisher na michuzi,
huko utamkuta kisha utamwambia ni wapi akarekebishe kwenye ukurasa wake huo wa wavuti
Ni kweli ni vema akashauriwa kwenye hiyo tovuti yake, maana inawezekana kabisa hajapata mshauri mzuri. Alitakiwa angalau apate mtu wa kumfanyia 'editing' kabla hajaileta hewani
 
MKuu maisha ya "kuigiza" ni magumu, sisi weusi tuna kasumba moja mbaya na sugu sana mioyoni na miilini mwetu ya kutopenda vya kwetu labda ukitoa wale waasisi wa nchi zetu kama akina Nyerere na Kwame Nkrumahm ambao hata walipoenda Ulaya walirejea makwao pasipo kutukuza umagharibi, kizazi hiki balaa tupu na pengine kinatia kichefuchefu.

Mchina, Mkorea au Mwarabu ni mara chache sana kumkuta akijipengekeza kwa wamagharibi kwa kuongea kiingereza (Lugha ya watawala), hata kama anajua vizuri atajifanya hafahamu kabisa na pengine kuomba mtafsiri . Na katika kuongea kiingereza ni mara chache mno kukuta watu wa mataifa mengine wanajifanya kuongea kwa lafudhi (accent) ya Kizungu, na pengine hata mzungu anapotaka kuongea kishwahili, huwezi kusikia akilazimisha kuongea kwa lafudhi yetu ya kishwali.

Lakini cha kusikitisha na kuumiza mioyo, sisi waswahili ambao maisha yetu yote tumekulia sehemu ambazo hata kishwahili chenyewe hakiongeleki kutokana na kushamili kwa lugha za kienyeji, ukijua kidogo kizungu aidha kwa kusoma au kubahatisha, hapo hata mama yako mzazi ambaye hajui "a" wala "be" unataka kumbabaisha na kizungu, unamchanganyia kwenye mazungumzo..... oh, "you know, eeeh, i min.....yes yes....."...

Kasumba tuliyonayo ni kuona ukiongea Kiingereza unakuwa mtu mwenye kuheshimika mbele ya jamii, na kwetu hata mtoto mdogo akijua kiingereza (ata akiwa mzungu) watu wanamwogopa kwa kudhani amesoma kumbe hiyo ni lugha kama njia ya mawasiliano tu......sana athari zake hao watoto wetu tunaowapeleka hizo shule zinaitwa za kimataifa zinazotoa elimu kwa lugha ya kiingereza (english medium schools) wamekwisha alibika kabisa, kiingeeza kimaechanganyika na kikuyu au kijaluo kwa kuwa walimu ni wa Kenya na akiwa mtaani (uswahilini) mtoto anataka watoto wenzie wajue au mama yake ambaye hakusoma kiingereza anamsemesha kiingereza, mama au wenzake wanabaki wakimtazama, tu muda wote, hakuna mawasiliano tena !.... pengine kama mama ndio hivyo tena ana baki "Yes, yes.....mh, mh,..."". MBAYA KABISA!

Ukienda ulaya au Marekani hata kama kishwahili ulichokuwa ukiongea kilikuwa na lafudhi ya Kibondei, Kipare, kichaga, kinyakyusa au kihayahaya (eh, kule nyumbani! sawaaa!), hata ukikaa siku moja, ukirejea nyumbani unataka uongee kama Mzungu au Mmarekani Mweusi bila kujua tunadharaulika mbele ya wenye lugha yao na kutuona tunafaa kuendelea kutawalika kupitia lugha!....

Uswahili mzee, mbwembwe nyingi, najua hata Kanumba akiambiwa asome huo wasifu wake mbele za watu atajifanya kusoma kwa lafudhi ya Kizungu, lakini wanaokijua wameshaona ni madadu matupu aliyoandika kwenye huo wasifu wake na hata kiingereza kingine kwenye tovuti utumbo mtupu!......ni vyema atoe kabisa au akishindwa aombe wanajamii tumsaidie kupata tovuti yenye tafsiri ya kiswahili kwani wateja wake ni sisi waswahili wenzake, sijui kama kuna mzungu asiyejua kiswahili anaweza kuvutika na picha za kishawhili au kuelewa hata hicho "Kishwangilishi cha kisanii" kilichotumi lugha .

Binafsi inaniumiza saaaana kuendelea kuiangalia hii tovuti kwa kuzingatia heshima niliyonayo kwake huyu msaani kijana na mtanzania mwenzangu anayehangaika!.........pengine hajui athari zake, tafadhili kama Kanumba unafuatilia, rekebisha hilo, sisi tunaendelea kukuunga mkono lakini jaribu kuheshimu unayopewa, haya sio usanii, utazidi kufanikwa........

WIvu wa Maendeleo: "JIFUNZE KUTUMIA FIKRA ZA WENGINE KUREKEBISHA PALE ULIPOKOSEA NA SIO KUACHA KABISA FIKRA ZAKO KWA KUONA ZA MWENGINE NI BORA ZAIDI ......UTAPOTEA"
 
Ukiwa public figure ni lazima u-manage your image.... Kanumba angetakiwa atafute ushauri kwani kumbukeni kuwa internet ni ya ulimwengu mzima, and people from everywhere will judge you on that....na ukiwa public figure you have to be aware of that. Mi nadhani mchangiaji katoa ushauri mzuri na mashabiki wake wangefany ala busara kumshauri abadili na kuiweka katika standard English...
 
"Usipojua, usijifanye unajua, wakijua hujui, hutaweza tena kujua!" upo umuhimu mkubwa wa kuomba ushauri pale unapofanya kitu chochote chenye kuweza kukunianika katika jamii na ukifanya hivyo, utaonekana shujaa. hakina aliyezaliwa kamili, hata Yesu aliomba ushauri!
 
Mkuu umesema kweli nakubaliana na ww...hata filamu zao wanazocheza zinatia kichefuchefu unapoangalia ina jina la kingereza lakini lugha inayotumika ya mazungumzo ni kiswahili.
 
Swali je umemuelewa?if yes then tatizo ni nini?
Kanumba nampa tano hadi hapo alipo ameworkhard sana.Je wewe unaeijua vizuri lugha ya mkoloni umefanya nini,imagine unakufa leo utakumbukwa kwa lipi?
Kanumba anapiga shule sasa.mwacheni kama kumzodoa mmemzodoa sana na naamini akijifunza kutokana na makosa

Matatizo ni mengi tu,

1) Kueleweka pekee si lengo pekee la lugha.Lazima kuwe na misingi iliyokubalika inayofuatwa. Hata kama mtu ataelewa lugha isiyo sahihi, msemaji hana guarantee kwamba ametumia lugha sahihi inayotakiwa kueleweka na kama msomaji/ msikilizaji hataelewa hili litatokana na mapungufu yake.In other words, ukitumia lugha isiyo fasaha, unafanya bahati nasibu kuhusu kueleweka kwako. Huu msemo wa "kama umeelewa tatizo ni nini" unaonyesha uzembe wa kufikiri na kukubali mediocrity. Kwanza ushaanza kusema tatizo ni nini kabla ya kujua kama kaeleweka au hajaeleweka, nikikwambia sijamuelewa kwa sababu katumia lugha ya ajabu, utasemaje?

2) Hili jambo linaonyesha tatizo kubwa kuliko la lugha tu.Ina maana huyu mtu haelewi kitu kinachoitwa proof reading.Inaonyesha huyu bwana hajui kitu kinachoitwa ukalimani.Inaonyesha huyu bwana hana team nzuri, yeye mwenyewe si team player pia.Kwa sababu hata mtu asiyejua kiingereza vizuri anaweza kuongea na watu wakamuandikia kitu kizuri tu, au akaenda sehemu akasema mimi kiingereza sijui vizuri lakini nina mambo mazuri ya kusema na kufanya, nahitaji kuongea kiswahili na mtu anifanyie ukalimani, watu watamuelewa.

Jana nilikuwa namuangalia kijana mmoja wa bongoflava kutoka X-PLASTAZ, wanarudia rudia BET Video Awards, kijana huyu alirap na malegends wa hip hop kama kina KRS-1 na wengine wanaochipukia siku hizi, yeye alirap Kiswahili, wakawa wanaandika captions za kiingereza, alifanya vizuri tu, mpaka KRS-1 akawa anajisikia self conscious line ya KRS-1 ya kwanza ilikuwa "I can't rap in Swahili, but...." yaani pale ku rap Kiswahili ilikuwa ni kitu cha ujiko,kitu fulani exotic.

Sasa basi, wanaokuja kumtetea Kanumba kwa minajili ya kujivunia culture yetu wanakosea,kwa sababu watu wanaopenda culture yao hawatumii lugha za wenzao.Wafaransa kibao wanajua kiingereza lakini ukienda Paris na kusema kiingereza wanajifanya kama hawajui, wanataka ujifunze kifaransa. Fidel Castro anajua kiingereza lakini interview zake zote anaongea Kihispania cha Cuba na wakalimani wanatafsiri.

Sasa kwa mtu anayejidai kukumbatia utamaduni wetu, huku kujikaragosi kwa kukumbatia lugha ya kiingereza ambayo hatuijui ndiko kutukuza utamaduni wetu? Mimi ningemtegemea mtu anayependa utamaduni wetu, hata kama ni msomi anayejua kiingereza cha Mkapa, ningemtegemea atumie kiswahili as a matter of principle, sembuse huyu mnyanyapuaji?
 
Aisee hii ni kali. Kama huu ndio U STAR basi tena!!! Huku ndio kujivika Viatu vya Goliati wakati wewe una Umbo la Mbilikimo!!!
 
Swali je umemuelewa?if yes then tatizo ni nini?
Kanumba nampa tano hadi hapo alipo ameworkhard sana.Je wewe unaeijua vizuri lugha ya mkoloni umefanya nini,imagine unakufa leo utakumbukwa kwa lipi?
Kanumba anapiga shule sasa.mwacheni kama kumzodoa mmemzodoa sana na naamini akijifunza kutokana na makosa

"Ninachojua ni kwamba watu wengi unapowakosoa mara nyingi huwa ni wakali.Nadhani hamkuelewana na huyu bwana.Ni kwamba kanumba kwakuwa amepende habari zake ziwe kwenye mtandao, basi angewausisha watu waliosomea mambo haya, mpaka sasa hivi kuna wataalamu wanaoandika bibiogaphy vizuri sana kusudi wamwandike na kitu kiingie kwenye mtandao na kivutie watu wengi.Na mimi nasema amechemka sana, lazima hivi vitu uusishe watu wakushauri sio kujiandikia unavyojua.Kitu chochote lazima uwe na templates au uusishe wausika,vinginevyo utaendela kucheka na kufanya upumbavu watu wanakukosoa wewe unakuwa mkali tu eti watanzania hawanipendi, mtu ambaye hakupendi hawezi kukwambia makosa yako.
 
Lengo la kuwa na tovuti ni kuwasilisha ujumbe kwa wanaoitumia tovuti yako. Hivyo ni vyema ukatumia njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako bila kelele wala mikwaruzo. Kanumba angeweza kabisa kutumia kiswahili na ujumbe wake ukafika. Aidha si vibaya kutumia kiingereza kufikisha ujumbe huo, cha msingi ni yeye kugharamikia kidogo kwa kuwatumia watu wenye weledi wa lugha ya kiingereza ambao wanaweza kumtayarishia maelezo mazuri ambayo yatawafanya wanaotembelea tovuti yake kuelewa ujumbe anaokusudia.
 
Matatizo ni mengi tu,

1) Kueleweka pekee si lengo pekee la lugha.Lazima kuwe na misingi iliyokubalika inayofuatwa. Hata kama mtu ataelewa lugha isiyo sahihi, msemaji hana guarantee kwamba ametumia lugha sahihi inayotakiwa kueleweka na kama msomaji/ msikilizaji hataelewa hili litatokana na mapungufu yake.In other words, ukitumia lugha isiyo fasaha, unafanya bahati nasibu kuhusu kueleweka kwako. Huu msemo wa "kama umeelewa tatizo ni nini" unaonyesha uzembe wa kufikiri na kukubali mediocrity. Kwanza ushaanza kusema tatizo ni nini kabla ya kujua kama kaeleweka au hajaeleweka, nikikwambia sijamuelewa kwa sababu katumia lugha ya ajabu, utasemaje?

2) Hili jambo linaonyesha tatizo kubwa kuliko la lugha tu.Ina maana huyu mtu haelewi kitu kinachoitwa proof reading.Inaonyesha huyu bwana hajui kitu kinachoitwa ukalimani.Inaonyesha huyu bwana hana team nzuri, yeye mwenyewe si team player pia.Kwa sababu hata mtu asiyejua kiingereza vizuri anaweza kuongea na watu wakamuandikia kitu kizuri tu, au akaenda sehemu akasema mimi kiingereza sijui vizuri lakini nina mambo mazuri ya kusema na kufanya, nahitaji kuongea kiswahili na mtu anifanyie ukalimani, watu watamuelewa.

Jana nilikuwa namuangalia kijana mmoja wa bongoflava kutoka X-PLASTAZ, wanarudia rudia BET Video Awards, kijana huyu alirap na malegends wa hip hop kama kina KRS-1 na wengine wanaochipukia siku hizi, yeye alirap Kiswahili, wakawa wanaandika captions za kiingereza, alifanya vizuri tu, mpaka KRS-1 akawa anajisikia self conscious line ya KRS-1 ya kwanza ilikuwa "I can't rap in Swahili, but...." yaani pale ku rap Kiswahili ilikuwa ni kitu cha ujiko,kitu fulani exotic.

Sasa basi, wanaokuja kumtetea Kanumba kwa minajili ya kujivunia culture yetu wanakosea,kwa sababu watu wanaopenda culture yao hawatumii lugha za wenzao.Wafaransa kibao wanajua kiingereza lakini ukienda Paris na kusema kiingereza wanajifanya kama hawajui, wanataka ujifunze kifaransa. Fidel Castro anajua kiingereza lakini interview zake zote anaongea Kihispania cha Cuba na wakalimani wanatafsiri.

Sasa kwa mtu anayejidai kukumbatia utamaduni wetu, huku kujikaragosi kwa kukumbatia lugha ya kiingereza ambayo hatuijui ndiko kutukuza utamaduni wetu? Mimi ningemtegemea mtu anayependa utamaduni wetu, hata kama ni msomi anayejua kiingereza cha Mkapa, ningemtegemea atumie kiswahili as a matter of principle, sembuse huyu mnyanyapuaji?
nimeipenda hii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom