Mashoga wa Tanzania wana Haki zote kama Watanzania wengine?

MKJJ,

Ni kweli kuwa katiba yetu inawapa uhuru sawa raia wake wote pamoja na mashoga kama akina auntie Moody. Je ni kweli kuwa katiba yetu inatambua uwepo wao?? Ninavyofahamu TZ hatujawahi kusema popote kama tunatambua uwepo wa jinsia hiyo ya mashoga. Hii ya kusema kuwa rais wote wanahaki sawa haina maana kama katiba haitambui uwepo wao. Katiba nafikiri inatamka kuhusu uwepo wanaume, wanawake, watoto, vijana, wazee, vilema (may be mashoga wako huko) na posssibly albinos. Je una maana mashoga wakijamiiana ni sawa kwa sheria zetu?? Nakumbuka miaka michache iliyopita nilisikia kama kuna sheria imepitishwa ZNZ ambayo haiwatambui mashoga na wakikutwa ni lupango miaka 25.

Katiba haitambui uwepo wa Zeruzeru je Zeruzeru hawana haki kama 'mtu'? Katiba haitambui uwepo wa walevi je walevu hawana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa "utu" wao. Katiba inatumia neno "kila mtu" it includes everybody and excludes no one.
 
Tatizo sio haki za Washoga Tanzania, tatizo jamii yetu inakubali mashoga?

Samahani lakini kwa swali langu ni mfano tu kwa Mzee Mwanakijiji na Gaijin..

Vipi kama watoto wenu wa kiume wakiwa mashoga wakawaletea wenza wao nyumbani muwatambue kama wakwe zenu mtakuwa tayari kuwapokea?

Swali zuri sana; haya kwa mfano anamleta mtu kwangu na kusema ni mkwe wangu si ninayo haki ya kukataa kutambua uhusiano huo. Dhamira ya mwanadamu haiwezi kulazimishwa. Lakini unataka ufanye nini uchukue bastola na kuwaua? Wa ngapi wanaleta wezi, vibaka n.k majumbani mwetu na kama wazazi tunawaonesha watoto wetu kutopendezwa nao. Lakini katika hierachy ya uovu utaona kuwa madhara yanayotokea ni kwa hao wawili na dhambi zao na Mungu wao. Jukumu letu kama kuwashawishi kuona makosa ya matendo yao lakini kama hawageuki hatuna cha kuwafanya zaidi ya kuwasaidia watoto wetu wengine kuzidi kujua asili ya mahusiano ya wanadamu na yanavyohusiana na jinsia.

Hatuwezi kuanza "kamata kamata ya mashoga" wakati tutakaotaka kuwakamata ni wale wanaoonekana kama wanawake. Hatutawakama mabasha au wasagaji.
 
Nikirudi kwenye shinikizo la ushoga ni lazima tushtuke na tukereke. Sababu hasa ni jambo lililo kinyume na maumbile ya Mwanadam. Sheria zetu zipo wazi, ukipatikana na ushahidi kuwa umemuingilia mwanamme/mke kinyume ya maumbile, adhabu yake miaka 30 jela.

Nafahamu hili vizuri na nimelipa maanani; swali niambie kama serikali tunaenda kuanzia wapi kutafuta ushahidi wa ushoga?

a. Kila mume na mke wajaze fomu kila siku asubuhi kutuambia kama hawakufanya tigo?
b. Tukiona wanawake wawili wanaingia kwenye chumba kimoja (ewe nyumbani kwao au vinginevyo) tuwagongee kwa kuwashtukiza ili tujue wanachofanya?
c. Vipi wanaume wawili tukiwaona wanatembea pamoja na kucheka kwa tabasamu halafu wakaingia kwenye nyumba moja na kulala hadi asubuhi twende tukachunguze mashuke?

How do we get evidence ya vitendo vya ushoga ili to enforce the law?
 
Tanzania kama taifa tuna mengi ya kuiga kutoka mataifa yaliondelea, hili la ushoga haliendani na utamaduni wetu, hata kwenye nchi zilzioendelea ushoga haukubaliki na wengi ni wanasiasa ndio wanaolibeba suala la ushoga kwa manufaa yao binafsi, mifano ipo mingi na ya wazi; kila binadamu anahaki ya kufanya maamuzi yake binafsi, hatuna haja kujadili kitu ambacho hakiendani na utamaduni wetu wala hakina maslahi ya taifa letu.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Nafahamu hili vizuri na nimelipa maanani; swali niambie kama serikali tunaenda kuanzia wapi kutafuta ushahidi wa ushoga?

a. Kila mume na mke wajaze fomu kila siku asubuhi kutuambia kama hawakufanya tigo?
b. Tukiona wanawake wawili wanaingia kwenye chumba kimoja (ewe nyumbani kwao au vinginevyo) tuwagongee kwa kuwashtukiza ili tujue wanachofanya?
c. Vipi wanaume wawili tukiwaona wanatembea pamoja na kucheka kwa tabasamu halafu wakaingia kwenye nyumba moja na kulala hadi asubuhi twende tukachunguze mashuke?

How do we get evidence ya vitendo vya ushoga ili to enforce the law?

Are you in the game? What are you trying to push for?

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Hawana haki kama heterosexual. Kuna stigma kubwa sana against mashoga, iwe politica au social stigma na wanaochangia wengi ni politica and religious figures, wakijifanya kuongea kwa niaba ya watanzania wote.
They are molested and categorized and segregated jus for who they have sex with, shida ambayo wewe huipati.
Mbaya zaidi wakiamua kwenda kufungua kesi bado watatukanwa tena for daring. Soma hapa:
Homosexuality is not only openly condemned by powerful social actors such as church leaders and politicians but is also illegal.

In his open letter to the Anglican Diocese of Central Tanganyika Mdimi denounced the violent prosecution, hate and ostracism that gay Tanzanian had to face (Mdimi, 2007). Anyamele mentioned in his 2005 report on Sexual minorities (recognized and co-funded by the world bank) that Tanzanian Homosexuals were being segregated professionally and socially and mentioned that ‘adverse comment’ were made regularly against homosexuals by senior politicians, including head of state. (Anyamele 2005)

Sexual activities between men are punishable of 14 years in prison (no mention of inter female sex) and celebration of a gay union in a way that approximate marriage is punishable of 7 years in prison (section 154 to 157 of the Tanzanian Penal code).



Mbona uchawi una social stigma hivyo hivyo? so is Ulevi, wizi n.k uchangudoa una social stigma na mambo yanayowakuta maCD labda hayawakuti hata mashoga; kwanini wasituambie tuwatambue rasmi machangu doa na haki zao za binadamu? Kwamba watu wanatendewa vibaya na vyombo vya sheria au jamii linawahusu watu wengi tu vile vile kwenye jamii.
 
Katiba haitambui uwepo wa Zeruzeru je Zeruzeru hawana haki kama 'mtu'? Katiba haitambui uwepo wa walevi je walevu hawana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa "utu" wao. Katiba inatumia neno "kila mtu" it includes everybody and excludes no one.
But kwa mashoga kuna organic laws which are specificaly repressive to them, unlike other minorities. Mirorities kama albino na wengine at least they are legal na wanaweza kujiunga, na kujiendeleza. Ila homosexuals hawatambuliki, they are illegal, it is an offence to claim homosexuality! sasa hapo kuna haki gani? haki zenyewe anticonstitutional?
 
Mbona uchawi una social stigma hivyo hivyo? so is Ulevi, wizi n.k uchangudoa una social stigma na mambo yanayowakuta maCD labda hayawakuti hata mashoga; kwanini wasituambie tuwatambue rasmi machangu doa na haki zao za binadamu? Kwamba watu wanatendewa vibaya na vyombo vya sheria au jamii linawahusu watu wengi tu vile vile kwenye jamii.
Kwa hiyo unawafananisha mashoga na wachawi?
 
Kwa leo nakuunga mkono Ritz. Nashangaa sana watu kusema kua mashoga wana haki kama watanzania heterosexuals.
Hivi ni nani kati yetu anapewa identity kufatana na jinsia ya sexual partner wake? Maana this is true kwa mashoga na mabasha.
Ikiwa you have sex with people of your gender in Tanzania hiyo inakua sababu ya watu kukuangalia tofauti, kuwaambia watoto wao wakuogope, kujadili mambo yako publicly, kupigwa ,kuwa segregated kikazi etc.
Huwezi ku-adopt, huwezi kuoa wala kuolewa, huwezi kuvaa nguo unazo taka na kujitetea haki yako.
Hata nchi za njie zinashindwa kuingia in touch na gay lesbian and transexual community sababu they are ILLEGAL! huwezi kuanzisha kikundi cha wanachama GLT sababu vyama kama hivyo havisajiliwi!
Nashangaa Mkadara ananambia kua 'culture yetu' haijawa tayari kupokea ndoa ya watu wenye jinsia moja. Yetu sisi kina nani? nani anasema kwa jina la watanzania wote? mbona hao gays lesbians and transexual tunao waongelea ni tanzanian pia? Hivi tukisema kila mtanzania anahaki ya kuoa/kuolewa kwa nini tunataka ku-restrict anaoa/anaolewa na nani?
Anaendelea kwa kusema mashoga walianza kwa kuwaingilia watoto wetu alafu maswala ya mapenzi yakaja baadae. Huvi unajua watoto wengi hulaitiwa na ndugu zao (kaka, mjomba, baba mdogo au baba, and sometimes mama, dada etc)? na hao watu wanafanya hivo bila kua shoga au basha, ni tabia zao mbaya tu. Na mapenzi kati ya jinsia moja yalikua tu, ni vigumu kusema yalianza lini.
Tuwe wazi, haki hizi hazipo na "culture" is only a pretext we use, a cover.

RR.
Kwa leo tu ndio umeniunga mkono kumbe uwa upendi michango yangu!

Tuvumiliane mkuu, ndio maana ya forum kuna vichwa tofauti tofauti.

Naungana na wewe kwenye mchango wako kwenye hii thread..
Mashoga hawana haki Tanzania!
 
Kwa leo nakuunga mkono Ritz. Nashangaa sana watu kusema kua mashoga wana haki kama watanzania heterosexuals.
Hivi ni nani kati yetu anapewa identity kufatana na jinsia ya sexual partner wake? Maana this is true kwa mashoga na mabasha.
Ikiwa you have sex with people of your gender in Tanzania hiyo inakua sababu ya watu kukuangalia tofauti, kuwaambia watoto wao wakuogope, kujadili mambo yako publicly, kupigwa ,kuwa segregated kikazi etc.
Huwezi ku-adopt, huwezi kuoa wala kuolewa, huwezi kuvaa nguo unazo taka na kujitetea haki yako.
Hata nchi za njie zinashindwa kuingia in touch na gay lesbian and transexual community sababu they are ILLEGAL! huwezi kuanzisha kikundi cha wanachama GLT sababu vyama kama hivyo havisajiliwi!
Nashangaa Mkadara ananambia kua 'culture yetu' haijawa tayari kupokea ndoa ya watu wenye jinsia moja. Yetu sisi kina nani? nani anasema kwa jina la watanzania wote? mbona hao gays lesbians and transexual tunao waongelea ni tanzanian pia? Hivi tukisema kila mtanzania anahaki ya kuoa/kuolewa kwa nini tunataka ku-restrict anaoa/anaolewa na nani?
Anaendelea kwa kusema mashoga walianza kwa kuwaingilia watoto wetu alafu maswala ya mapenzi yakaja baadae. Huvi unajua watoto wengi hulaitiwa na ndugu zao (kaka, mjomba, baba mdogo au baba, and sometimes mama, dada etc)? na hao watu wanafanya hivo bila kua shoga au basha, ni tabia zao mbaya tu. Na mapenzi kati ya jinsia moja yalikua tu, ni vigumu kusema yalianza lini.
Tuwe wazi, haki hizi hazipo na "culture" is only a pretext we use, a cover.

RR, nadhani unajaribu kuzungusha maneno wangu; tunasema mashoga wa Tanzania ambao ni wa Tanzania wana haki kama Watanzania wengine. Sijasema kama "watanzania heterosexual". Kimsingi na kinadharia ni kuwa Watanzania wote wana haki sawa. Suala la ndoa ni haki ya wanaume na wanawake na deviant sexual behaviour za aina zozote hazikubaliwi tu ati kwa sababu wanaofanya wanasikia raha. Jamii imejiwekea mipaka kwenye mambo hayo na kwa kadiri jamii inavyokwenda inajikuta inabadilika na kuwa more accommodating. I'm quite sure itatokea kuwa sheria hizo za anti-homosexuality zitakuja kufutwa.

Na sidhani kama mashoga wa TZ wanacholilia ni ndoa kwa sababu thats is a losing battle; hata hizo nchi zilizoendelea sana duniani ni karibu nchi tatu (nyingine ni miji) ambazo zimekubali some form of gay marriage. Lakini Marekani haitambui at the Federal Level ndoa za mashoga chini ya DOMA; hata Uingereza haina sheria inayotambua ndoa za mashoga. Watu wasichanganye "civil unions" ambazo zipo kwenye miji na states mbalimbali kuwa ni sawa na ndoa. Siyo sawa.
 
Umesoma makala ya mwanakijiji vizuri? hili ndilo tatizo la watanzia wengi mnasoma hamuelewi!! vivyo ndio nyie mnatupeleka kwenye mikataba mibovu. nakuakikishia ndugu yangu wewe sio tatizo lako ni mfumo wa tanzania na shule zake zinatuletea watu kama nyie wavivu wa kusoma vitabu, kuchambua kuelewa maudhui.

mwanakijiji hazunguzii sheria, maana sheria zipo na hazifuatwi na hao wenye dola, lini umewahi kuona shoga kakamatwa na polisi na tunakuwa nao kila siku kwenye madisko? mbona wanaokamatwa ni akina dada zetu(dada poa), kama hawana mbinu na vifaa kwa nini wasitengeneze kitengo maalumu au wakawapa baadhi ya polisi utaalamu wa kuwakamata na kuwafikisha kwenye mahakama ili hiyo sheria unaisema ichukue mkondo wake?

dola linachojua ni kupiga marufuku watu kuandamana iwe vyama vya siasa au asasi mbalimbali, na kujiaandaa na mabomu ya machozi na magari ya kuwasha? kwani haya magari yalikuwepo jamani si yaliletwa wakati wa mkapa? dola iliona umuhimu wa kuiongezea polisi vifaa? kwa nini sasa wasiwaongezee ujuzi na vifaaa vya kuwakamata mashoga?

mwanakijiji amekupa mfano wakati wa serikali ya clinton walivyoweza kuongezea vipengele kwenye sheria zao za ndoa, hapa kwetu zipo na huko pia zipo mbona tunao watu mitaani mwetu wanaishi mume na mke wote wa jinsia moja yaani wanaume? mbona hawajakamatwa? ukiwashogelea watakuambia ni marafiki? utamzuia rafiki angu kulala kwangu hahahaaaaa

wantanzaia- wadangayinka
Hivi umesoma vizuri na kuelewa nilichomjibu MM? Au umekurupuka tu? Au ndio mwenzetu kwa kuwa unazipenda makala za MM basi kila atakachosema unameza tu. Unanikumbusha enzi za 'zidumu'. Nyie ndio mliotufikisha hapa tulipo leo,na hizo 'zidumu' zenu. Funguka kimawazo, usikubali kulishwa hata mapumba tu. MM anataka tuchanganye haki za binadam na haki za mashoga! Ww unaona sawa? Huo ni upuuzi. Unadhani Uk na USA hawajui kuwa haki za binadam zipo? Na kuwa haki za mashoga hazihitajiki? Kwa kuwa mashoga hapa kwetu hawabaguliwi wala hawadhuriwi? Kama una mawazo hayo unahitaji kufikiri upya. MM anataka pawe na haki za wanasiasa na uraia, ww unadhani wanasiasa hawana haki ktk nchi hii? Eti kwa kuwa wamezuiliwa kuandama na walipoandamana kwa nguvu wakaonja joto ya jiwe. Huo nao ni upuuzi mwingine. Kuwa mtu wa siasa sio maana yake udharau mamlaka na sheria zilizopo. Kwa kufupisha maneno, wazungu wanataka mambo ya mashoga yawe 'rasmi' kwa utamaduni wetu wa kiafrika hayo mambo ya ushoga yapo lakini hayatambuliki rasmi! Tafakari.
 
Mkuu Mwanakijiji, na wachangiaji wengine wa ili suwala la Ushoga wa jinsia zote mbili... Ili suwala si tata au nyeti sana kwa Watanzania, japokuwa si katika vitendo vya kiasili vya mwanadamu, lakini ni moja ya vitendo ambavyo vina miaka mingi sana katika jamii zetu. Japokuwa sisi wenye kuamini imani za kuwepo Mwenyezi Mungu, tuna lilaani kwa nguvu zote na tunajuwa kabisa kuwa halikubaliki katika jamii zetu.

Mkuu, hizo sababu ulizo zieleza hapo juu kuwa mashoga nchini Tanzania wana haki kama raiya wengine, ni kweli maneno yako, naweza kuongeza kuwa haki walionayo ni haki ya kimsingi za kiraiya, awe shoga mume au mke. Kinachopiganiwa hapa na hao wanaojaribu kutuletea hiyo demokrasia ni kuwatambua rasmi na ikiwezekana kuwapa upendeleo kama wanaoupata wanawake, Kwa lable ya Haki za wanawake au walemavu na watoto na haki za mashoga...!

Hii maana yake nini, hapa ni kuwatambua kama wanavyo tambuliwa wanawake, lakini wanashindwa kuelewa kwamba hizo haki wanazotaka kina David tuzitambuwe tayari mashoga wanazo, kama ulizo ainisha hapo juu. Kama ni shoga wa kike tayari anao upendeleo kama mwanamke na kama mwanaume, asili na tamaduni zetu tayari ishampa upendeleo kwenye hii mifumo dume yetu, sasa hawa kina Cameron wanapotuambia kuwa tuwape haki zaidi ya hizo walizo nazo kama raiya itakuwa ni upendeleo na zaidi ya haki wanazopaswa kuwa nazo. Kwa sababu Tanzania ina amini katika usawa wa kijinsia, kwa lengo la kuleta usawa kati ya jinsia zote kike na kiume, na hii imekuja kwa sababu ya kile kilicho onekana kama dhuluma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine.

Sasa tunapoambiwa tuwape haki hawa Mabaradhuli ni haki gani zaidi ya hizo hapo juu, kama usawa wa kijinsia tunatambua haki ya kuwa mme au mke, sasa hawa wapo katika kundi gani?

Kwa kuongeza labda niwafahamishe wachangiaji wengine, kwamba Serikali ya Tanzania tayari wana mawasiliano mazuri tu na hawa mashoga hata kabla ya David Cameron kutamka aliyo yatamka.

Nakumbuka Dr. Luncy Nkya alishakutana nao hawa kwa kofia ya Naibu Waziri wa Maendeleo, Vijana na Jinsia wa Tanzania. Alikutana nao katika mwaka 2009 (The Weekend African 29-30 Sept. 2009) Aidha, Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP. Tanzania Gender Networking Programme) unafanya shughuli zake kihalali, na wameshafanya kongamano la mabaradhuli eneo la Mabibo- Dares Salaam siku chache hata kabla ya kauli ya Cameroon.

Na kwa upande wa Zanzibar kuna eneo linalijulikana kwa jina la Chukwani kuna club maalum ya mashoga (Coconut Beach) ambayo uko mabaradhuli na wasagaji, wanajimwaga na kustarehe bila bugdha yoyote ile. Hii ni Club inayofanya shughuli zake kihalali na inatoa matangazo yake wazi kabisa. Na serikali ya Zanzibar inaelewa kuwepo kwa klabu hiyo yenye leseni kamili. Na hata Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZACP) ina kitengo maalum cha kushughulikia afya za mashoga. (Hiki kitengo kipo karibu na kituo cha daladala Hospitali ya Mnazi mmoja), na ukifika hapo utapokelewa na mabaradhuli wawili waliowekwa rasmi kukaribisha na kuhoji mashoga wenzao, ili wasinyanyaswe.

Bila ya kusahau kuwa mwanzoni mwa mwezi Septemba 2011, taasisi ya UMATI kisiwani Pemba iliendesha semina maalum ikiwashirikisha mashoga na baadhi ya mabasha katika ofisi yao iliyopo Wete karibu na Hospitali kuu.

Haya yote yanafanyika na serkali haisemi kuwa ushoga unatambuliwa rasmi nchini Tanzania. Raiya wakiongozwa na viongozi wa dini wanalipinga swala hili kwa uwezo wao mdogo, japokuwa kuna jitihada kubwa ya makemeo, kulaani juu ya suala la ubaradhuli lakini serikali ishakubali kuwapa ruhusa ya kuendesha mambo yao tayari. Waswahili tuna msemo mmoja unasema hivi, Mwanzo wa ngoma ni lele!

Itakuja kufikia wakati tutalazimika kukubali ndoa za mashoga... Na tukishakubali ilo, tutaambiwa pia katika safu za uongozi wa kiserikali lazima kuwepo mashoga aidha kwenye ubunge wa kuteuliwa au ngazi yoyote ya kitaifa... Mwishowe tutakuja ambiwa kuwa ni kosa la jinai kutokuwa shoga.

Hata hivyo, lazima tukiri kwamba, itikadi na dhana ya ujamaa na kujitegemea, ilishashindwa siku ile ile ilipotangazwa kwa Watanzania. Tanzania hatukuwa kujitegemea hata siku moja, tangia tulipo pata uhuru kamili toka kwa Muingereza. Na kujiunga kwetu kwenye jumuiya ya madola ni moja wapo ya njia ya kutuwezesha kupata misaada kutoka kwa Muingereza aliye itawala Tanzania... Na kwa maana hiyo masharti ya kupewa misaada lazima hiwepo, ikiwemo ya haki za binadamu, haki za wanawake na watoto na sasa haki za kuwatambua mashoga kama kundi maalum katika jamii. Japokuwa tayari wanapata haki kama zilivyo elezwa hapo juu, lakini kinacho takiwa na kina David Cameron ni kuwaamasisha raiya kutowanyanyapaa mashoga kwenye uduma zote za kijamii na wawe na haki ya kuoana baina yao, kama wanavyofanya kwenye nchi zao...! Na hii ndio demokrasia ya nchi zinazotuma misaada...!

Hao wanaotupa misaada inabidi tuwaelewe wanachokipigania kwenye swala la demokrasia, na hata wanasiasa na raiya walio wengi ama hawaielewi demokrasia kwa udhati wake au wamechanganyikiwa, kiasi cha kutoelewa wanachokipinga wala wanachokiunga mkono.

Kinachodhihirika hapa, kwa upande mmoja wanasiasa na wanaharakati wanaunga mkono demokrasia na katiba zake na kwa upande wa pili wanapinga matunda yanayotokana na mfumo huo. Wengi wameshindwa kuelewa kwamba ubaradhuli unaotetewa leo ni matokeo ya kukumbatia utatandawazi na tamaduni za kigeni na kwa upande wa serikali inaogopa kunyimwa misaada kwa kisingizio cha kuwanyima uhuru badhi ya raiya (personal freedom), kwa sababu uhuru huu humo ndani ya hiyo demokrasia.

Narudia tena, Wanasiasa wengi wanashindwa kuelewa hiyo demokrasia inayopiganiwa na nchi zinazotupa misaada, aidha, wameshindwa kuelewa kwamba demokrasia sio tu kuchagua rais, wabunge, au madiwani, bali demokrasia inagusa kila kipengee cha maisha ya mwanaadamu kutokana na aina zake nne za uhuru: uhuru wa kumiliki (uchumi), uhuru wa maoni, uhuru wa itikadi na uhuru binafsi unaomfanya mtu atende alitakalo ukiwemo ushoga wa aina zote, usagaji, umalaya, uvutaji nk. Huku kazi kuu ya serikali katika mfumo wa kidemokrasia ni kulinda na kudhamini aina hizi za uhuru. Kwenda kinyume na aina hizo nne za uhuru ndio husemwa pamevunjwa haki za Binaadamu.

Ni wakati umefika sasa kwa Serikali, wanasiasa, viongozi wa dini pamoja na raiya, kuamua ni demokrasia ya aina gani wanayoitaka kuifuata, aidha ile ya nchi zinazotupa misaada au kuratibu zile demokrasia na tamaduni zetu za Kiafrika.

Mwanzo wa ngoma ni lele.
 
Na kama mashoga wapo ndani ya jamii zetu mnataka wapelekwe wapi ni vizuri mkajadi uwepo wao ili kuweza kujua nini cha kufanya na si kukurupuka na kuanza kulaumu marekani na uingereza

safi sana, umetoa wazo zuri. Inabidi tujiulize kuwa, 'kama wapo ktk jamii zetu, tutawafanya nini? Tuwaue? Inamaana hawana haki ya kuishi? Wapi katika vitabu vya dini panaposema wauawe?
 
Ukiona watu wazima wanaanza kuongelewa vitu vya kipuuzi ujui ni watu wa ovyooo!

ni uppuzi kuongelea, kuandika, upuuzi huu..

kinachotakiwa ni kupuuzwa tena kudharauliwa na kutengwa..oops

huna akili wewe? Wewe ndie mpuuzi. Kila tatizo ukiliweka pending utafika wapi? Huo ni ushamba uliokidhiri. Just solve tatizo na sio kulikimbia. Haya mambo yanazozungumziwa hapa yapo kweli. Tusijifanye hatujui.
 
Huwezi kuwawekea haki katika katiba kwa kuwa leo aweza kuwa shoga kesho akaacha.......sawa na mlevi

Hivi ushoga husababishwa na nini hasa?, Maumbile ya mtu au ni hulka ambayo mtu anaweza kuijenga na kuiacha kama atakavyo?. Maana kuna mjadala mkubwa sana kuhusu chanzo cha watu kuwa mashoga.
 
Nafahamu hili vizuri na nimelipa maanani; swali niambie kama serikali tunaenda kuanzia wapi kutafuta ushahidi wa ushoga?

a. Kila mume na mke wajaze fomu kila siku asubuhi kutuambia kama hawakufanya tigo?
b. Tukiona wanawake wawili wanaingia kwenye chumba kimoja (ewe nyumbani kwao au vinginevyo) tuwagongee kwa kuwashtukiza ili tujue wanachofanya?
c. Vipi wanaume wawili tukiwaona wanatembea pamoja na kucheka kwa tabasamu halafu wakaingia kwenye nyumba moja na kulala hadi asubuhi twende tukachunguze mashuke?

How do we get evidence ya vitendo vya ushoga ili to enforce the law?
Mpaka sasa mahakama zetu zinasubiri ushahidi wa mwingiliwa. Na atakayeshtakiwa na kuhukumiwa (kama ushahidi wa kutosha utawasilishwa mahakamani) ni mwingiliaji. Kiafrika haitarajiwi mtu apende kufanywa kwa hiari yake na kama ikitokea mtu wa hivyo (kupenda kufanywa kwa hiari) jamii itamhesabu kuwa ni hamnazo anayehitaji msaada wa tiba na sio kushabikiwa, eti anapenda mwenyewe.
 
Na kama mashoga wapo ndani ya jamii zetu mnataka wapelekwe wapi ni vizuri mkajadi uwepo wao ili kuweza kujua nini cha kufanya na si kukurupuka na kuanza kulaumu marekani na uingereza
Kwani muda wote walikuwa wanapelekwa wapi?

Wabongo kwa kupenda choko choko hamjambo!
 
Yote tisa lakini tukitaka kufuata haki na uchunguzi ktk swala hili la USHOGA halikuanza kwa mapenzi ya wahusika. Historia ya ushoga inaanza na watoto waliokuwa abused na ndugu, jamaa na watu waliokuwa wakiwaamini wakawaingilia kimapenzi. Kwa hiyo mwanzo wa kupiga marufuku Ushoga ulitokana na sio tu mila na desturi bali kuwalinda watoto wetu ktk vitendo hivyo kama tunavyowalinda watoto ktk maswal ya mapenzi ya kawaida. Ushoiga haukuanza kwa mapenzi ya wahusika bali kuingiliwa kwa nguvu na ushawishi wa matamanio ya baadhi ya watu wazima.

Sasa maadam siku hizi Ushoga umekuwa baina ya watu wazima waliopendana, hii haikatazwi isipokuwa jambo moja tu linalonichanganya. - SHOGA hawezi kuwa shoga bila kufanya kitendo cha kuingiliana kimwili na mtu wa jinsia moja.. Yaani kitendo ndicho tu kinampa identity mtu, kiasi kwamba mtu yeyote hawezi kudai yeye shoga ikiwa hajawahi kuingiliwa ama kuingilia mtu wa jinsia yake!...mmmmhnnn!. Hapa ndipo Utata unapokuja na hakika kinacholaani wa ni kitendo lakini sio WATU..

Kwa nchi zetu ushoga haupokelewi vizuri lakini kama alivyosema Mwanakijiji, huwezi kudai haki za Mashoga wakati mashoga wanazo haki zote kutokana na kwamba sisi hatulaani WATU bali tunalaani kitendo na ndio mila na desturi zetu. Hivyo haki zinazodaiwa haziwezi kuwa applied kwetu kwa sababu mashoga ni watu baina yetu wanaopendwa kama watu wengineo isipokuwa inapofikia swala la kuhalalisha ndoa zao hapo tena huchukiwa hata wahusika wenyewe maana tunahalalisha KITENDO..

Na nchi kaa Uingereza, Marekani na Canada hjawawezi kutulazimisha tukubali ndoa za mashoga kama haki ya mashoga wakati wao wenyewe sehemu kubwa ya Utawala wao hawana sheria inayoruhusu ndoa za mashoga. Ndoa za mashoga ni swala la kijamii na litapewa uzito kulingana na wahusika ktk mazingira yao wenyewe lakini haliwezi kuwa swala la kimataifa..
Nchi zao zimejengwa kwa misingi ya kikristo, na ndiyo maana keleke ziko hapo kwenye kuoana...Yani the sanctity of the marriage according to Christianity.

Sijui kuhusu dini nyinignezo,hata hivyo culture zetu ni kweli zinalaani vitendo hivyo.

Ila sijui kwanini wanatulazimishia mambo ambayo "Hayatatuwekea ugali mezani"?

Ufisadi wanaufumbia macho,kwani hawaoni watu wanapigwa mabomu na risasi kila siku na wala si mashoga?

Hizi double standards nyingine bana, ndo maana sina imani na mtu kabisa!
 
huna akili wewe? Wewe ndie mpuuzi. Kila tatizo ukiliweka pending utafika wapi? Huo ni ushamba uliokidhiri. Just solve tatizo na sio kulikimbia. Haya mambo yanazozungumziwa hapa yapo kweli. Tusijifanye hatujui.
Matusi sio utamaduni wetu. Hii hoja watu wanaogopa kuchangia, wanahofia isiwe rasmi yaani ikazoeleka kwenye jamii mpaka kuonekana ni kitu cha kawaida.
 
Wanaweza wakawa na haki kibinadamu ila kwa Mungu wamelaani na kwangu pia
 
Back
Top Bottom