Mashindano ya kimataifa ya saba ya mchezo wa bao

Nino

Member
Jun 21, 2007
38
1
MASHINDANO YA KIMATAIFA YA SABA YA MCHEZO WA BAO
=====================================

KIBA (Klubo Internacia de Bao Amantoj) linaandaa Mashindano ya Kimataifa
ya Saba ya Mchezo wa Bao

Wanaruhuswa kushiriki mabingwa na wanafunzi.

Chama cha Bao cha Kimataifa (KIBA) kinakualika kucheza Bao la Kiswahili
katika nchi nje ya Afrika.

Anayetaka kushiriki katika mashindano haya hatakiwa kuwa mwanachama wa
chama chochote. Wacheza bao watawekwa katika makundi mbalimbali
kulingana na fani zao. Ukiwa bado mwanafunzi wa mchezo huu, usikose
nafasi hii ya kukutana na wachezaji wengine na ya kujifurahisha wakati
wa tamasha la Czech Open 2014, mjini Pardubice, nchini Česko (Jamhuri ya
Cheki), Julai 12-13, 2014.

Washabiki kutoka Kenya au Tanzania hukosi kutusaidia kusambaza mchezo
huu wa jadi wa Afrika Mashariki!

Tembelea wavuti wa KIBA (http://www.kibao.org/bao07sw.html) kwa maelezo
zaidi na ukitaka kucheza kwa njia ya barua pepe na kufanya mazoezi.

Tarehe za mashindano: Julai 12-13, 2014.

Tunatafuta pia msaada ili tuweze kuandaa mashindano ya kimataifa
yanayofuata nchini Tanzania, mjini Dar es Salaam au Zanzibar au Lindi au
Mtwara. Ukiweza kutusaidia bila malipo yoyote tafadhali utuandikie.

KIBA
www.kibao.org
 
Back
Top Bottom