Mashabiki wamtaka Messi awapatie taji.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,833
BUENOS AIRES, Argentina
AMINI au usiamini kuwa ni lazima Lionel
Messi athibishe ubora wake mbele ya
mashabiki wa Argentina kuwa yeye ni
mwanasoka bora wakati atakapokuwa
amevaa jezi ya timu ya taifa yenye rangi za
michirizi ya blue na nyeupe.
Messi nyota anayetegemewa na mashabiki
wa Argentina kwenye fainali Copa Amerika
zilizoanza jana na kudumu kwa wiki tatu na
nusu.
Messi ni mara chache sana ameonyesha
kiwango chake akiwa na Argentina kama
afanyavyo Barcelona ambako uwezi
kuhesabu.Mwaka jana alishudia Argentina
ikipokea kipigo cha mabao 4-0 na kutolewa
na Ujerumani kwenye robo fainali ya Kombe
la Dunia. Messi hakufunga bao lolote kwenye
mashindano hayo.
Sasa kila jicho litakuwa kwa Messi. Pamoja
na kuwa na sifa kubwa bila ya mafanikio,
Argentina ni wenyeji wa fainali hizo. Messi
anashuka kwenye mashindano hayo akiwa
na mafanikio makubwa kutoka kwa
Barcelona, na kocha mpya Sergio Batista
amejaribu kuiga mfumo wa uchezaji wa
Catalan wa pasi za haraka na kumiliki mpira
zaidi.
ìMessi atakuwa na mafanikio makubwa
Copa Amerika,î alisema Batista. ìKuwa
mchezaji bora wa dunia kuna maanisha
mengi, tutajaribu kumfanya acheze kwa
huru ili tupate matokeo mazuri kwake.î
Messi anaishi mbali na nyumbani. Aliondoka
Argentina na kwenda Barcelona akiwa
mtoto ametumia maisha yake yote akiwa
Hispania, lakini hajawai kufikiri kuchezea
nchi hiyo.
Carlos Tevez anategemea kuwa mfungaji
mkuu wa Argentina. Anajulikana kama
ìCarlitos,î ni kipenzi cha watu wengi nchini
humo akiwa karibu na Messi. Tevez aliianza
soka Boca Juniors, alikulia mitaa ya Buenos
Aires ajari ya gali nusura imfanye asicheke
tena.
Argentina mara ya mwisho kutwaa taji la
kimataifa ni mwaka 1993, Copa Amerika.
Huku mara ya pili kutwaa Kombe la Dunia
ilikuwa mwaka1986.
Wiki iliyopita River Plate iliyotwaa mataji
mengi zaidi nchi humo ilishuka daraja na
kusababisha kuzuka kwa vurugu kubwa
kati ya mashabiki na polisi 2,200. Eneo
lililofanyika vurugu hiyo ni uwanja wa River
Plate wa Monumental ambako fainali ya
Copa Amerika itafanyika hapo Julai 24,
sehemu hiyo inajulikana kwa sasa kama
uwanja wa vita na sasa kumefungwa
kupisha uchunguzi wa chanzo cha vurugu
hizo.
 
No team work ndio maana wanamuabudu Messi. Sasa huyo Messi sijui atacheza namba zote peke yake?

Mkuu hata enzi za Maradona alikuwa ni Star pekee na timu ilitengenezwa around yeye na walichukua kombe la Dunia..

Si hivyo tu single handedly Maradona aliweza kuifanya a bottom team NAPOLI kushinda Serie A... Arguably labda Messi anaweza akawa kama Maradona lakini mpaka Argentina ishinde World Cup na Messi itakuwa tabu sana kwa Mesi kuweza kuvaa viatu vya Almando
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom