Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 23,144
- 26,648
Thanks Jasusi, elimu ni pana na wala tuizungumzayo hatumaanishi ya vitabuni tu na wewe unafahamu fika juu ya niongeleacho. Mfano makamanda wa Chadema wanavyozunguka nchi nzima kutoa somo la uraia kwa wananchi na jinsi wananchi wanavyowaelewa na kuitikia kiasi cha kubadili kabisa wimbi la mtazamo wa kisiasa za mageuzi nchini mwetu. Hii ni moja wapo ya elimu ambayo wananchi wameikosa na CCM imefanya kila jitihada kuwanyima kwa ajili ya wachache wabaki kuwa katika nafasi wanazotaka bila kunyoshewa vidole na wananchi.
Serikali haijawa na mfumo wa kuwafunda watu namna ya kutoa elimu ya kujitegemea kama enzi za awamu ya kwanza ambapo vijijini kulikuwa na msukumo wa kujitegemea na watu baada ya kuhitimu shule walikuwa na mwelekeo wa uzalishaji vijijini. Leo elimu hiyo imekosekana, vijana toka vijijini baada ya kuhitimu shule wanakimbilia mijini. Ukiona vijana walivyojaa mijini huwezi kuamini wanakula nini na wanaajiriwa wapi na ndio maana wako waitikiaji wazuri sana kwenye mihadhara kwa kuwa hawana cha kufanya. Nenda vijiji wamebaki vijana wachache wana ambao nao wengi wanatafuta nafasi ya kwenda mijini na vijiji vimebaki makazi ya wazee tu.
Amini nisemayo kwani nimefanya utafiti na kushuhudia hali ilivyo vijijni na mijini. Shule za kata zimesaidia kuwashika walio mashuleni kubaki huko, na wakishahitimu wanatimkia mijini, ni dalili ya kukosa somo la elimu ya kujitegemea ambalo nio muhimu kwa mazingira ya kujiajiri vijijini ingawa nako kuna changamoto nyingi zinazotokana na kukosekana kwa miundo mbinu mbalimbali na kukosekana kwa utility.
..asante,kwa mwerevu atakuwa amekuelewa vema.na hapa ndo kuna shida!