Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,877
- 2,758
Hivi hicho kidhungu amesema Masha au wandishi wetu makanjanja? Eti works! Shame!
Hivi nyie ndio mnajua sana kingereza? Punguzeni jazba muflisi
Hivi hicho kidhungu amesema Masha au wandishi wetu makanjanja? Eti works! Shame!
It is not correct to say, as Masha does, that there is a complete dearth of books about contemporary Tanzania. It is my ardent hope that Masha will find time to read the following three books, in the order given:
1. The Making of Tanganyika, Judith Listowel, London, Chattto & Widus, 1965.
2. From Goatherd to Governor: The Autobiography of Edwin Mtei, Edwin Mtei, Mkuki and Nyota
Publishers, 2009.
3. Tanzania in Transition From Nyerere to Mkapa, Kjeli Havnevik and Aika Isinika (eds.), Mkuki and
Nyota Publishers, 2010.
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema vijana wengi nchini hawataki CCM kwa sababu hawaoni kilichofanyika tangu kilipoanzishwa.
Masha alisema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko na kwamba, hali hiyo inatokana na kutosoma vizuri historia ya Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV, alisema hatua ya kutopenda chama hicho imetokana na vijana kutosoma historia.
Vijana wengi hawaipendi CCM, wengi wanataka mabadiliko siyo kosa lao, hawakufundishwa. Kuna wakati nilikuwa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza nazungumza, kijana mmoja akasimama akasema nyie, wazee ndiyo wanarudisha nyuma nchi. Nikaangalia nyuma nikajiuliza huyo mzee yuko wapi... Nikagundua kumbe na mimi ambaye nilikuwa najiona kijana kniko kwenye kundi la wazee alisema Masha.
Masha ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Fortunatus Masha, alisema vijana wengi wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo hawalioni ndani ya CCM na kuongeza kuwa, hali hiyo inasababishwa na kutokuwapo kwa mkakati wa kuwafundisha historia ya mafanikio ya Serikali na viongozi wake. Leo hii ukienda Nairobi ukitaka kitabu kuhusu maisha ya Raila Odinga utaipata, ukitaka historia ya (Daniel) Moi .. Kenyatta utaipata. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili nijue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna, alisema Masha na kuongeza:
Sasa kama mtoto ambaye anataka kujua nchi yake, anakosa hata pa kuipata, nchi yake ikoje, marais waliotawala, tumefikaje hapa? Lazima waseme tumekuwa maskini kwa sababu ya chama ambacho kiko madarakani.
Kuhusu kushindwa kwake ubunge mwaka 2010, Masha alisema amekubali kushindwa na anaendelea na kazi zake nyingine. Ukiingia kwenye uchaguzi ni sawa tu na kuingia kwenye mpira, kuna kushinda na kushindwa, kikubwa ukishashindwa kubali matokeo endelea na maisha. Tatizo watu wengi na hasa wanasiasa wenzangu hawana kazi nyingine za kufanya, alisema Masha.
Alipinga madai kuwa kipindi chake cha ubunge na uwaziri hakufanya lolote katika jimbo lake, badala yake alitoa mifano ya kazi alizofanya na kwamba, wanaoeneza hayo ni watu wenye fitina. Sidhani kama ni kweli, unajua kwenye siasa kuna fitina imani yangu ni kwamba kazi yangu nilifanya na kazi yangu ya uwaziri niliifanya. Of course (bila shaka) kutokana na mfumo tulionao, mwenzako lazima akumalize ili akushinde, alisema Masha na kuongeza:
Leo hii tunapoongelea Nyamagana kuna chuo cha polisi kimejengwa, kuna Sekondari ya Mkolani imejengwa nje ya bajeti ya Serikali ni kutoka kwa wafadhili na marafiki, theres a lot of works (kuna kazi nyingi). Alisema alikuwa akisomesha watoto 236 kwa mshahara wake wa ubunge na kwamba, tangu alipoingia bungeni mshahara wake ulikuwa ukipelekwa jimboni kusaidia wasiokuwa na uwezo.
Leo hii ndiyo watu wanakumbuka, ndiyo nasema leo hii hata mke wangu na watoto wangu nao wafurahi kidogo kile ninachokipata, nipeleke kwenye maendeleo ya familia, alisema. Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.
Mwananchi
Nimekubaliana na majibu ya Masha pamoja na mchepuo wa maisha yake baada ya kubwagwa ubunge. Kimsingi siasa ni mchezo mchafu, ukiamua kuuendeleza unaweza kushtukia hata umekufilisi kama kama hukufanikiwa nafasi uliyogombea. Na walioshinda ndio maana wanafanya jitihada kubwa na kutumia njia haramu kurudisha gharama walizotumia kupata nafasi hizo.
Kama nafasi inaruhusu bora kuamua kuendesha shughuli binafsi zinazokupatia lishe na kuyaendesha maisha kwa utulivu kuliko haya ya nafasi za kisiasa za kunyoosheana vidole kila kukicha bila kikomo.
MASHA ANA ufalme wa kumtosha, hahitaji JK... pia uelewe JK ana less than 50% influence kwenye serikali iliyo madarakani
wewe unaangalia juu, kazi zote zipo local government....
komaa-komaa ujue maisha,
inatia aibu sana mtu kama muhingo, a well seasoned journalist anakubali kuwa DC, what a waste!!
tubadilike, we can sustain our families bila hata political appointments
Mkuu, avatar yako ile tuliizoea sana irudishe kamanda, mpaka nimejiuliza huyu ni Mungi yupi but siyo issue kanyaga twende,Kama ni kweli kwamba vijana hawaipendi ccm kwa sababu hawakufundishwa historia ya Tanzania, ni afadhali kwa faida ya ccm hawakufundishwa, maana wangefundishwa wangeshaipindua hii serikali ya kihuni zamani sana. Ametolea mfano kenya, kwamba walifundishwa historia. Ndiyo maana kanu haipo madarakani, ni kwa sababu waliijua historia ya kenya.
Masha: Vijana wengi hawaipendi CCM
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema ...... Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili ajue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna," alisema Masha ......Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.
Jenerali Ulimwengu alishawahi kuwa mkuu wa wilaya?, je ilikuwa bahati mbaya au U-DC wa hivi sasa ni too dilute? najaribu kufikiria U-DC wa Muhingo na makala zake za nyuma hasa before uchaguzi
Wakuu Ngoja nichomoke kwenye hii thread Mimi upande wangu nilikuwa simpendi Masha kabisa nawatakia hoja njema
Masha: Vijana wengi hawaipendi CCM
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema vijana wengi nchini hawataki CCM kwa sababu hawaoni kilichofanyika tangu kilipoanzishwa.
Masha alisema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko na kwamba, hali hiyo inatokana na kutosoma vizuri historia ya Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV, alisema hatua ya kutopenda chama hicho imetokana na vijana kutosoma historia.
Vijana wengi hawaipendi CCM, wengi wanataka mabadiliko siyo kosa lao, hawakufundishwa. Kuna wakati nilikuwa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza nazungumza, kijana mmoja akasimama akasema nyie, wazee ndiyo wanarudisha nyuma nchi. Nikaangalia nyuma nikajiuliza huyo mzee yuko wapi... Nikagundua kumbe na mimi ambaye nilikuwa najiona kijana kniko kwenye kundi la wazee alisema Masha.
Masha ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Fortunatus Masha, alisema vijana wengi wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo hawalioni ndani ya CCM na kuongeza kuwa, hali hiyo inasababishwa na kutokuwapo kwa mkakati wa kuwafundisha historia ya mafanikio ya Serikali na viongozi wake.
Leo hii ukienda Nairobi ukitaka kitabu kuhusu maisha ya Raila Odinga utaipata, ukitaka historia ya (Daniel) Moi .. Kenyatta utaipata. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili ajue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna, alisema Masha na kuongeza:
Sasa kama mtoto ambaye anataka kujua nchi yake, anakosa hata pa kuipata, nchi yake ikoje, marais waliotawala, tumefikaje hapa? Lazima waseme tumekuwa maskini kwa sababu ya chama ambacho kiko madarakani.
Kuhusu kushindwa kwake ubunge mwaka 2010, Masha alisema amekubali kushindwa na anaendelea na kazi zake nyingine.
Ukiingia kwenye uchaguzi ni sawa tu na kuingia kwenye mpira, kuna kushinda na kushindwa, kikubwa ukishashindwa kubali matokeo endelea na maisha. Tatizo watu wengi na hasa wanasiasa wenzangu hawana kazi nyingine za kufanya, alisema Masha.
Alipinga madai kuwa kipindi chake cha ubunge na uwaziri hakufanya lolote katika jimbo lake, badala yake alitoa mifano ya kazi alizofanya na kwamba, wanaoeneza hayo ni watu wenye fitina.
Sidhani kama ni kweli, unajua kwenye siasa kuna fitina imani yangu ni kwamba kazi yangu nilifanya na kazi yangu ya uwaziri niliifanya. Of course (bila shaka) kutokana na mfumo tulionao, mwenzako lazima akumalize ili akushinde, alisema Masha na kuongeza:
Leo hii tunapoongelea Nyamagana kuna chuo cha polisi kimejengwa, kuna Sekondari ya Mkolani imejengwa nje ya bajeti ya Serikali ni kutoka kwa wafadhili na marafiki, theres a lot of works (kuna kazi nyingi).
Alisema alikuwa akisomesha watoto 236 kwa mshahara wake wa ubunge na kwamba, tangu alipoingia bungeni mshahara wake ulikuwa ukipelekwa jimboni kusaidia wasiokuwa na uwezo.
Leo hii ndiyo watu wanakumbuka, ndiyo nasema leo hii hata mke wangu na watoto wangu nao wafurahi kidogo kile ninachokipata, nipeleke kwenye maendeleo ya familia, alisema.
Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.
yawezekana aliona na alizungumza, ila nijuavyo mimi si kila wanachozungumza kinaenda media
Nakuunga mkono Mkuu. Kiongozi yeyote anayetumia Cheo chake kudharau watu simpendi. Huyu nilianza kumchukia tangu alipokoromea Mlinzi pale JMall na kumwuliza kama hajui yeye (Masha) ni nani ili aachwe aendelee kuongea na simu kwenye kibanda cha ATM. Halafu, inakuwaje ana mtoto wa umri wa miaka kumi na saba na bado anajiweka kwenye kundi la vijana ? Kwa nini atumie pesa yake kusomesha watoto 236 ? Kazi ya Mbunge sio kutumia pesa yake kuleta maendeleo, bali kuishawishi Serikali kuleta maendeleo. Kwa nini mtoto wake asome Africa Kusini, shule za Kata wanamjengea nani ?