Masanja Mkandamizaji eti nae ni mchungaji????

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,383
1,354
Heri ya mwaka mpya wa 2014, moja kwa moja bila kupoteza muda leo nataka niseme kuhusu hawa wachungaji wanaoibuka kama uyoga wa masika. Jamani hivi kweli ndugu zanguni walokole imefika mahali mnashabikia ujinga ujinga simply because mnatafuta hela kwa waumini? Mimi nakumbuka enzi zetu wakati tunakuwa ukimsikia mtu ni mchingaji kweli hakuna ubabaishaji ni mchungaji hasa na anajua anachokifanya.

Hivi kweli jamani eti leo Masanja Mkandamizaji eti ni mchungaji na anaitwa na hawa wahubiri kwenye makongamono na anatoa neno, jamani mimi sijui sana lakini siku ya kiama ikifika naona watakaoumbuka ni wengi sana.Eti jana anahubiri live kupitia Wpo redio anasema eti vijana wa kisasa wanakula mapaja ya duniani eti kwa waliookoka watakula mapaja mbinguni du hahahaha sijui tunaelekea wapi jamani
 
Back
Top Bottom