Masanduku hewa ya kupigia kura yaandaliwa Igunga

Status
Not open for further replies.
wapi wa 16?
hahahaa!!! umeonaeee!!!
ccm AT WORK....propaganda. hakuna anyeyaamini haya tena. Machalii wapo makini, ujinga huu ukijulikana, haitakuja hapa kama taarifa ya namna hii, itakuja taarifa ya msiba kwa waliokamatwa na masanduku hayo.

Sasa hivini muda kwa wana-Igunga kucha kuchagua:
Mu+Msafiri.jpg
 
Tanzania daima jumatano

ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya wananchi wa Igunga kuamua nani atakuwa mbunge wao, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa amenasa siri nzito ya jinsi vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), walivyojipanga kuiba kura, Tanzania Jumatano limebaini.

Akizungumza na gazeti hili jana katika mahojiano maalum, Dk. Slaa alisema kwa takriban wiki moja sasa, CCM imekuwa ikifanya mbinu mbalimbali na juzi na jana walikuwa na vikao vizito kupanga jinsi ya kuiba kura baada ya kubaini kuwa chama hicho hakiwezi kushinda.

“Safari hii, CCM wamekabwa kwelikweli na ukiona mtu mzima (CCM), analalamika, ujue ameshikwa mabaya. Sasa kwa kujua hilo, wamepanga mikakati ya kuiba kura. Jana walikuwa na kikao cha siri kilichofanyika Peac Hotel na leo walikuwa na kikao kingine, mipango na kila walichojadili nimepata,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA katika uchaguzi uliopita na kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitaja mbinu nyingine ya CCM kuhakikisha inapata ushindi kuwa ni pamoja na kutengeneza kura hewa, kuchoma karatasi za kula kama walivyofanya Msalala, kununua shahada na kuwapiga wafuasi wa CHADEMA.

“Kama mlivyosikia, tayari wameanza kuwapiga watu wetu, wameanza kuwapa vitisho, vijana wanakamatwa na kuwekwa ndani hovyo ili kuwatisha,“ alisema Dk. Slaa.

Kiongozi huyo wa CHADEMA, pia alisema mbinu nyingine inayotumiwa na CCM ni kumwaga pesa na kutolea mfano wa kijiji cha Karenga ambacho kimepewa sh milioni 10 kwa kisingizio cha kutumika kwenye miradi ya maendeleo, jambo ambalo alisema sio kweli.

“Katika baadhi ya vijiji jana nilishuhudia mwenyewe watu wa CCM wakigawa mahindi. Vijiji hivyo ni Mwamwapuli, Mwamwagogo na vingine ambavyo sivikumbuki kwa sasa, kote huko waligawa mahindi ili kuwarubuni wawapigie kura,” alisema Dk. Slaa.

Hata hivyo pamoja na mbinu zote hizo za kuiba kura, Dk. Slaa alisema chama chake kimejipanga vizuri na kuwahakikisha wanachama wake kuwa hakuna kura itakayoibwa.

“Nakuhakikishia, mbinu zote tunazijua, tumejipanga vizuri sana kuhakikisha hakuna hata kura moja itakayoibwa au kuchomwa moto. Tutapambana hadi tone la mwisho na tuko tayari kufia kwenye vituo vya kupigia kura,” alitamba Dk. Slaa.

Alilitahadharisha jeshi la polisi pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa makini siku hiyo, vinginevyo taifa linaweza kuingia katika matatizo mazito sababu ya kuibeba CCM ambayo alisema kwa sasa haibebeki.

Malalamiko ya Dk. Slaa, yaliungwa mkono na Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimedai kuwa CCM ina mpango wa kuiba kura na inacheza rafu kwa kuleta malori saba ya sukari, kugawa mahindi na kuingiza Janjawid ili kuwatisha wananchi wa Igunga siku ya kupiga kura.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, aliliambia gazeti hili kuwa malori hayo yako njiani kutoka Mara kuelekea Igunga kwa lengo la kugawa kwa wapigakura.

“Kwa sababu vyombo vya dola ukiripoti havitachukua hatua kwa vile wanailinda CCM, tumejipanga vya kutosha kuyadhibiti malori hayo, tunazo taarifa za kutosha tunajua yamelala wapi juu wameweka nini, chini wameweka nini.

“Tumewapanga vijana wetu na tutayakamata kwa nguvu zetu kisha tutawaonyesha waandishi wa habari na taifa lione, tunatoa tahadhari kwamba mbinu zao zimegundulika, makontena ya sukari yanaletwa Igunga ili kuigawa siku mbili kabla ya kupiga kura.

“Hatutakubali haki za Watanzania kuchagua kiongozi bora ziondolewe kwa sababu ya kilo za sukari…tunalishughulikia hili,” alisisitiza kiongozi huyo wa timu ya kampeni za CUF Igunga.

Aidha, ameionya CCM kuacha mpango wa kutaka kugawa mahindi Septemba 30 na Oktoba mosi kwa wakazi wa jimbo hili kwa kuwa hiyo ni rushwa wanayoitoa kwa mgongo wa njaa.

“Hapa tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuingilia kati; CCM imepanga miundombinu ya kuhakikisha wakazi wa jimbo zima la Igunga wanapatiwa mahindi; wanayo magari ya kutosha ya kugawa mahindi licha ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kutetea jukumu hilo.

“Huwezi kuikamata serikali; inasema hapa pana njaa tumeliacha. Tunalo tatizo kubwa; walikua wanayagawa mahindi hayo kwa ngazi ya kata sasa wanataka kuwarubuni wapigakura kwa kugawa tena kwa jimbo zima.

“Kama watu wameweza kukaa kipindi chote hicho wakiwa na njaa hawawezi kufa tarehe 30 na tarehe mosi tuwaache wakapige kura halafu CCM wapite wagawe mahindi yao tarehe 3 hapo hatuna shida lakini wakiendelea na mkakati huo tumejipanga kuwazuia wasigawe mahindi hayo,” alisisitiza Mtatiro.

Naibu katibu mkuu huyo amelalamikia pia vitisho vinavyotolewa na vijana wa CCM aliowataja kuwa ni Janjawid ambao wamemaliza semina yao mjini Shinyanga huku akidai kuwa wataingia mjini Igunga leo usiku.

“CCM tumewakalia maji ya shingo hivyo wanahitaji vijana hao wafanyekazi ya kutengeneza vitisho kwa wananchi ili wasijitokeze kupiga kura hasa kwenye maeneo ambayo hawaungwi mkono.

“Tathmini yetu kwenye uchaguzi huu inaonyesha kati ya kata 26 tumebaini CCM hawaungwi mkono katika kata 19 kwa hiyo msistuke hapa tarehe 30 mkakuta watu wamekatwakatwa mapanga ili wasiende kupigakura…

Alisema wamejipanga kudhibiti wizi wa kura kwa kuwa na majina ya wapigakura kwenye vituo vyote 427 vya jimbo la Igunga, huku akiitahadharisha CCM kutafuta mbinu nyingine ya kuiba kura.

Akizungumzia madai ya CUF kwa njia ya simu, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Mungulu, amekana kupokea taarifa za Janjawid.

“Siku zote nasema hawa wanasiasa wanatuingiza kwenye propaganda zao, sisi polisi hatuna taarifa zozote kuhusu madai ya CUF wala Janjawid labda wamepeleka kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo,” alisema kamanda Mungulu.

Kwa upande wake mratibu wa kampeni za uchaguzi wa CCM Igunga, Mwigulu Mchemba, alisema hakuna sukari inayoletwa Igunga kuja kugawiwa kwa wananchi huku akisisitiza kuwa ugawaji wa mahindi umeratibiwa na serikali kwa maeneo yote yaliyokuwa na upungufu wa chakula.

Katika hatua nyingine, siku chache baada ya kikundi cha watu waliojiita viongozi wa Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) wilaya ya Igunga, kutoa tamko la kuwataka Waislam wilayani hapa kutoipigia kura CHADEMA, siri imefichuka kuwa watu hao ni makada wa CCM.

Habari za uhakika kutoka katika chanzo cha kuaminika kilicho ndani ya kundi hilo zinasema kuwa kikundi hicho hakikuwa na dhamira ya kweli ya kutetea Uislam kama walivyodai mbele ya waandishi wa habari, bali kilikuwa na ajenda ya kisiasa kikitumiwa na CCM ili kuidhoofisha kisiasa CHADEMA.

Kufuatia madai hayo ya kuvuliwa hijabu, Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) wilaya ya Igunga, lilitoa tamko kulalamika na kulaani kile walichokiita kunyanyaswa na kudhalilishwa kwa mwanamke wa Kiislam, DC Kimario.

Kufuatia kutolewa kwa tamko hilo lililoonekana wazi kubeba ajenda ya kisiasa, gazeti hili lilianzisha uchunguzi wake ambao umebaini kuwa watu hao ni wanasiasa kutoka vyama vya CCM na CUF ambao baadhi yao ni viongozi wakuu hapa wilayani.

Kwa mfano, mmoja wa watu hao, Maulid Athuman Mussa, aliyejitambulisha kama katibu wa Bakwata wilaya ya Igunga imebainika kuwa ni katibu wa wilaya wa chama cha waananchi (CUF).

“Ndugu mwandishi ulikuwa sahihi kabisa uliposema walikuwa wakisukumwa na jambo lililojificha nyuma ya pazia, ukweli ni kwamba wenzetu ni wanasiasa kabisa, wengi ni makada wa CCM na yule katibu wa wilaya wa Bakwata ni katibu wa CUF, walitumiwa tu na CCM kuidhoofisha CHADEMA, wengine tulikuwepo pale kama bendera fuata upepo,” kilisema chanzo chetu hicho.

Mussa alionekana dhahiri kuwa na msukumo wa kisiasa wakati alipokuwa akisoma hicho kilichodaiwa kuwa tamko la Waislam, na ndiye aliyesababisha mkutano huo kuvurugika baada ya kukataa kujibu maswali ya waandishi wa habari.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa karibu watu wote waliokuwepo katika mkutano huo wa waandishi na kujitambulisha kwa nyadhifa mbalimbali za uongozi wa Bakwata wilayani hapa, ni makada wa CCM na baadhi yao wamewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa chama hicho wilayani hapa.

Mwandishi wetu alimfuatilia mmoja wa watu hao na kufanikiwa kupaona nyumbani kwa kada huyo wa CCM ambako ilikuwa ikipepea bendera ya chama hicho, hali inayothibitisha pasipo kuacha chembe ya shaka kuwa mtu huyo ni kada wa CCM.

Ijumaa, Septemba 23, mwaka huu, watu waliojiita viongozi wa Bakwata wilaya ya Igunga, waliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwa lengo la kutoa tamko la kulaani kile walichodai tukio la kuvuliwa hijabu mama wa Kiislam, Fatma Kimario, ambaye ni mkuu wa wilaya ya Igunga.

Helikopta nne zatikisa Igunga

Katika hatua nyingine, anga la mji wa Igunga na viunga vyake limeanza kutikiswa na helikopta nne za vyama vya siasa zilizokuja kumalizia kampeni za lala salama.

Vyama vinavyotumia helikopta ni pamoja na CHADEMA yenye helikopta moja, CCM mbili na CUF ambacho ni mara ya kwanza kutumia usafiri huo kwenye kampeni, kina helikopta moja.

Habari zaidi kutoka Igunga zinasema kuwa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ambaye alizindua kampeni za CCM, atawasili tena Igunga kwa ajili ya mkutano wa mwisho wa kufunga kampeni hizo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom