Marufuku walimu waliogoma kushiriki sensa - serikali!

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Taarifa kutoka TAMISEMI, kwenda kwa maafisa wa Takwimu kwa njia ya fax, zinasema kuwa Waalimu walioshiriki mgomo wasiandikwe kusaidia katika zoezi la sensa. Je bila waalimu zoezi hili litafanikiwa?

Kuna kundi gani katika jamii lenye kufanya kazi hiyo kama sio waalimu? je serikali itabagua kuwaacha wale walioenda kufundisha wakati wa mgomo? Kama waalimu hawatashiriki sensa kuna haja gani shule kufungwa?

Nawasilisha kila mtu afuatilie kule alipo ila barua hiyo iliyotumwa kwa fax nimeiona, nikipata mwanya nitaleta hapa jamvini.
 
Ni kweli kabisa Walimu waliogoma hawatashiriki Sensa kwa hofu kwamba watahujumu zoezi zima lakini pia kama adhabu. Na kwa kuongezea kuna mkakati wa kuwaadhibu Walimu wote walioshiriki kwenye mgomo.

Majina yalitakiwa yawe yamefika TAMISEMI jana saa 7 mchana yakiambatanishwa na Check No na TSD Na. kwa hatua zaidi.
 
Yaah..kuna washikaji zangu waligoma..wameambiwa watume TSD NO na afisa elimu
 
sasa kama hawakutaka wagome, walinda mahakamani kufanya nini? si wangetoa amri tanzagu J3 kuwa lazima wafanye kazi suala la mgomo kudai mishahara halipo na halitumiki kudai haki Tanzania.... ngoja tujiande na vita na malawi sasa
 
Du kweliii mi nafikiri kama walimu wata achwa kwenye hili zoezi la sensa, kwa madai kwamba watahujumu sijui mitihani ya Taifa ya darasa la saba itakuwaje watasimamia watu wengine tofauti na walim?
 
Visasi kwa kwenda mbele.Watu wazima wanafanya mambo ya kitoto.Tusubiri tuone huu mziki wa CD 700.
 
Bora vijana walioko mtaan wapate kazi la Sensa.....Idadi ya Vijana waliomaliza vyuo vikuuu hawana kazi ni kubwa sana kama walimu wakigoma na kuchukuliwa vijana waliomaliza vyuo itatosha na wengine watabaki kitaaaa
Serikali Sikivu kweli nimeamini sikivu... Walimu wote waliogoma wasishiri sensa,, ila tangazeni nafasi hizo ziombwe vijana wajaze
 
Du kweliii mi nafikiri kama walimu wata achwa kwenye hili zoezi la sensa, kwa madai kwamba watahujumu sijui mitihani ya Taifa ya darasa la saba itakuwaje watasimamia watu wengine tofauti na walim?

Mitihani ya taifa sasa hivi itatungwa na mabwana afya na mabibi afya na kusahishwa na ma DC.
 
Safi sana ni vizuri walimu wakiachwa kwenye zoezi lote la sensa wawatumie graduates, form six na form four hao si wamegoma bwana waendelee tu na mgomo wao.

Hivi jamani kiukweli graduates ambao hawana ajira hawawezi kufanya kazi ya sensa wakipewa semina ni ukweli uliowazi wanaweza tena sana zoezi la sensa liendelee kama kawaida tusiyumbishwe na tamaa za watu wachache kama wao wenyewe waliomba hizo kazi bila kulazimishwa wakijua wazi mshahara wake ukoje iweje leo watake mshahara mnono.

Raisi Jakaya Kikwete alishasema wazi huna haja ya kugoma kumsumbua muajiri ukiona masilahi madogo na hayakutoshelezi acha kazi nenda kuliko na masilahi mazuri zaidi hata ukitaka ubunge kwa kuona wao wana masilahi mazuri acha kazi kagombee ubunge uwe mbunge.

Jamani walimu acheni kazi nendeni kuzuri msisumbuke bure hayo madahi yenu hayatekelezeki mnajidanganya bure; mwanzoni mwa mgomo watu walikuwa wanajua mnadai madai yenu ya miaka mingi kumbe yale madai yenu yote mmeshalipwa mmetafuta sababu nyingine na kwa kuwa mnatumika kisiasa mmeleta madai mapya mnataka mshahara uongezeke kwa 100% na posho ya mazingira magumu 30% na posho nyingine jumla mnataka nyengeza ya 180% kwenye kipato chenu.

Kwa sasa kaeni mkijua haiwezekani hasiyetaka aache kazi vinginevyo mtaachishwa na kupewa kazi wengine itakuwa kama ilivyowakuta madaktari na katika hili naiunga serikali mkono ichukue hatua stahiki kukomesha tabia kama hiyo!
 
serikali iache kuwatisha walimu maana wakiendelea kugoma Taifa litaharibika sana. Hakuna kitu kibaya kama mgomo baridi; walimu wanaweza potosha watoto wetu, mfano mwalimu anafundisha hesabu 1 + 1 = 11
20+0 = 200 nk.
hapo kutakuwa na taifa?
 
Binafsi nadhani kuna maamuzi mengine yanatolewa na wakubwa(serikali) bila kufanya tathmini ya kina na madhara yake hapo baadae inawezekana wao hayo maamuzi hayana madhara kwao kwa namna yoyote ile tumeona jinsi mgomo wa madaktari ulivyozimwa na kauli za liwalo na liwe sasahivi tunashuhudia walimu wameingia kwenye kasumba kama madaktari.

Ukitazama kwa jicho la makini utaona sio watoa maamuzi au jamaa zao wanaoathirika na maamuzi yao mfano suala la huduma na kukosekana kwa vifaa mahospitalini,wao wakiugua wanapelekwa nje ya nchi wakati watanzania walio wengi wanaenda kwenye hizi hospitali zetu zisizo na vifaa vivyo hivyo katika suala la walimu watoto wao na jamaa zao wanasoma shule za St.Masawe ambako hakuna migomo wengine wanasomeshwa ughaibuni na isitoshe kwa kodi tunazolipishwa sisi watanzania wenye kuhangaika juani kutwa kuchwa tukitafuta riziki.

Nasema haya sio kwamba naunga mkono migomo mbalimbali inayotokea hapa bongo lakini nadhani ndio njia ya kuwafanya watawala waweze kuamka kutoka usingizi wa pono na sisi wabongo(hasa tuishio vijijini) kwa kweli tumelala sana hatuna budi kuamka kutoka katika lindi la usingizi ambao tunaogelea humo.
 
Mimi ningeiona serikali ipo makini kama ingekua inajitahidi kufanya mambo kwa uharka kwenye kushughulikia mambo muhimu,mawaziri waliokwiba pesa hadi leo hwajaguswa,majangili kibao hawajakamatwa like wezi wa wanyama wetu,ila kwa walimu wanawakomalia had weekend na kudan wanwakomoa,hapo hawawakomoi walimu wanadeal na walim na familia zao,na si kweli wamba waziri wa TAMISEMI atajihisi kuwa anafanya kazi kwakuwakomoa walimu,yeye ataonekana wa maana endapo atafanikiwa kuwaharkishia madni wanayoidai serikali
 
Maamuzi yale yale ya kukomoana!!! Sijui kukomoana huku ni kwa faida ya nani!!!!?
 
Back
Top Bottom