Marufuku walimu waliogoma kushiriki sensa - serikali!

Nashukuru kama kuna watu wanasapoti maamuzi ya serikali kwamba wasiyumie walimu kny sensa maana na hao ni wapumbavu.
Kuna shule zipo vijijini sana ambako hata kama utapeleka graduates watakimbia baada ya siku mbili kutokana na kutokuwepo kwa huduma za maana
 
Kudai hiyo kazi ni kujidhalilisha. Walimu acheni kujidhalilisha hakuna kazi za kufanya huko makwenu? Hata mitihani watafute wanaf. wa vyuo.
 
Wangejua Hakuna mwenye haja ya kuhesabiwa wangeahirisha hata iyo sensa kwani haina tija zaidi ya kuchezea kodi zetu
 
panadol

Sikiliza wewe I went for national ID registration nilio wakuta huko kama ni kada ya kidacho cha nne au sita na Chuo Kikuu basi hata ku spell ni issue let alone kuandika majina ya sehemu na watu kwa usahihi. Elimu za kata na kukariri Chuo kikuu ?
 
Last edited by a moderator:
Walimu na nyie mlizidi mnadeka km watoto wakati mlijua kuna Sensa, sasa na huyo Gratian Mkoba mwambieni hata walimu wa UPE tupo tumwagieni mitaala tutafundisha tu kwa SENSA KAENI PEMBENI muone uchungu ikiisha mrudi madarasani baada ya kukatwa siku mlizogoma. wenzenu huko Iringa walishamshtukia Kiongozi wenu kuwa huu mgomo lazima atakata panga michango yenu.
 
wewe kweli panadol! kuacha kazi sio hoja ya msingi kwani humo duniani watu wanapigania haki na kutafuta angalau usawa katika mambo mbalimbali. so walimu kugoma ni harakati za kutetea haki zao na si vinginevyo, laiti watu wangekuwa na mawazo ya kukimbia matatizo kama wewe, basi wengine wangekimbia hata familia zao wakati wa shida!Rai yangu kwa WAALIMU waendelee kugoma mpaka kieleweke kwani kila aliyefanikiwa kwenye hii duniani alitumia juhudi,nguvu na maarifa japo wakati mwingine aliingia matatani.
 
Sensa ya mwaka huu ni utata mtupu! tutapata takwimu zile zile za kubahatisha zenye ukweli mdogo maana limeingia doa toka mwanzo.
Mara waislamu wasishiriki mara walimu waishiriki. Haya bwana ngoja tuone
 
Ni kweli kabisa Walimu waliogoma hawatashiriki Sensa kwa hofu kwamba watahujumu zoezi zima lakini pia kama adhabu. Na kwa kuongezea kuna mkakati wa kuwaadhibu Walimu wote walioshiriki kwenye mgomo. Majina yalitakiwa yawe yamefika TAMISEMI jana saa 7 mchana yakiambatanishwa na Check No na TSD Na. kwa hatua zaidi.

Nchi hii ukishaamua kutetea haki yako hakuna kurudi nyuma, waalimu sasa wataandamwe na kila mabaya tutayasikia juu yao - kisa wamethubutu kudai haki yao. wanachosahau watawala wetu ni kuwa kutawala kwa ujanja hakudumu hata siku moja
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Visasi kwa kwenda mbele.Watu wazima wanafanya mambo ya kitoto.Tusubiri tuone huu mziki wa CD 700.

sijui serikali hii imejaa watu wa aina gani? Yaani serikali inalipa kisasa kwa maticha.aisee visari kwenda mbele.watu wazima ovyo.
 
panadol;

Hv unajua nn unachokisema ama unaropoka maana usichokijua ni asawa na usiku wa giza. Ni nani anayepanga Mwalimu alipwe kidogo, asiwe na allowance alhali kada zingine za watumishi wawekewe mishahara mizuri na allowances za kutosha?
Furaha ya Mpumbavu ni Upumbavu Wake (Sijakutukana)
 
Last edited by a moderator:
Sasa ni mtindo wa 10+0=100,!150-50=1!!Mpaka kieleweke!wasitumie sensa km njia ya kuwapooza walimu au fimbo ya kuchapia walimu!serikali inatakiwa iangalie athari zitakazotokea mbelen!Tatizo serikali dhaifu hainaga vision ya mbali!Tutajazalisha taifa lenye wasomi lakin mambumbu!
 
Serikali ya wajinga hii I wont be surprised yule kilaza wa magogoni kukataa kura za waalimu kwa Magamba party
 
Serikali ya wajinga hii I wont be surprised yule kilaza wa magogoni kukataa kura za waalimu kwa Magamba party

azikatae mara ngapi?au umesahau.
Ni vile tu watu ni wagumu kuelewa.YOU CANT PUSH ARROUND THE PRESDENT.
 
Duh!! hata haka kamshahara hakafiki trh 7, na sensa anataka kutunyima...
 
Taarifa kutoka TAMISEMI, kwenda kwa maafisa wa Takwimu kwa njia ya fax, zinasema kuwa Waalimu walioshiriki mgomo wasiandikwe kusaidia katika zoezi la sensa. Je bila waalimu zoezi hili litafanikiwa? Kuna kundi gani katika jamii lenye kufanya kazi hiyo kama sio waalimu? je serikali itabagua kuwaacha wale walioenda kufundisha wakati wa mgomo? Kama waalimu hawatashiriki sensa kuna haja gani shule kufungwa? Nawasilisha kila mtu afuatilie kule alipo ila barua hiyo iliyotumwa kwa fax nimeiona, nikipata mwanya nitaleta hapa jamvini.

Na VIPI Wabunge - MAFISADI wa TANESCO wao ni MARUFUKU KUFANYA NINI?
 
Back
Top Bottom