Elections 2010 Marmo apigiwa yowe la mwizi kijijini kwao

Jack Beur

JF-Expert Member
Feb 26, 2010
222
246
Ndugu wanaJF, nimesafiri kikazi nipo eneo la Mbulu mjini,top story hapa mjini ni kuhusu kuzomwea na kuitwa mwizi waziri Marmo.

Habari zinasema alifika kijijini kwao katika harakati zake za kampeni kwa mbwembwe za magari yaliyopambwa picha zake na za JK na mziki mkubwa wa kwaya yao ya TOT,wanakijiji waliposikia walijikusanya na kuanza kupiga yowe la mwizi wa kura! Mwizi wa kura kwani wanamshutumu kuwa huwa anashinda ubunge kwa kuiba kura kwa miaka yote na kibaya zaidi katika kura za maoni za ndani ya CCM NEC haikurudisha jina la mgombea aliyekuwa chaguo lao.

Watu wamemchoka Marmo kupita kiasi kwani wanadai amejaa kibri na majivuno, katika mkutano wake mmoja wa kampeni eneo linaitwa Haydom alishawaambia wakazi wa eneo hilo hata kama wasipompigia kura atashinda kwa kura za watu wanaovaa mashuka wasio na elimu huko vijijini. Kilichotokea hawa watu wa Hydom wakawasimulia hao wanaoitwa hawana elimu, alipoenda kifanya kampeni wakamtimua kwamba wameishapata habari jinsi anavyowadharau, kazi anayo mwaka huu.
 
Kama Marmo ni mwizi ni dhahiri bosi wake ambaye ni JK basi ndiye mwizi hodari wa kura. Safari hii hata NEC watajuta kujenga mazingira na hivyo kulea wizi wa kura kwani hatutawapa mwanya hata kidogo.....................................
 
Marmo yupi?

Yule jamaa anashinda baa ya Tabata Mawenzi kupiga ulabu?

Kumbe na yeye anagombea Ubunge? Duh!
 
Du!, hii ni kali kama wanavijiji wameanza kuelewa elimu ya uraia, basi nchi ipo karibu kukombolewa kutoka mikononi mwa mafisadi!
 
Marmo yupi?

Yule jamaa anashinda baa ya Tabata Mawenzi kupiga ulabu?

Kumbe na yeye anagombea Ubunge? Duh!

Pia mimi sijawahi kumwona mawenzi ila Lile jimbo kalimonopolize nasikia huko kwao ndio anajiita msomi
 
Ndugu wanaJF, nimesafiri kikazi nipo eneo la Mbulu mjini,top story hapa mjini ni kuhusu kuzomwea na kuitwa mwizi waziri Marmo.

Habari zinasema alifika kijijini kwao katika harakati zake za kampeni kwa mbwembwe za magari yaliyopambwa picha zake na za JK na mziki mkubwa wa kwaya yao ya TOT,wanakijiji waliposikia walijikusanya na kuanza kupiga yowe la mwizi wa kura! Mwizi wa kura kwani wanamshutumu kuwa huwa anashinda ubunge kwa kuiba kura kwa miaka yote na kibaya zaidi katika kura za maoni za ndani ya CCM NEC haikurudisha jina la mgombea aliyekuwa chaguo lao.

Watu wamemchoka Marmo kupita kiasi kwani wanadai amejaa kibri na majivuno, katika mkutano wake mmoja wa kampeni eneo linaitwa Haydom alishawaambia wakazi wa eneo hilo hata kama wasipompigia kura atashinda kwa kura za watu wanaovaa mashuka wasio na elimu huko vijijini. Kilichotokea hawa watu wa Hydom wakawasimulia hao wanaoitwa hawana elimu, alipoenda kifanya kampeni wakamtimua kwamba wameishapata habari jinsi anavyowadharau, kazi anayo mwaka huu.
kuna mawili, either wambulu hawaaminiki au post ina ushabiki
 
Back
Top Bottom