Mariam Wangwe na Jukwaa la Wahariri

Status
Not open for further replies.
PM,

Nimesoma maelezo yako na asante kwa kufanya juhudi kutuelemisha.

Ila kwa mawazo yangu naona msimwingize huyo mama kwenye mambo ya siasa.

Kufiwa na mume tena uliyekuwa unamtegemea kwa mambo mengi ni jambo kubwa mno.
 
PM,

Nimesoma maelezo yako na asante kwa kufanya juhudi kutuelemisha.

Ila kwa mawazo yangu naona msimwingize huyo mama kwenye mambo ya siasa.

Kufiwa na mume tena uliyekuwa unamtegemea kwa mambo mengi ni jambo kubwa mno.[/quote]

To be frank, I am lost here! There are wives who butcher their husbands despite the fact that they depend on their husbands for "everything".
 
PM,

Nimesoma maelezo yako na asante kwa kufanya juhudi kutuelemisha.

Ila kwa mawazo yangu naona msimwingize huyo mama kwenye mambo ya siasa.

Kufiwa na mume tena uliyekuwa unamtegemea kwa mambo mengi ni jambo kubwa mno.

Mkuu Mtanzania nani amemwingiza nani kwenye siasa?
Kwani hizo kauli za huyo mama ni PM ameziingiza kwenye siasa ama ni mama mwenyewe?

Nina mashaka sana...Kwasababu kama huyo Deus alikuwa ni mtu wa ccm na ana mawasiliano na kina RA....Then huyu mama ambaye alikuwa akitilia mashaka uhusiano wa Deus na Wangwe wa kupigiana simu usiku wa manane...The kwanini na sisi tusitilie mashaka uhusiano wake mama huyo na Rostam?

On the other hand shahidi mkuu ni mtu ambaye anajulikana na wakubwa...Kwanini wamwachie huyo mama kusema haya mambo na wakati kijana mwenyewe aliwapigia simu viongozi wa juu na hata polisi wa rank za juu mara baada ya ajali na Wangwe kufariki dunia?

Hivi kwa akili ya wengine hapa jamvini kuwa chadema wamehusika na kifo cha Wangwe halafu ccm isiwakamate?

Kuna mgawanyiko kwenye familia hiyo na udhaifu uliojitokeza hadi akapoteza maisha yake licha ya kujuwa kuwa yuko hatarini ulisababishwa na uhusiano wake na Deus Mallya na mama huyo akiwa yuko anaangalia tu.

Sasa udhaifu huo unaendelea kuwala baadhi ya wanafamilia hiyo na ccm wameingia hadi ndani kwa kutumia udhaifu huo.

Ni opportunity ya mgawaniko ndani ya chama ulio kuwa created na chuki mbaya za kikabila....Chuki ambazo zinapandikizwa kimakusudi.

Mambo kama haya ni ya kimafia kwani hayajali ubinadamu...Kuanzia kwenye kusambaratisha chama hadi familia...Ni mbinu ya kimafioso na wanatumia dola kuzungusha maneno kwa manufaa ya kisiasa huku wakitumia nguvu ya fedha za umma kumalizia any remnants.

Na mimi binafsi ninakubaliana na wale wote wanaosema kuwa kutokutowa makala/ripoti hiyo kunaweza kuleta madhara zaidi kwasababu wananchi hawawezi kufanya maamuzi sahihi kama hawapewi taarifa sahihi.

Wananchi wana haki ya kupata habari na ni juu yao kusoma kati kati ya mistari,na kuchambuwa ili kuelewa wapi palifanyika makosa nk.

Ni ripoti wanayostahili kuipata kwasababu ni kiongozi aliyekuwa akilipwa na pesa zao.

NB:Ujumbe wangu kwa Sakina Datoo,Kubenea na R.Mengi....Kuachia shetani aendelee kutawala kwa kudai kuwa unawaepusha wananchi wasidhurike na shetani huyo...Then unaweza kujikuta na wewe ukifanya kazi ya shetani.
 
kwa nini rostam aziz asihojiwe kuhusiana na kifo cha wangwe?
kwa kuwa magazeti yake yaliandika kuhusu nadharia ya ajali za kubuni, kuwa huenda accelerator ilifungiwa jiwe, baada ya hapo mtikila naye anazungumza habari hizi.

kwa nini tuasiamini kuwa rostam azizi alifanya njama na huyu mariam wakamuua wangwe, halafu wakaanza kupandfikiza mbegu ya uhasama dhidi ya chadema, ili kuzuia chadema wasizungumzie yale mambo yake ya wizi wa pesa za epa?
 
Walitumia karata ya ukabila kupandikiza hoja ya kisiasa ndani ya chadema iliyopeleka mgawanyiko wa kisiasa na hivyo loop hole hiyo ikatumika kisiasa.
Naomba ianzishwe thread ya Deus Mallya profile na kila mtu alete data za mahusiano yake na watu wote na tunataka kujuwa handlers wake,sababu zilizomfanya kuwapigia viogogo simu nk.
Hivi kama simu angempigia mtu wa chadema mambo yangekuwaje?
ccm wamedhamiria kulichukuwa jimbo hilo by any means.
 
Wakati wa maziko, shughuli iliandaliwa na familia kwa ushirikiano na CHADEMA, chama mfiwa na Zitto Kabwe akateuliwa kuingia kwenye kamati.

Wakati wa maandalizi ya arobaini, CHADEMA haikushirikishwa kwa namna yoyote badala yake walishirikishwa CCM, NCCR, CUF na TLP.

Mimi kama mwandishi naenda mbali zaidi kuuliza maswali kuhusu yote haya ninayoona ili nisiandike tu nilichoona au kuambiwa, niandike kilivyo. Ndio maana ya habari za uchunguzi.

Msiba ulikuwa Kimakorere, lakini arobaini ilifanyika kwa Profesa DSM. Hii ni kwakuwa kule pamoja na kuwa alibaki Kaka wa Marehemu Bwana Keba lakini pia alikuwa Mke mkubwa. Na uzito usingekuwepo kama DSM. Tulipopewa nakala ya Risala ya Wanandugu, wengine tuliisoma katika jicho la uchambuzi na kuwauliza maswali mengi pale pale.

Kwa kweli kuna siasa nyingi katika huu msiba zinazofanywa na vyama vyote.

PM

Kitu kimoja kinanishangaza kwenye hii habari ni suala la arobaini.

Kadri ninavyojua mimi, Prof Wangwe ni msabato kama mimi, wasabato huwa hatuna mambo ya arobaini baada ya mtu kuzikwa na as far as I know, wakristo wengi hawana sherehe/huzuni za arobaini.

Ilikuwaje Prof Wangwe afanye arobaini ya mdogo wake (au ndio maendeleo ya kukaa Dar es Salaam miaka mingi)? Inaonekana hii arobaini ilifanywa kwa nia nyingi tofauti na maana yake. Mama Mariam huyu ana kesi kibao na mke wa kwanza wa Wangwe, mimi ningemshauri akae kimya kwa sasa ili aweke mambo ya familia yake kwenye line kwanza.

Again,

Nimeshangaa kusoma kuwa Prof Wangwe alifanya arobaini kwa mdogo wake ambaye ni marehemu (mfu)!
 
PM,

Nimesoma maelezo yako na asante kwa kufanya juhudi kutuelemisha.

Ila kwa mawazo yangu naona msimwingize huyo mama kwenye mambo ya siasa.

Kufiwa na mume tena uliyekuwa unamtegemea kwa mambo mengi ni jambo kubwa mno.

Ni kweli kufiwa na mume ni jambo zito sana, lakini ndio afikie hatua ya kuanza kutuhumu watu hadharani wakati yeye mwenyewe anakiri kuwa hana ushahidi kuwa mumewe aliuawa?
 
Ni kweli kufiwa na mume ni jambo zito sana, lakini ndio afikie hatua ya kuanza kutuhumu watu hadharani wakati yeye mwenyewe anakiri kuwa hana ushahidi kuwa mumewe aliuawa?

Kama hataki kuingizwa kwenye siasa, basi akae pembeni ili asiingizwe, lakini akiendelea kujiingiza then itakua ni fair kumchambua!
 
Siasa za tanzania naona zinaelekea pabaya kwani watu wanamtumia marehemu kwa masirahi yao binafsi, hapa hakuna cha masirahi ya marehemu zaidi ya kujinufaisha wenyewe.
 
...............huyu mama anatumika...kwanza arubaini haipo kwa wakiristo..na sana sana kuna kitu kinaitwa kuvunja tanga ambayo kwa kawaida ni siku inayopangwa na ndugu inaweza kuwa baada ya msiba pia ..ambapo watu wanaodai au kudaiwa na marehemu hujitokeza.,,warithi wa familia ,[kama kuna wosia],msimamizi wa mirathi huchaguliwa...na mambo yote mazito kifamilia ie kama una watoto nje ya ndoa lazima wawekwe wazi na mashuhuda kwenye hatua hii ili ukoo uwatambue...

kimsingi shughuli hii ya msiba [ambayo wenzetu hupenda kuiita arobaini],na wakiristo wengi tumeiga kwa wenzetu ..hutumika kwa minajili hapo juu...na sehemu muafaka ni sehemu marehemu alipozikwa ..kwa kuwa marehemu hakuzikwa dar ...hakuna mantiki ya kufanyia arobaini dar...

kigezo cha pili arobaini lazima ifanyike sehemu ambayo ndugu wengi wa marehemu wanawweza kupatikana...ie kama ilifanyika dar na watoto wote wa marehemu na wake zake wote wakaweza kufika ingekuwa na ,mantiki...lakini kama mke mke mdogo ameamua kuteka shughuli hii kwa manufaa fulani ...ni jambo la ajabu..na litaendelea kumletea migogoro huko tarime....
 
PM,

Nimesoma maelezo yako na asante kwa kufanya juhudi kutuelemisha.

Ila kwa mawazo yangu naona msimwingize huyo mama kwenye mambo ya siasa.

Kufiwa na mume tena uliyekuwa unamtegemea kwa mambo mengi ni jambo kubwa mno.

Mtanzania

Huyu Mama anajiingiza mwenyewe kwenye siasa, wala sikumtuma mimi. Yeye alikuwa CCM mara baada ya kumpata marehemu baada ya kuwa mbunge akatangaza kujiunga na CHADEMA. Siku chache kabla ya marehemu kufariki, alitangaza kuwa kuwa wakati mumewe atagombea uenyekiti wa CHADEMA yeye atagombea uenyekiti wa wanawake wa CHADEMA. Na katika ile halfa ya kuchangia yatima iliyofanyika golden tulip akajitangaza kuwa yeye ni mbunge wa viti maalum CHADEMA. Niliwahoji viongozi wa upinzani kuhusu kile walichokipeleka kwa IGP, Lipumba akasema wazi kuwa ni maelezo toka kwa huyo Mama ambayo ni maelezo hayo hayo yalikuja kusemwa baadaye na Mtikila. Waliokuwa kwenye press conference ya Mtikila. Mtikila huyu huyu wakati akizungumza na waandishi siku ile ya arobaini akiwa karibu na huyu mama alisema amepata bomu ambalo atalilipua. Halafu unajua kwamba Prof Wangwe si mama mmoja na baba mmoja na marehemu? Ni kaka yake katika ukoo tu? Sasa kwanini arobaini ikaacha kufanyika nyumbani kwa marehemu Tarime? Haya ndio maswali ambayo waandishi wenzangu wa habari za uchunguzi ni vizuri mkajiuliza na mkawauliza walengwa. Someni The African katikati ya wiki inayokuja

PM
 
...............huyu mama anatumika...kwanza arubaini haipo kwa wakiristo..na sana sana kuna kitu kinaitwa kuvunja tanga ambayo kwa kawaida ni siku inayopangwa na ndugu inaweza kuwa baada ya msiba pia ..ambapo watu wanaodai au kudaiwa na marehemu hujitokeza.,,warithi wa familia ,[kama kuna wosia],msimamizi wa mirathi huchaguliwa...na mambo yote mazito kifamilia ie kama una watoto nje ya ndoa lazima wawekwe wazi na mashuhuda kwenye hatua hii ili ukoo uwatambue...

kimsingi shughuli hii ya msiba [ambayo wenzetu hupenda kuiita arobaini],na wakiristo wengi tumeiga kwa wenzetu ..hutumika kwa minajili hapo juu...na sehemu muafaka ni sehemu marehemu alipozikwa ..kwa kuwa marehemu hakuzikwa dar ...hakuna mantiki ya kufanyia arobaini dar...

kigezo cha pili arobaini lazima ifanyike sehemu ambayo ndugu wengi wa marehemu wanawweza kupatikana...ie kama ilifanyika dar na watoto wote wa marehemu na wake zake wote wakaweza kufika ingekuwa na ,mantiki...lakini kama mke mke mdogo ameamua kuteka shughuli hii kwa manufaa fulani ...ni jambo la ajabu..na litaendelea kumletea migogoro huko tarime....

Huyu Mariam hawezi kwenda Tarime kufanya hiyo arobaini yake atapigwa mawe kama Mtikila. Kwanza kwanini sasa huyu mama asihojiwe kuhusu kifo cha Wangwe maana sasa kuna kila sababu kwamba yeye ni mtu ambaye kifo cha Wangwe kinaweza kumpa maslahi zaidi na ukaribu wake na watu fulani unaanza kutoa mwanga wa nini kinafanyika, watu ambao walianza kuelezea mazingira ya kifo, maelezo ambayo Mtikila ameendelea nayo lakini kwa kubadili wahusika wakuu kwa kuifanya kama sinema ya Kihindi.

Ni Changamoto kwa waandishi wa Tanzania kuanza kufanya utafiti wa yaliyojiri kwenye sakata zima la kifo cha Wangwe
 
Spika:Mjane wa Wangwe asikurupuke

Habari Zinazoshabihiana
• Wangwe kuadabishwa na kamati iliyojadili akina Mengi na Malima 10.02.2007 [Soma]
•

Na Hassan Abbas

SIKU moja baada ya mjane wa aliyekuwa mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe, Bibi Miriam Wangwe kuliomba Bunge liunde Tume kuchunguza mauaji ya mumewe, Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta amemtaka mjane huyo asikurupuke na badala yake aviachie vyombo vyenye mamlaka vishughulikie suala hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu jana kutoka jimboni kwake, Urambo, Tabora, Bw. Sitta alisema Bunge halina nguvu za kisheria wala nyenzo za kuchunguza utata wa kifo cha Wangwe kama alivyoomba mjane huyo.

"Hiyo si kazi ya Bunge ajue hivyo. Masuala yote yanayohusu jinai si kazi yetu kuchunguza, kuna vyombo maalum.

"Haiwezekani hata kidogo Bunge ambalo ni Baraza la kutunga sheria likajiingiza katika mgongano wa kiutendaji na vyombo vyenye wajibu huo," alisema Spika.

Juzi akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam mjane huyo wa Wangwe, alilalamikia kile alichokiita kusuasua kwa uchunguzi unaofanywa na jeshi la polisi na kuliomba Bunge liingilie kati.

"Sikubaliani na uchunguzi wa Polisi, sitaki mambo yaende hivi, leo yametokea kwa mume wangu kesho yatatokea kwa Mbunge mwingine.

"Mume wangu alikuwa mtu wa watu, mpigania haki za wanyonge na mtu wa (Samuel) Sitta (Spika wa Bunge).Nitamwandikia kumweleza msimamo wangu na wa familia kwa ujumla kuchunguyze kifo hicho," alikaririwa akisema Miriam.

Msimamo huo wa Miriam pia umekuja ikiwa ni wiki moja sasa tangu gazeti hili katika toleo lake la Jumapili iliyopita lilipomkariri, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Bw. Robert Manumba, akisisitiza kuwa mpaka sasa msimamo wa kiuchunguzi wa jeshi hilo ni kwamba mbunge huyo alikufa katika ajali ya kawaida ila akaruhusu wenye siri zaidi wajitokeze.

Akizidi kulikana ombi la mjane huyo wa Wangwe, Spika Sitta alifafanua kuwa katika utendaji kuna idara ambazo zina nyenzo na utaalamu wa kufanyakazi hiyo, ziheshimiwe.

"Hata kama tunaweza kuwa na nia nzuri katika hili lakini hatuna nyenzo, wataalamu wala nguvu ya kisheria ya kutafiti suala hili," alisisitiza Bw. Sitta.

Kutoka: MAJIRA
 
Huyu naye kaibukia wapi ? Yeye kwanza si msemaji wa familia ila mvunjaji wa familia yeye kadakia kwa juu
 
..Sitaki kuamini kuwa Mrs Wangwe anashikwa masikio na vyama vya siasa ataingia kwenye mchezo ambao hataweza kuucheza
 
Kabla ya yote ni vizuri kumuuliza huyu mama kuwa iweje alipofika tu kuona mwili wa mume wake akakimbilia card za benki. Hivi amewakilisha hizo card za benki kwa wanafamilia? Hivi uhusiano wake na wake watatu wa wangwe aliozaa nao watoto lukuki na kupambana pamoja hadi alipoukwa ubunge ukoje? Hivi iweje mama huyu na usomi wake wote pamoja na connection yake kifamilia na vigogo wa asasi nyeti nchini akae nyumbani bila ya kazi yoyote miaka yote hiyo? Hivi iweje Marehemu Chacha aanze juhudi za kuvuruga CHADEMA mara tu alipoliingia penzi la mama huyu ambaye ni mwanachama wa damu wa tabaka tawala lilojaa ufisadi?

Hivi sio huyu mama ndiye aliyekuwa akisaidiana na GACHUMA, Binamu wa Marehemu Mzee KEBA aliyesimamia kifungo cha Chacha gerezani wakati ule, na mawaziri wa CCM akiwemo Mama Kabaka kusammbaza sumu za kuwa Chacha aliuawa na maadui ni CHADEMA? Sasa alitegemea nini kutoka kwa viongozi wa CHADEMA wakati ni yeye aliyekuwa akiwalisha sumu ya chuki hadi wanafamilia ambao ukitoa kada KEBA hapo kabla hawakuwa na tatizo na wanaCHADEMA? Labda akamuulize RPC na RC ni kwa nini walimwambia kuwa hawatakuwa responsible na USALAMA wa Mbowe wakati ndio jukumu lao....

I mean kama huyu mama aliweza kuwa kipenzi cha wapinzani hovyo kina MBATIA, MREMA, LIPUMBA waliodandia lifti ya ndege ya MBOWE halafu wakafikia kumgeuka na sasa MTIKILA....ninamini kuwa hii inaweza ikawa missing link inayotafutwa kwa wale wenye kuamini kuwa marehemu Chacha hakufa kifo cha ajali ya kawaida....

Naamini huyu mama ndiye wa kubanwa maana ana mengi ya kufill the gaps haswa kuhusiana na watu ambao Marehemu Chacha Wangwe alikuwa akikutana nao mara kwa mara wiki chache kabla ya kifo chake....

Na pia tuangalie ajira halisi ya mama huyu........
 
Nakubaliana na wachangiaji watatu hapo juu...Ila TZ Njema sikubaliani na wewe kumponda Mrema hata kidogo.
PM nakubali kuwa mume akifa mtuhumiwa wa kwanza ni mke...And vice versa.
Hivyo kama ni kweli kuna uwezekano wa marehemu kuuwawa...then ni lazima wa eliminate wake zake kwanza kabla ya kuchunguza wengine...Ndiyo utaratibu huo na Mama anaulilia.
 
Kabla ya yote ni vizuri kumuuliza huyu mama kuwa iweje alipofika tu kuona mwili wa mume wake akakimbilia card za benki. Hivi amewakilisha hizo card za benki kwa wanafamilia? Hivi uhusiano wake na wake watatu wa wangwe aliozaa nao watoto lukuki na kupambana pamoja hadi alipoukwa ubunge ukoje? Hivi iweje mama huyu na usomi wake wote pamoja na connection yake kifamilia na vigogo wa asasi nyeti nchini akae nyumbani bila ya kazi yoyote miaka yote hiyo? Hivi iweje Marehemu Chacha aanze juhudi za kuvuruga CHADEMA mara tu alipoliingia penzi la mama huyu ambaye ni mwanachama wa damu wa tabaka tawala lilojaa ufisadi?

Hivi sio huyu mama ndiye aliyekuwa akisaidiana na GACHUMA, Binamu wa Marehemu Mzee KEBA aliyesimamia kifungo cha Chacha gerezani wakati ule, na mawaziri wa CCM akiwemo Mama Kabaka kusammbaza sumu za kuwa Chacha aliuawa na maadui ni CHADEMA? Sasa alitegemea nini kutoka kwa viongozi wa CHADEMA wakati ni yeye aliyekuwa akiwalisha sumu ya chuki hadi wanafamilia ambao ukitoa kada KEBA hapo kabla hawakuwa na tatizo na wanaCHADEMA? Labda akamuulize RPC na RC ni kwa nini walimwambia kuwa hawatakuwa responsible na USALAMA wa Mbowe wakati ndio jukumu lao....

I mean kama huyu mama aliweza kuwa kipenzi cha wapinzani hovyo kina MBATIA, MREMA, LIPUMBA waliodandia lifti ya ndege ya MBOWE halafu wakafikia kumgeuka na sasa MTIKILA....ninamini kuwa hii inaweza ikawa missing link inayotafutwa kwa wale wenye kuamini kuwa marehemu Chacha hakufa kifo cha ajali ya kawaida....

Naamini huyu mama ndiye wa kubanwa maana ana mengi ya kufill the gaps haswa kuhusiana na watu ambao Marehemu Chacha Wangwe alikuwa akikutana nao mara kwa mara wiki chache kabla ya kifo chake....

Na pia tuangalie ajira halisi ya mama huyu........

Mwaka jana niliwahi kuandika hapa hapa .Kwanza asante sana ndugu Tanzanianjema kwa uchambuzi wako mfupi ila una mwaga nyeti kibao.

When I met late Chacha Wangwe siku hiyo pale Hotel G & G Musoma , ilikuwa jioni moja baada ya wao kuwa wametoka Jimboni kwao .I had sometime kusema na huyu mwanamke nikagundua she was a looser na mtu aliyekuwa anavizia jambo fulani .Alionyesha chuki za wazi juu ya Chadema na hasa Mbowe na huku akitaka kuniaminisha kwamba Chacha alifaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema .Alionyesha chuki za wazi kwa Zitto na wakataka kunilisha sumu dhidi ya Zitto lakini wakashindwa maana walishindwa kunijibu maswali yangu.

Yule mama uwezo wake wa kufikiri nafikiri una kikomo kikubwa so leo akianza kuingia hapa na kusema haya sitashanagaa kama Prof Wangwe na Kebe walivyo panda jukwaani na kusema waligundua wao kwamba mbavu zimevunjwa .What a shame .Kwa mtu kama Prof .Wangwe we all know kwamba ni mwana CCM na mshikaji wa karibu wa JK lakini sikutegemea ajivue nguo kisa CCM wapate jimbo .

Huyu Mama ana mengi na ni mty hatari si kwa umma pekee bali hata familia ya Marehemu Wangwe .Ni yeye aliyekuwa na mawazo ya kumwambia wangwe kwamba awe mkombozi wa Chadema maana Mbowe kashindwa kuongoza na kuleta majungu na maneno ya ukabila ambao leo hii pamoja na Wangwe kushindwa kuonyesha Ukabila ndani ya Chadema lakini hata yeye hana kusimamia juu ya ukabila.
 
Mwezi uliopita katika debate moja jamaammoja alisema kwamba vyamavya siasa haswa vya upinzani vinategemea upepo wavyombo vya habari ndio na vyenyewe viibuke vianze kusema na kadhalika ---ni kweli si unaona hii ya mrs wangwe ? Ni vyombo vya habari vimemwandika sasa chadema inataka kuchukulia credita hapohapo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom