Marekani kuzalisha kawi ya Nuklia

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
Rais wa Marekani Barack Obama, ameunga mkono kutengenezwa kwa vinu vya kuzalisha kawi ya nuklia nchini humo baada ya kipindi cha miongo mitatu.
Rais Obama amesema Marekani inahitaji kuzalisha kawi safi ya nuklia ili kuweza kukidhi mahitaji yake na pia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.

Rais wa Marekani pia ameahidi kusimamia mkopo wa dola bilioni nane utakaotumika kugharamia ujenzi wa kiwanda cha kwanza lakini sharti kuwepo sheria itakayolinda uharibifu wa mazingira kuambatana na mpango huo.

Uamuzi huo hata hivyo umekosolewa na kundi la wanaharakati wa kupinga uzalishaji wa nguvu za nuklia, lijulikanalo kama Beyond Nuclear. Wanaharkati hao wanamesema mpango huo haupaswi kutekelezwa.

http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2010/02/100217_us_nuclear.shtml
 
Back
Top Bottom