Marafiki wachungwe ktk mapenzi.

ISSA SHARAFI

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
407
75
Naomba msaada wenu wa mawazo wanajf, niko ktk mahusiano na msichana mmoja kwa muda mrefu sana na niko na mipango naye yaani nahitaji kumuoa lkn kuna rafiki yangu mmoja ambaye anamsumbua sana huyo mpenzi wangu kwa kumtaka kimapenzi hata kama amemwambia kuwa yeye ni mchumba wa mtu yaani mimi ila jamaa anamlazimisha eti awe spea tairi. Je nifanye nini mwenzenu?
 
Haikuhusu,ni suala la mpenzio na uaminifu wake.Hata upande kichaa huwezi kumzuia mpenzi wako kufanya lolote!
 
Niamini-kuna jinsi huyo 'mchumba' wako akijiweka huyo rafiki yako hawezi kumsumbua...huyo atakuwa attention seeker. Na ukiona kaacha kukuhadithia kuhusu huyo rafiki yako jua ushaumizwa
 
Naomba msaada wenu wa mawazo wanajf, niko ktk mahusiano na msichana mmoja kwa muda mrefu sana na niko na mipango naye yaani nahitaji kumuoa lkn kuna rafiki yangu mmoja ambaye anamsumbua sana huyo mpenzi wangu kwa kumtaka kimapenzi hata kama amemwambia kuwa yeye ni mchumba wa mtu yaani mimi ila jamaa anamlazimisha eti awe spea tairi. Je nifanye nini mwenzenu?

...Yanini kuwa na rafiki ambaye anataka kukutenda kiasi hicho!? Rafiki yako wa kweli hawezi kufanya upumbavu kama huo.
 
Siku akimkubalia usitegemee akusimulie...akubal ameet nae af muende wote mumchambe atakoma tu,tena kama ana mpenz nae mumtishie kumwambia
 
Huyo si rafiki; ni adui.
Au ndio umekuwa mtindo wenu wa kuchukuliana wasichana?
 
Wewe ni mwanaume bana!tafuta evidence then mface huyo rafiki yako live ukiwa na vithibitisho then mwambie "wewe hapana taka yeye vizia mali zako" asipokuelewa huyo sio rafiki bali mnafiki tu!
 
Kaka hapo cha msingi usiwe na haraka na hiyo ndoa,mwambie malengo yako huyo msichana kuwa unataka kumwoa,halafu endelea kuwachunguza kwa mda,najua kama msichana ana msimamo na akampa jamaa makavu najua huyo jamaa atakuogopa na urafiki utaisha.Kama girl wako amekubali ombi la jamaa basi uachane naye mana hata baadaye kwenye ndoa atakuwa kikwazo
 
Wewe ni mwanaume bana!tafuta evidence then mface huyo rafiki yako live ukiwa na vithibitisho then mwambie "wewe hapana taka yeye vizia mali zako" asipokuelewa huyo sio rafiki bali mnafiki tu!

ni suala ambalo liko ndani ya uwezo wa huyo dada mwenyewe au na yeye ni dizaini ya sitaki-nataka?
 
Mwambie huyo dada amalizane nae mwenyewe, kuna namna ya kumwambia mtu HAPANA akakuelewa.

Mama Ashrat wasichana wengi wanajua vizuri jinsi ya kumwambia mtu na akaachana naye,ila kama anakuwa mkimya ujue msichana mwenyewe atakakuwa anataka
 
Sioni tatizo kwa mpenzio kutongozwa na c suala la kukuumiza kichwa kwa sababu hata kabla ya kuwa na wewe alishatongozwa na wengine lakini ameamua kuwa na ww au umefungua mlango?

We unaelewa fika jinsi baadhi ya wanaume walivyo vinganganizi, cha msingi ni kumwambia huyo mpenzi wako asipokee simu yake, asijibu sms, asikutane naye katika mazingira yoyote ambayo yanampa nafasi ya kuongea naye(faragha).

Kwa kuwa hajawa mkeo mwache alishughulikie mwenyewe ww uwe mshauri tuu, unaweza kutumia nguvu kubwa kesho ukabwagwa na wakaanza uhusiano itakuumiza sana.
 
Huyo anataka kukazia uchumba tu; sisemi kama anasema uongo ila amechukulia udhaifu wa rafiki yako kama dili la kukufanya uharakishe mambo ya harusi kwani wengi wanamtamani. Ujajua wasichana wanaopenda ndoa wewe.
 
Unajua tunatofautiana. Mimi rafiki sijuhi kaka wa mchumba wangu angenitaka aisee ningejiuliza mambo mengi saaana. Yani amenichukulia rahisi sana(dada poa). Hilo ni bonge la dharau na wala nisingemwambia mtu; ningemchimba biti kali baadae nauchuna. Am sure asingerudia tena.

Unajua kusimulia simulia sijuhi nani kanitaka, nani kanitaka inaonyesha kuna satisfaction unayosikia ukitakwa. Kwa lugha rahisi ana enjoy kutakwa.
 
Unajua kusimulia simulia sijuhi nani kanitaka, nani kanitaka inaonyesha kuna satisfaction unayosikia ukitakwa. Kwa lugha rahisi ana enjoy kutakwa.

probably anataka kumwonyesha jamaa kwamba yuko kwenye kiwango na ni marketable...
 
hiyo usiingilie kabisa mwachie mwenyewe...mm rafiki yangu wa karibu ilimkuta hiyo,binti alikuwa anamwambia jamaa anasumbuliwa na rafikie,jamaa akagombana na rafikie...baadae akaja kugundua binti yule akitoka na jamaa...so kama kweli anakupenda hapo ndo utamsoma uaminifu wake umefikia wapi....
 
Back
Top Bottom