Wrevta
JF-Expert Member
- Jan 18, 2023
- 1,440
- 1,720
Habari zenu nyote, najua kila mmoja anapitia matatizo yake kivyake ila naomba nipate kibali cha kushauriwa juu ya tatizo langu hili.
Baba zangu, kaka zangu, dada zangu, na rafiki zangu wa MMU; Mimi nina miaka 25 na sijawahi kuwa na mpenzi ingawa ngono ninashiriki kama kawaida.
Nina anxiety, ninapata wapenzi safi tu na wapo wanaoonesha kunipenda ila shida ni pesa, sina pesa za kutosha kuwatosheleza slay queens wa sasa, je, nitadumu nao?
Kuna kaka alileta stori humu kuwa alimnyang'anya rafiki yake mpenzi siku ya sherehe ya kuzaliwa ya mpenzi huyo. Kisa kikiwa ni pesa. Yaani huyo brother na rafiki yake walikwenda ukumbini na kukuta mgogoro, pesa ya sherehe ya mpenzi wake haikutosha na mwenye ukumbi anataka kuwatoa nje.
Huyu brother hakuwa na hela ya kutosha kujazia deni la ukumbi, hivyo rafiki yake akatoa kiasi akajazia (ni kama laki moja hivi), na usiku huo akamlala shemeji yake huyo. Na urafiki wao ukafa siku hiyo. Mapenzi kati ya huyo brother na mpenzi wake yakafa siku hiyo.
Naogopa mno hiki kunikuta. Nafanyaje? Kuwa na mpenzi siyp shida ila je, nitadumu nao na wakati ninasoma, na hela yangu ni ya kuunga unga? Yaani 'pesa ya madafu'?
Nitaweza kumnunulia zawadi za kuanzia laki moja kila birthday yake? Nitaweza kumrushia vocha za 20000 kila akiishiwa salio? Nitaweza kumpeleka lodges na hotels nzuri? Achilia mbali gharama za beach nk!
Naomba mnisaidie maoni yenu... uoga huu umefanya nisiwe na mahusiano mpaka muda huu. Nafikiria mno, wasichana wazuri wanahitaji pesa, mimi nategemea wazazi bado kwa sababu nasoma na sifanyi kazi, wapi nitatoa laki mbili mbili za vacation?
Pia, mimi ni mpole mno na nahitaji nibadilike niwe katili angalau hata kidogo ila naona naharibu tu. Nikisema nijaribu kuwa muongeaji au mcheshi najikuta naharibu tu na kujisikia vibaya, na kuamua kuirejea asili yangu ya ukimya na upole.
Maoni yenu ni muhimu sana. Inafika wakati naona wivu(si wivu mbaya) humu watu wanavyofunguka kuwahonga mamilioni wapenzi wao na hawalalamiki, kumaanisha kuwa wanazo hela za kutosha. Najisikia vibaya kiasi, na kupata hasira ya kutaka kupambana nizishike hela.
Sijawahi hata kutoa 10000 na kumpa msichana. Kuna wakati nawaza hata niwe punda tu wa kusafirisha drugs ili nipate pesa ninazotaka, ili niwe kwenye mahusiano ya kudumu na nipate tendo bila kipimo. Anyways nasikiliza ushauri wenu.
Njia ipi ni sahihi kwa sasa? Uelekeo upi ni sahihi? Nina haja ya kuwa na mahusiano ya kudumu, yatakayonipa uhakika wa tendo la ndoa bila pesa?