Mara ya mwisho....

Nilikuwa namsifia jamaa yangu akaniambia eti nataka kumwibia.
Kila nikimpa sifa ananiambia mwanamke mwizi utamjua tu.
Nikaacha kuwasifia hawa wanaume wetu wa kiafrica hasa wa TZ hawaelewi ukimsifia
 
Kwanza,wenza si vyema kuwa wanaoneshana maungo yao mara kwa mara,kwani inaweza kusababisha kukinai!Pili kwa mtu mwenye kuijua thamani ya mke/mume hawezi kumsifia kwa umbo/rangi au mambo ya kuonekana kwani mambo hayo ni ya mwilini na kama umekua na huyo ulienae kwa misingi hiyo matatizo yako jirani,usisubiri mpaka ujengewe kujiamini na mtu mwingine nje yako,jiamini mwenyewe!Kama unashindwa kujiamini mbele ya mke/mume wako,hufai kuwa na wadhifa huo!
Eiyer kumbuka mume husisimka kwa kuona...afu love=distance+adventure...adventure (mume) inatengenezwa na jinsi anvyoyaona maumbile yako hata aende wapi atakumbukia tu(nyerere's song niwapo safari nakumbuka mambo mema ya kwetu(mama maria!!)...sifa ni kitu kinachomjenga mke hebu siku mme akukandie kadamnasini itakuwa mbaya....nahitimisha mwanamke aliyependwa(sifiwa) ndiye bora zaidi
 
MORIA,mke/mume ni wako tu,hutakiwi kuwa mtupu kwake kila mara,hizo sababu ulizozitaja zinahitajika kwa wale ambao ni fake,hawajui kupenda maana yake nini!Na hawa ni wengi sana nowdays that's why divorce kila kukicha!Jiamini mwenzi wako atakukubali tu!
 
Mjengee mwenzako kujiamini kwa kumsifia na kumjulisha kwamba unapenda alivyo...hata kama ni kibonge sana...kimbaumbau...ana makovu...ana kitambi au ana ukilema wa aina yoyote ile.Mfanye ajisikie vizuri awapo na wewe...mfanyie ajisikie huru bila aibu/woga mbele yako...mfanye ajisikie amani na pia furaha.Mwonyeshe mtazamo chanya juu ya muonekano wake ili ajiamini. Na kama kuna kitu ambacho unadhani kinahitaji kurekebishwa (achana na kuongeza viungo kwa madawa ya mchina) kama kupunguza mwili mshawishi vizuri kwa upendo afanye hivyo ili na wewe uweze kutidhika nae pia kumfurahia.

leo hauko sarcastic...............kama siku ile..............................maazo mazuri haya...................ingawaje yaweza pia kujenga tabia ya kinafiki ya kusifia mambo ambayo yanakinzana kabisa na vionjo vya moyo wako....................
 
MORIA,mke/mume ni wako tu,hutakiwi kuwa mtupu kwake kila mara,hizo sababu ulizozitaja zinahitajika kwa wale ambao ni fake,hawajui kupenda maana yake nini!Na hawa ni wengi sana nowdays that's why divorce kila kukicha!Jiamini mwenzi wako atakukubali tu!
Sijasema kila saa ila ni muhimu kwa mke alijue hili sisi husisimka kwa kuona... na hakuna ufake ktk kufanya hili...ndiyo silaha yako! hata baba yetu isaka alionekana akicheza na mkewe kihasara hasara enzi hizoo..mbona mnawazuia beki3 wasiwe naked? au jaribu kuaga mume unaenda kwa soko ukiwa umevaa vibaya vibaya....divorce ni masuala yenye mlolongo mreeefu unaoanzia mbaali..
 
Kwa kweli mara nyingi sana siwezi kuhesabu ni mara ngapi namsifia na najisikia vizuri kufanya hivyo kwani na yeye ananisifia mara nyingi hivyo ni desturi yetu kusifiana. Ila tuongeze na pole kwa kazi, samahani na ahsante ni vitu muhimu saana kwenye ndoa zetu. Ahsante sana Lizzy kutukumbusha jambo hili muhimu kwa wapendanao!
 
Nilikuwa namsifia jamaa yangu akaniambia eti nataka kumwibia.
Kila nikimpa sifa ananiambia mwanamke mwizi utamjua tu.
Nikaacha kuwasifia hawa wanaume wetu wa kiafrica hasa wa TZ hawaelewi ukimsifia
Aisee, pole sana, yaani huyu inaonekana yuko addicted na kitu fulani, pole lakini usikate tamaa endelea kumsifia unapoona kweli amefanya vizuri, pia jaribu kufuatilia historia yake huenda kuna kitu in the past kilichomuathiri kisaikolojia
 
MORIA,mimi siku nikija oa nakuhakikishia kuwa mwili wa huyo mke wangu hautakuwa kigezo cha mimi kuwa nae,kuwa naked kwa hg sio sawa kwani anatakiwa ajisitiri,pia hata kama akitoa nguo zote bado mwenye maamuzi ya kuchukua hatua yoyote ni mimi!Utupu wake hauwezi kuwa kigezo!
 
msifia mkeo/mwenza kwa kuwa msafi na kuwajibika inatosha kabisa kumfanya ajisikie kuthaminiwa. Kwa mfano ww mkeo akuambie ''magu, u ar a good and responsible man. asante kwa kututunza mimi na watoto. na kwa kutupenda na kutujali'', hata kama ww sio handsome bado utajiskia ka-handsome flani,lol!


My dear umeongea yoote, ubarikiwe sana.
 
Mara ya mwisho kumsifia mke/mume/mpenzi wako ilikua lini?!

Kumsifia mwenzi wako haswa mkiwa faragha kuhusu mwili wake/sura/umbo/sauti n.k kunaongeza kujiamini kwake.Fikiria mwanamke ambae hata wakati wa kuvaa nguo anajifunika na taulo au anafunga kabisa mlango na komeo wakati wapo wawili tu ndani ya nyumba hata kukiwa na tatizo kwenye sekta ya mapenzi ataanzia wapi kumweleza mwenzake na kumwaga hisia zake?! Mwanaume ambae nae anavua na kuvalia humo humo bafuni ili mwenzie asimuone anawezaje kueleza mapungufu yao iwapo yatajitokeza kwenye sekta ya mapenzi?!

Mjengee mwenzako kujiamini kwa kumsifia na kumjulisha kwamba unapenda alivyo...hata kama ni kibonge sana...kimbaumbau...ana makovu...ana kitambi au ana ukilema wa aina yoyote ile.Mfanye ajisikie vizuri awapo na wewe...mfanyie ajisikie huru bila aibu/woga mbele yako...mfanye ajisikie amani na pia furaha.Mwonyeshe mtazamo chanya juu ya muonekano wake ili ajiamini. Na kama kuna kitu ambacho unadhani kinahitaji kurekebishwa (achana na kuongeza viungo kwa madawa ya mchina) kama kupunguza mwili mshawishi vizuri kwa upendo afanye hivyo ili na wewe uweze kutidhika nae pia kumfurahia.

...nice one Lizzy, ...mkiwa faragha, ukiwa kazini, safarini, nk...msifie kila unapomkumbuka.
 
ukikasoma haka katoto (Lizzy) utagundua kenyewe kako demanding na kanapenda 'kufanyiwa' na sio kufanya...it is complicated and very strange how one can be such demanding ... pole kwa bhana 'ake!!
Woww....asante kwa kunielewa.Kama mhusika angekaua ananielewa kama ulivyonielewa wewe ningekua na furaha sana.
 
Naogopaga mke wangu kuona Biology yangu...Liizy leo tu nimemwambia bibie...wewe mzuri katoa sauti ya kile kicheko cha taarabu...nikanyamaza kimya....sitajaribu tena kusifia...
Sasa sindo kafurahi....ama?!
 
mmmmmmh, duh...................najuta kusifia,maana nilikuwa namsifia akajihisi malaika na mimi ni kibwengo tu....akanikimbia!Lakini zoezi nimelianza jana kwa kukusifia kwa michango yako, sasa kwenye umbo,sura,muonekano............mpaka nikuone au kama unafanana na avatar yako................niambie nianze kushusha misifa.
MyK watu wanaolewa sifa wapo...na kama asingelewa kwako angelewa mtaani akaona we huoni uzuri wake acha aende kwa wanauona.Kwahiyo kwa vyovyote vile hamna ulichokosea.Kuhusu mimi we nisifie tu bwana hata kama urefu wangu ni nusu wa unaouona kwenye avatar...au umbo ni mara mbili wa unaloliona.
 
Nilikuwa namsifia jamaa yangu akaniambia eti nataka kumwibia.Kila nikimpa sifa ananiambia mwanamke mwizi utamjua tu.Nikaacha kuwasifia hawa wanaume wetu wa kiafrica hasa wa TZ hawaelewi ukimsifia
Hahahaha....atakua alikua haamini sifa unazompa.Kuna watu hua hawajioni kama wanavyoonekana kwa wengine....hata akiwa na akili sana ye anajiona wa kawaida.
 
Back
Top Bottom