Mapya yaibuka: Maafisa wa TMAA walipewa hela ili Smelter isijengewe Tanzania

Maneno mengi utekelezaji sifuri!!!

Kama hao TMAA na ACACIA ni waongo si serikali ijenge basi hizo smelters!!! Serikali ikijenga, tunawatoza gharama ndogo hao ACACIA wanaosema not economical kwa wao kujenga smelters.

Nadhani gharama zetu zitakuwa very affordable kwa sababu tunaamini ujenzi wa hizo smelters not expensive kama akina TMAA wanavyosema!!

Ile ripoti ya TMAA mie nimeisoma mara nyingi sana!! Wengi wenu humu mnaangalia wanasiasa wamesema nini!!!

Mosi, TMAA hawakusema smelters zisijengwe bali bali walisema not commercially viable. Hata hivyo, wakapendekeza nini cha kufanyika to make the whole thing viable.

Moja ya mambo waliyokuwa wameyataja ni kiasi cha mchanga kinachozalishwa na nishati ya ku-run hiyo mitambo!!!!

Kwa upande wa Barrick, wao walisema "not economical TO US" kujenga smelters!!

From economic point of view, mtu anaposema not economical haimaanishi kwamba kujenga ni hasara!

However, kwavile wamesema "not economical to us (acacia)" manake kuna better option kwao kuliko kujenga smelters. Hiyo ndiyo tafsiri ya not economical!

Lakini ambacho "not economical" kwa Barick/Acacia/investor kinaweza kuwa very economical kwa serikali. This so because, wakati ACACIA wanaangalia economic benefits serikali inatakiwa kuangalia socio-economic benefit!!

Mbona simple tu!!!!

Rais kama aliweza kununua ndege 3 kwa mpigo anaweza pia kuwapa pesa Stamico wajenge smelter na wenye migodi hata wa nchi jirani watautumia. Hapa kazi tu.
 
hivi kwa nini south africa,ghana na mali wanaoongoza kwa dhahabu hawana hizo smelter according to size wanayoitaka?

Unabishana na watu wasiolewa hasara Taifa linaenda kupata kwa kufanya biashara ya kujenga smelter.

Serikali itatumia kodi za wananchi kujenga kitu ambacho hakitaleta faida wala manufaa. Ni jambo la kusikitisha sana kiasi unatamani kulia kwa ujinga na ushabiki huu.

Wengi wape lakini ukiwauliza hiyo smelter itakuwa ni ya copper, zinc, silver au? Hawatakupa jibu. Wao wanataka smelter.

Ukiwauliza kama kuna uzalishaji wa kutosha kuwa na smelter, pia hawana jibu. Ushabiki wa kijinga.

Ukiwauliza smelter hiyo itaendeshwa kwa gharama nafuu na ubora kushinda washindani wake (Japan, Germany etc) hutajibiwa. Lakini wao wanataka smelter.

Maana isijekuwa ni bei rahisi na bora kupeleka "mchanga" Japan kuliko hapa kwa sababu gharama kubwa kuzidi mali husika.

Hao wanaosema smelter ijengwe sijui kama wamejiuliza kushuka kwa commodity prices kutaathiri vipi biashara hiyo.

Sidhani kama wamejiuliza evolution ya technology kwamba kesho Graphite inaweza kuwa mali kushinda copper.

Environmental assessment imefanyika na gharama zake zinajulikana?

Leo hii wasomi wanaotoa maoni tofauti wanaitwa wamehongwa, vibaraka, hawana uzalendo na majina mengine.

Muda utaongea. Ngoja uchumi ufe kwa uwekezaji wa miradi mfu.
 
CCM bwana anatafuta sympathy? Hampati ng'oooo wote ni majizi tu
Tena mwizi mwenyewe walikaa meza moja na kukubaliana namna ya kutuibia kwa njia ya makaratasi leo hii wanajifanya as if ndio wameingia madarakani 2015 nawaza tu hawa viongozi hasa wanaotokana na ccm wakapimwe vichwa
 
Nimeosoma huu uzi nimeamini bado ujinga upo wa kutosha. ..

Nani kawambia mabepari wanafurahi tukipiga maendeleo ya kiuchumi. ...makighafi tunazo tukipata technology unajua nini kitatokea...yutaweza kuinuka na kuondoa utegemezi. ...kama chinani

NDIO sababu wanatujaza ujinga siku zote tusiweze kusimama. ..KWA mtu anayeona mbali kujenga smelter ni jambo strategic.
Ndo maana Wazungu wameziacha nchi za Kiafrika katika umaskini. Mpaka wakati kiongozi kama huyu anaingia madarakani kiwewe kinawaingia. Wangependa sana tuwe tegemezi.nKilicho na mwamzo kina MWISHO.
 
Hili seke seke la mchanga ukijumlisha na kauli tata za mkulu zinafanya Tanzania ionekane sio business friendly kwa investors. Hata wawekezaji wapya watasita kuja kwa kuhofia serikali kutokua na utawala wa sheria. Mifano mengine ni ishu ya dangote na makaa ya mawe, gesi, rais alipoamuru tank la maji lijengwe kwenye mlima ambao investor alikua wanafanya utafiti wa madini huko kanda ya ziwa na leseni yao ifutwe.

Mambo mengine serikali inatakiwe ifanye kimya ili tusipate negative publicity.
 
Ukiandika hapa jukwaani ili upate point za JF na like kibao unajiumiza mwenyewe.Andika hapa JF kwa manufaa yako na wanaokuzunguka bila kuathiri matakwa ya vizazi vyote cha sasa na vijavyo. Utaheshimika sana
Ninakuunga mkono. Zaidi ya hapo, kwa analytical fingings za akina Prof. Muruma kuhusiana na kiasi cha dhahabu na madini mengine yaliyomo kwenye mchanga huo, ni wazi kuwa lazima itakuwa na faida kubwa tu. Na si lazima tununue hiyo smelter kwa cash. Tunaweza kuilipia kwa installment kidogokidogo kutoka kwa faida tutakayokuwa tunapata.
Hilo linawezekana sana.Maana penye nia pana njia
 
wote hao ni ccm msituzengue kujifanya st's wakati kila mtu anaiba upande wake nani msafi ccm
 
Tuwapige mabomba wote waliohusika na huu upuuzi na wizi wa madini yetu ndiyo itakuwa fundisho kwa Wajinga wengine.

Tukikaa kulialia bila kuwachukulia hatua kali kama kuwapiga bomba ama kitanzi Tanzania hatutasonga mbele daima.

Mahakama ya mafisadi ingeanza nao kisha bomba wapigwe pale Taifa live.
 
Will it now be economically viable kujenga smelters zetu sasa hivi? Tusichukue maamuzi ya hasira kujenga. Tusije kujenga smelters madini yakaisha in the next decade tukaishia kusindikia mihogo ya Maneromango.
Issue hapa haikuwa kujenga Smelter pekee bali ni process ya KUZUIA maendeleo.Kama ingekuwa tayari IMEJENGWA Tanzania tungekuwa mbali sana. Miaka IMEENDA WALIOKULA WAMETULA.
Na kama usemavyo upungufu hauko mbali. HATA HIVYO tuna HAKI ya KUDAI FIDIA kutoka pande zote TMAA officials waliojijengea MAGOROFA pia kutoka kwa Makampuni husika ya Madini.
 
Issue hapa haikuwa kujenga Smelter pekee bali ni process ya KUZUIA maendeleo.Kama ingekuwa tayari IMEJENGWA Tanzania tungekuwa mbali sana. Miaka IMEENDA WALIOKULA WAMETULA.
Na kama usemavyo upungufu hauko mbali. HATA HIVYO tuna HAKI ya KUDAI FIDIA kutoka pande zote TMAA officials waliojijengea MAGOROFA pia kutoka kwa Makampuni husika ya Madini.


Officials wote wa TMAA tuwapige bomba (ile kitu watu wanaogopa sana kwa kudanganya serikali na nchi na. Kutuibia madini yetu )
 
Tatizo letu mdomo tuachie tume complaining za nini?kama kuibiwa meibiwa Leo? pungezeni mihemuko tumieni busara kelele hizi hazisaidii
 
Mambo mengine yanachekesha sana, tatizo letu sisi Waswahili nikurudia rudia lame excuses zinazotolewa na ma investors - Waswahili wanabadirisha maneno fulani hapa na pale, lakini ukiangalia kwa umakini mapendekezo ya wawekezaji na ya mapendekezo ya waswahili ni selfsame - actually Waswahili wana elekezwa na wawekezaji nini cha kuandika - ndiyo ujinga tulio nao - wanapewa handout zilizo tayarishwa in advance na wawekezaji,waswahili wanabadirisha kidogo maneno machache halafu wanawalisha mapendekezo hayo ya kuzunga Serikalini kama ni ya kwao vile - wakati wakijua wazi kwamba hiyo si kweli.

ACACIA wanasema "not economical" kwa wao kujenga smelters!! Sasa kama hicho si kichekesho tukiite nini? Kama wangesema tangu waje nchini kwamba machimbo ni ya muda mfupi 5 years say baada ya hapo migodi itakuwa exhausted hapo tungewaelewa, lakini wanyonyaji hawa wamechimba mchanga kwa karibu miaka ishirini na bado wanaendelea kuchimba from now to eternity halafu waswahili tunakubali visingizio vyao vya kijinga eti wao kununua na kujenga Smelters nchini hailipi - ukiwahoji kwa miaka karibu ishirini wamevuna fedha kiasi gani mpaka wanashindwe kujenga kinu cha uyeyushaji madini nchini, ukiwahoji hivyo sijui kama utapata jibu lenye mshiko - walisha tuona ni mazezeta.

Sasa check comments/mapendekezo ya waswahili (TMAA) wanarudia yale yale ya wawekezaji eti hawapingi Smelters kujengwa nchini hisipokuwa they're not commercially viable - wanabadirisha maneno lakini meaning inabaki ile ile i.e maneno yanajirudia yale yale i.e "old wine in a new bottle." Watu/wahujumu hawa kama wangekuwa kwenye Taifa kama China wangeishia kwenye gallows/summary excution.

TMAA sijui kama waliwahi chukuwa trouble ya kutembelea Taifa la Zambia kwenye Copper Belt kuangalia vinu vinavyo tumika kuyeyushia Gold, Copper, Cobalt, Titunium nk, vinu hivyo vilikuwepo tangu enzi za Rais Kahunda ingawa miaka ya hivi karibuni migodi imenunuliwa na Wachina lakini Wachina hawaku uproot mashine na vinu vya kuyeyushia madini kwa kisingizio kwamba haviko economical kuviendesha hivyo mchanga usafirishwe kwenye ma container kwenda Uchina kuyeyushwa - Wachina hawakufanya/leta visingizio vya kijinga kama hivyo - maajabu hayo yapo hapa kwetu Tanzania tu.

Sasa swali: Wazambia walifanikiwaje wakati sisi huku tunakwama kwa kutoa visingizio mbali mbali, TMAA wanakimbilia kutembelea vinu vya Japan vinavyo tumiwa na wawekezaji kufanya udanganyifu - wanafikiri wengepata majibu gani in our favour zaidi ya ku-reinforce excuses za kuendeleza udanganyifu wao eti Smelters are bloody expensive kuzinunua regardless za capacity ya uyeyushaji!!

Mbona Wachina wameleta nchini Smelters za kuyeyushia madini ya kumiminia tires kwani zina tofauti gani kiufundi si kiasi cha adjust temperature kukidhi melting points za madini husika - process hiyo haina tofauti na fractional distillation za crude oil nk vimimika vinajichuja kutegemea na boiling points zake wakati madini yanajichuja kutegemea na melting points zake - watu wote walio soma kemia/chemical,processing Engineering wanajua vizuri ukweli huo.
Well said. Mwenye masikio na asikie.Tatizo wengi niwajuaji wasio na ufahamu kichwani. Inasikitisha sana. I believe together we can
 
Mwandika habari hii kama si kwa vile ni lumumba angekuwa ni wa Ufipa saa hii kale ka jengo kangesha tiwa hatiani na search warrant mkononi kufukua maficho.
Ati walihongwa. Jamani, acheni majungu. Walihongwa ngapi, Na nani,na wapi?? Wekeni na akiiba
Jambo hili halihusiki na mambo ya kisiasa bali ni MAISHA yako jamaa zako na Watazania kwa ujumla.Acha mawazo ya uchama katika mambo ya kimsingi kitaifa.
 
TMAA ndio walisaini mikataba ya madini? Issue ya smelter ilitakiwa iwe part and parcrl ya mkataba onset! Ok, later TMAA walikuja kusema "not viable"; sasa wewe prove them wrong kabla ya kuwahukumu.

Else, wangeshauri smelter ijengwe na ika-underperform kwa sababu yoyote ile (umeme wa kupiana, uhaba wa mchanga, n.k.) leo pia mgewahukumu. Mambo gani hayo? Acheni siasa kwenye mambo ya msingi hususan kuanzia huko kwa watunga sera.
Hili suala wengi wanalikurupukia na mihemko kibao mkuu. Umesema vyema.
 
Hili seke seke la mchanga ukijumlisha na kauli tata za mkulu zinafanya Tanzania ionekane sio business friendly kwa investors. Hata wawekezaji wapya watasita kuja kwa kuhofia serikali kutokua na utawala wa sheria. Mifano mengine ni ishu ya dangote na makaa ya mawe, gesi, rais alipoamuru tank la maji lijengwe kwenye mlima ambao investor alikua wanafanya utafiti wa madini huko kanda ya ziwa na leseni yao ifutwe.

Mambo mengine serikali inatakiwe ifanye kimya ili tusipate negative publicity.

Strange!! I am not following you here - especially your last sentence, may you please clarify?
 
Back
Top Bottom