Mapokezi kiduchu ya Lissu! Dalili nyingine ya anguko la CHADEMA nchini Tanzania

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Huu ndio ukweli, tena Dar es Salaam! Mahudhurio hayakulingana na nguvu kubwa iliyotumika. Chama kilianza kampeni na uhamasishaji kwa takriban mwezi mmoja uliopita ukizingatia kwamba, Dar es Salaam ndio kitovu cha nchi ya Tanzania, kwamba CHADEMA yote nchini, ilihamia hapo!

Wabunge wake wote (walioangukia pua 2020), madiwani wa mikoa yote ya jirani na Dar es Salaam (walioangukia Pua-2020) wote walihudhuria. Kwa tathmini ya haraka haraka, wananchi wa Dar es Salaam hawakuitikia wito wa Chadema. Wameshindwa kuujaza uwanja mdogo wa Mwembeyanga!

Msigwa na kamati yake ya maandalizi wamekuwa hawalali usiku na mchana ili kuhamasisha watu kujitokeza kumpokea Lissu na hatimae kwenda pale Mwembeyanga kwenye mkutano wa hadhara. Mapokeo hayalingani na uzito wa tukio pamoja na nguvu kubwa iliyo tumika.

Lissu ameendelea yale yale, kulaumu bila kutoa way forward! Ameshindwa kuitumia nafasi hiyo nyeti kuongea machache ila yenye uzito wa kumjengea ushawishi kwa mikitano iitakayofuatia.

Kweli katiba mpya inatoa suluhisho la baadhi ya mambo ambayo yanafanyika kwa sasa lakini katiba mpya haileti punguzo la bei za vyakula nchini. Hili suala la bei za vyakula ni suala la wachumi bobezi, kuachiwa walete sera mpya na zenye kuendana na wakati uliopo.

Ongezeko la bei la vyakula linasababishwa na sera mbovu za kufungua mipaka na kuwaachia walanguzi wa nchi jirani wakiingia mpaka mashambani kwa wakulima wetu na hatimae kulangua vyakula pengine hata vikiwa bado kuvunwa.

Pia kuhusu wanyama kule saudi Arabia Zoo, ile zoo haina hata wa kutisha ki-vile. Alichotakiwa kuhoji Lissu ni uwepo wa ndege zinazotorosha wanyama wetu, lakini nimemshangaa kwa kukwepa kuliongelea hilo. Huenda ndio atatumia kwenye jukwaa lingine.

Ninajua maovu ya CCM lakini pia kuna mengi sana ya kuipongeza, huwezi amza hotuba mwanzo mwisho ni lawama na ubaya tuuu halafu huongei njia za utatuzi wa hayo unayolaumu, bali unakimbilia kuibebesha zigo katiba mpya.

Katiba ni takwa la wanasiasa, sababu wao wanasaka kuingia Ikulu. Wananchi takwa letu ni sera nzuri za kiuchumi, pamoja na huduma bora za kijamii.

Tuendelee kukosoana kwa hoja na sera, ila kwa wale tunaowajua sera zenu za matusi sintawashangaa mkiendelea. Maana hata Lissu aliteleza, bahati nzuri akapewa ki-memo ndio akapotezea kwa kusema hizo ni Amsha-Amsha!

Alamsikhi.
10101.
View attachment 2495592
 
Uliposema tu kwamba wabunge wote wa chadema waliangukia pua nilikuzalau.
Hivi kwa akili yako hiyo unaamini huo ulikuwa uchafuzi?
 
IMG_20230125_190754.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom