Mapishi ya maini fasta

long'oi

Senior Member
Jul 16, 2011
119
69
Wachache sana wanajua namna ya kupika maini yaive vizuri, yawe matamu ndani ya muda mfupi. Fuata recipe hii then utaenjoy

Mahitaji:
1. Maini 1/2kg
2. Kitunguu kikubwa sana kimoja
3. Karoti kubwa moja
4. Hoho (Yellow, Green na Red) kila moja ikate nusu yake
5. Nyanya tatu zilizoia vizuri, ziwe za ukubwa wa kutosha kutengeneza rost zito
6. Pilipili kama unapenda
7. Kotimiri
8. Limao kubwa lene rangi ya njani lenye Juice ya kutosha
9. Soya Sauce
10. Chumvi
11. Mafuta ya kupikia unayopenda (mazuri yale yatokanayo na mbegu za mimea)

Jinsi ya Kuandaa:
1. Menya maini yako, ondoa kabisa ngozi ya nje iliyopo kwenye maini kwa kuwa hufanya maini kutokuiva na kuwa magumu kisha yaoshe vizuri
2. Baada ya kuyyaosha yaweke kwenye chombo kisafi, kata limao lako kamulia juice yote kwenye maini yako, ongeza soya sauce kiasi, na chumvi kiasi. Chukua ganda la limau ulilokamua kwa kukwaruza kwangulia kiasi ganda la nje na kisha changaya maini yako. Yaache.
3. Katakata nyanya, kitunguu, karoti hoho, kotmiri na pilipili viwe tayari.
4. Chukua sufuri yako weka kwenya jiko tiamo mafuta kiasi, yakipata moto weka vitu vyote ulivyovianda kwa pamoja ndani ya hiyo sufuria. koroga kuvichananya. Viache viive kwa pamoja kati ya dk 5~7. Ipua ni tayari kuliwa.

Unaweza kula na
Ugali
Wali
Chipsi
Chapati, nk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom