Unajuwa siku zote adui yako muombee njaa. Lakin vile vile dua la kuku haliwezi kumpata mwewe.
Mimi nimeishi sana Tanganyika na kubahatika kusomea huko kuanzia skuli darasa la sita Mchikichini, Tambaza Boys sec, Ilboru boys Sec na UDSM na nikapita JKT ruvu na kumalizia Mgulani. Hivyo nimeona mngi sana ya kasumba kwutoka kwa wabara dhidi ya waZnz.
Nakumbuka hata darasani walikuwa na dharau sana lakin kichwani wengi walikuwa hamna kitu. Wao na kwa jinsi ya mafunzo walopewa huko sunday school ni kuona kila Mznz ni goi goi na hawezi kuwa na akili darasani na hawezi uongozi. Kitu hicho kwa watu wa Bara ni chuki walizopandikiziwa na makovu ya UKOLONI wa mwingireza mbao ulitukuza sana dini yao na kujenga skuli nyingi za madh'hebu yao ukilinganisha na zile za waislam. sasa wamezoea kuona wao ni wasomi na wana uwezo wa kila kitu kuliko wengine.
Kumbuka kwa hilo ndilo liliweza kupelekea hata muasisi wa Chadema na waziri wa fedha mstahafu Mzee Mtei kuona kwanini kuna waislam wengi katika Tume ya kukusanya maoni ya kuundwa kwa katiba mpya. Kwani wanaamini waZnz hawawezi chochote.
Sasa ndio jua linawachwe na kuleta ghilba na fitna kama hizo.
Kwa mwenye akili timamu nafikiri atajiulize.
1. Iweje jiichi lenye watu zaidi ya milioni 12 lilazimishe kuungana na nchi yenye watu chini ya laki moja na nusu. tena kwa uwiano ulio sawa kwa kila kura?
2. Tena baya zaidi jiinchi hilo likubwa likubali kupoteza utaifa wake na jina lake na kukumbatia jina la muungano.
3. Cha aibu zaidi jiichi hilo kukubali lisiwe na serikali yake na kukumbatia ile ya muungano wakti kiichi kidogo kinakuwa na Serikali yake.
Kwa mwenye akili atagundua kuna jambo hapo limefichwa ambalo mpaka leo wenzenu wa upande wa pili hawalioni wala kuligundua si kwa sababu JKN ni saint bali ni uzuzu wa mawazo na kutegemea kutafuniwa kila kitu.
Kwani mtu mzima unaweza kumtishia nyau?
Barubaru (na wengine wote wenye mawazo kama yako kwenye RED);
Hebu niambieni, kama Watanganyika wanalazimisha muungano Wanzazibari wanalazimika kukubaliana na huko kulazimishwa muungano wasioutaka? Kama ulivyosema, kwenye muungano Zanzibar ime-retain identity yake, ina baraza lake la kutunga sheria na ina rais wake, sasa kinachowashinda kujitoa kwenye muungano ni kipi?? Au mnataka Watanganyika waseme "Muungano basi!" ndio nanyi "muamue kujitoa"? Kuna Mtanganyika aliewazuia kuitisha kura ya maoni? Mbona mliunda serikali ya muungano wa kitaifa, Mtanganyika gani aliewazuia kwa hilo?
Barubaru, ulishaingia darasa lolote la Sunday School? Kam jibu ndio, ni la dhehebu gani na wapi? Kama jibu sio, umejuaje kuwa Sunday School kunafundishwa mambo ya Uzanzibari na Utanganyika (achilia mbali mambo ya kiasiasa)?