FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,886
- 109,218
Tukiitazama historia ya Dubai au UAE kwa ujumla, Oman, mwambao wote wa Zanzibar na bandari takriban zote za nchi za mashariki ya kati mpaka India na Asia ya mbali,utakuta kulijuwa na mwingiliano mkubwa wa kibiashara kati yao.
Bila shaka ni historia ndefu sana na ya zamani sana, kwa ufupi, leo tutazame mafanikio na neema kubwa iliyowadondokea Dubai na yalipotokea mapinduzi ya Zanzibar 1964.
Wimbi la awali la wakimbizi wa Zanzibar walianza kumiminika Dubai kati ya mwaka 1964 na 1968, Wazanzibari wengine, kwa mujibu wa data za UNHCR qazanzibari waliendelea kwenda kama wakimbizi baina ya mwaka 1967 mpaka 2013.
Katika miaka hiyo wengi wa watu kutoka Afrika Mashariki nzima wakaanza kumiminika kama wakimbizi Wazanzibari. Sheikh Rashid akaunda kamati ya Wazanzibari, katika wale waliofika mwanzo, waamuwe katika "wakimbizi" wanaokuja Dubai ni wepi Wazanzibari wa kweli wanaostahiki ukimbizi wa Zanzibari. AlhamduliLlah kwa kuwa kulikuwa na mwingiliano mkubwa wa watu wa Afrika mashariki wengi wanzangu na mie wasio na asili ya Zanzibari wskajipatia "status ya ukimbizi". Fsmilis. Nyingu za Dar. Tunafahamiana nao ambao wsliibgianjwente mkumbi huo na siku hizi wameshakuwa raia wa UAE kiuhalali kabisa. (kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.
Kwanini ikawa ni ushindi na neema kwa Dubai? Historia ya Zanzibar inaonesha wazi kuwa Zanzibar wakati wa mapinduzi ilikuwa ni nchi iliyoendelea sana kielimu na kiuchumi kuliko nchi nyingi duniani.
Sheikh Rashid bin Saeed Al Maktoum, ambae ni babu wa Mfalme wa sasa wa Dubai, aliposhauriwa na mshauri wake wa Kiingereza (Duff) kuhusu wakimbizi wa Zanzibar, hakusita kuwakaribisha na kuwapokea kwa nia njema kabisa.
Kwa bahati nzuri kabisa, wakimbizi wengi wa Zanzibar wa wakati huo walikuwa ni wasomi na wataalam wa biashara na siasa za kidunia.
Wasomi na wataalam hao ikawa ni neema kubwa kwa Ufalme wa Dubai. Ufalme wa Dubai ukajipatia washauri, wafanyakazi na wataalaam mbali mbali wenye utamaduni unaofanana kabisa na wao.
Wazanzibari hao hawakuliangusha jina la Zanzibar, walifanya kazi na biashara zao na. walishauri serikali ya Dubai kwa uaminifu kabisa.
Mapinduzi ya Zanzibar kisiasa yalizaa pia mapinduzi ya kiuchumi Dubai, yenye neema kubwa sana kwa Dubai. "Kufa kufaana".
Itaendelea kidogo kidogo kwa mtindo wa maswali na majibu.
Yeyote anaweza kuongezea nyama kwenye upungufu. Yeyote anaweza kuuliza yanayohusiana na hii mada.