abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
Duru zinaarifu kuwa Mfalme wa Saudia alijaribu kuishawishi Marekani iendelee kuunga mkono kubakia madarakani Mubarak pamoja na kuwa Wamisri waliowengi walikuwa wameshaanza mapinduzi ya kumtimua Mubarak aliyetawala Misri kwa miaka 30.
Gazeti la World Tribune la Marekani limenukulu duru za kijasusi nchini humo zikisema kuwa harakati hizo za kuzuia ushindi wa mapinduzi ya Misri zimepelekea hali ya mfalme Abdullah kuzorota zaidi.
Mtawala huyo wa Saudia alifanyiwa oparesheni Novemba 24 na Desemba 3 mwaka jana nchini Marekani na sasa anaripotiwa kuwa mapumzikoni nchini Morocco. Alhamisi iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Saud al Faisal alikanusha uvumi kuwa Mfalme Abdullah alikuwa ameaga dunia. Alisema hali yake kiafya ni nzuri na ana hamu ya kurejea nyumbani kuendelea na kazi zake.