Mapenzi yanamtatiza: Tumsaidie huyu Binti.............

Hv huu ugonjwa wa wanawake kutokusahau waliowatenda unanikera thana,ninaweza mshaur zaid na ufumbuz kwan uzowefu n nao.kwa uchache n hv,kwanza afute mawasiliano hta km kakalili namb ya yule jamaa,2.ajaribu kuwa busy na mpenz wake mpya,atasahau.Mengneyo wasiliana nami nkupe.
Senator p nikikwama kumsaidia kutokana na ushauri nilioupata hapa nitaku-pm uongee naye kwa simu lakini under my supervision Lol!!!
 
Last edited by a moderator:
Taratibu atamsahau huyo wa zamani na kumpenda huyu mpya, haiwezi kutokea right away! Inaweza kuchukua muda kidogo, cha msingi zaidi atulize akili.
 
2pa kule hajui thaman ya penz lake sa ye wanin tena,tena asithubu2 kumrudia kwan hajua km malaya hana likzo? Labda km yupo radh kushea io mal,na man akshajua dem mdhaif kiivo ndo atakua anajfanya kbolo-dinda akjua kua atasamehewa 2 lazma.kumsahau atamsahau 2 hakuna lenye mwanzo lkakosa mwsho mbn kabla ya kua nae alkua poa 2,tena naongeza iv mwambie akshkwa ashkamane
yaliyomo yamo Good ushauri mzuri. Natumai huyu mdogo wetu atakarabatika nisingependa apotee...Kweli yaliyomo yamo!!
 
Last edited by a moderator:
Taratibu atamsahau huyo wa zamani na kumpenda huyu mpya, haiwezi kutokea right away! Inaweza kuchukua muda kidogo, cha msingi zaidi atulize akili.

Kwa hiyo webondo...........hebu fafanua kama jamaa anampigia pigia simu haiwezi kuwa inamchanganya akili.....Kwa hilo afanyeje?
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo webondo...........hebu fafanua kama jamaa anampigia pigia simu haiwezi kuwa inamchanganya akili.....Kwa hilo afanyeje?
Alishaamua kuachana naye, aimamie katika uamuzi huo! Katika maisha ni muhimu sana kusimama imara sio tu katika masuala ya mapenzi. Amwarifu huyo mpenzi wake kuwa "akome kumpigia simu" kwani tayari ana mpenzi mwingine, lakini naye asiwe kigeugeu tena akishafanya hivyo.
 
Kumusahau mtu ni rahisi sana. Usijipe mda wa kufikiria mapenzi. Najua watanzania wengi mawazo yao mengi ni kuhusu mapenzi ndo maana anaona kazi kumuacha huyu mpenzi wake kiwembe. Tazama maisha yako kama mchaga na uwe na uelevu wa kufikiria kama njiwa. Tahadhari huyo aliyekupenda na wewe haumpendi utamuumiza sana akijua.
 
Well said webondo.....nimekumbuka wimbo wa marijani Rajabu:

Siwema usinipe mateso ya moyo
Na sasa nimechoka kweli nasemaa............

(chorus) nimezunguka tanzania bara aah unguja na pemba pia nimefikaa........................

Nitampatia wimbo huu lakini uliorudiwa na Lady Jay dee kwa sababu kizazi cha dot com hakimjui Marijani!!
 
Tena akijua anaweza kumuona kama malaya aliyekuwa anampotezea muda........mwisho wake majeraha mawili
 
Well said webondo.....nimekumbuka wimbo wa marijani Rajabu:

Siwema usinipe mateso ya moyo
Na sasa nimechoka kweli nasemaa............

(chorus) nimezunguka tanzania bara aah unguja na pemba pia nimefikaa........................

Nitampatia wimbo huu lakini uliorudiwa na Lady Jay dee kwa sababu kizazi cha dot com hakimjui Marijani!!
Haya poa poa! Au hata kamwimbie tu!
 
Ni binti mzuri kwa sura pia kichwani yuko vizuri........Ni rafiki yangu sasa yapata miezi saba. Tumekuwa tukipiga story mara kwa mara tunapokutana.

Kwa sababu ananiamini na kunichukulia kama kaka yake juzi amekuja kwangu na kunieleza tatizo lake ambalo hapo kabla hakuwa ameniambia...Ni kuhusu mahusiano yake.

Kwamba ana mpenzi wake anayempenda sana lakini miezi minne iliyopita alikuja kugundua kwamba anam-cheat, tena zaidi ya hayo akafikia kuzaa na huyo msichana.....Alivumilia na yakapita baada ya jamaa kumuomba msamaha. Mbaya zaidi baada ya kama mwezi alikuja kuona SMS ya mapenzi kutoka kwa msichana mwingine kwenye simu ya huyo jamaa.

Alifadhaika sana na kuamua kumuacha jamaa yake kwa hasira.....Na baada ya muda fulani akaja kumpata kijana mwingine ambaye ameonyesha kumpenda sana na anamjali...na inavyoonyesha mpenzi mpya anataka baadaye iwe ndoa kabisa.

Tatizo liko hapa: Anampenda sana jamaa yake wa kwanza...na yupo moyoni mwake hajafutika na kwamba anampigia simu kila wakati kumuomba msamaha warudiane. Kwake yeye anaona mtu wa future yake ni huyu mpezi mpya lakini anaona kama hayupo moyoni mwake na anashindwa namna gani amfute mawazoni jamaa wa awali ili ampende huyu mpya.

Sijamshauri mpaka sasa japo nimemuahidi kumpa ushauri wenye maana. Mimi "mbayuwayu" Naleta hapa JF nipate mchango wa mawazo ili nichanganye na zangu.

kaka wewe ni he mbona nahisi ka ndo mpenzi wake mpya af umemshtukia she wako bado anapenda alikotoka# thinking out loud
 
Sio kila wakati tunasimamia moyo....sometimes we have to let our loved ones go. they may love each other but they have nothing in common, hilo ndo tatizo. Atulie with time atamsahau.
 
kaka wewe ni he mbona nahisi ka ndo mpenzi wake mpya af umemshtukia she wako bado anapenda alikotoka# thinking out loud
cmoney Ingekuwa ni mimi ningesema, siogopi screen ya laptop au simu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom