Mapenzi ya kupenda na kupendwa

IGADESA

JF-Expert Member
Jan 15, 2021
295
721
Habari zenu wadau, nimejikuta nipo kwenye wimbi la mawazo nashindwa hata kuchagua niingie upande upi kati ya kupenda na kupendwa.
Kuna mabinti wawili wote wana umri kati ya miaka 24 -28, wote wanashepu matata, shida ni kwamba mmoja wao ananipenda sana yani karibu kila siku mara nyingi anapenda kunitumia meseji za salamu na mapenzi, huyo binti mwengine ni tofauti yaani nisipomtumia sms atapiga kavu hata wiki nzima ila nampenda sana maana inaniumiza yeye kupiga kimya ama kujibu sms kwa kifupi tu . Natamani huyu anaenishobokea awe huyo mwengine ninaemshobokea... Nipo njia panda nikubali tu niwe na anaenipenda ama nijipendekeze kwa ninaempenda?
 
Unayempenda hakupendi na anayekupenda humpendi,shida yako inaanzia hapa.

Ufundishe moyo wako kumpenda na kumpokea yule anayekupenda na umpotezee huyo asiyekupenda.

Kumbuka kumpenda mtu asiyekupenda Ni matumizi mabaya ya moyo na upotevu wa muda.
 
Huyo anaejipendekeza yukoje anatumaje sms

Nataka nijue ukute ni mimi niache kujipendekeza
Meseji za kujali tu..kuonyesha ananifikiria mfano kuniuliza ka nishakula...nimekionaje chakula nichokula uko nikokula nk..na mwishoe G9t sweet dreams😘 ... Meseji ka hizo ndo naita za kujipendekeza ambazo mie pia ndo natuma kwa mwengine ninaejipendekeza kwake mara nyingi.
 
Unayempenda hakupendi na anayekupenda humpendi,shida yako inaanzia hapa.

Ufundishe moyo wako kumpenda na kumpokea yule anayekupenda na umpotezee huyo asiyekupenda.

Kumbuka kumpenda mtu asiyekupenda Ni matumizi mabaya ya moyo na upotevu wa muda.
Shida ni kwamba Moyo unajiongoza wenyewe unapotaka...ukifosi mambo hata hisia zinaweza kugoma katikati ya mechi.
 
Meseji za kujali tu..kuonyesha ananifikiria mfano kuniuliza ka nishakula...nimekionaje chakula nichokula uko nikokula nk..na mwishoe G9t sweet dreams ... Meseji ka hizo ndo naita za kujipendekeza ambazo mie pia ndo natuma kwa mwengine ninaejipendekeza kwake mara nyingi.

yani mtu kukujulua hali ni kujipendekeza

Ina maana kila siku yeye ndio anaekutumia au na wew unamtumia

Sina uhakika kama anakupenda huwaga sisi hatupendii ukweli ukweli jichunguzee kama una ka hela ndio kinamendewa hapo
 
Karibu kila siku anatuma... Mi mpaka nijiskie kumsalimia maana naonaga noma kila siku anaanza yeye kunitumia.
 
Ila Kama anataka amiriki Nuclear Bomb ndani amsogeze anaemchuniaga wiki nzima..! Mwezi hatoboi ataleta Uzi humu usomekao "MPENZI WANGU HATAKI NIMGUSE" Atanishukru nimekaa hapa namalizia kuiba machungwa ya watu shambani
 
Meseji za kujali tu..kuonyesha ananifikiria mfano kuniuliza ka nishakula...nimekionaje chakula nichokula uko nikokula nk..na mwishoe G9t sweet dreams😘 ... Meseji ka hizo ndo naita za kujipendekeza ambazo mie pia ndo natuma kwa mwengine ninaejipendekeza kwake mara nyingi.
Ushakula?
Unakionaje chkula vs
Sawa nitajitaidi kuwa kauzu kwa wote.
Wote hawakufai
 
Back
Top Bottom