Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,443
- 4,153
Wakuu...
siku za karibuni nimeona rafiki zangu wawili wakivunja ndoa zao baada ya kutoswa na wake zao, hao wadada ni wa shoka, elimu A, na kazi walizopata ni za kimataifa
Cha kushangaza mmoja wao hakuwahi kuwa na issue na mkewe zaidi ya kuburuzwa kwenye maamuzi tangu mama amalize PhD yake; sasa nimesikia mama kapata kazi nje ya nchi, kaondoka bila kumuaga jamaa na amepeleka watoto wote boarding na jamaa hajui afuate njia ipi
Sasa najiuliza, hivi kuna uhusiano kati ya mafanikio ya mwanamke na kuvunjika kwa ndoa??? Nafahamu humu ndani kuna matawi yote na nategemea msaada maana mie nasomesha mke na nimeshaanza kuogopa
Please advice
Sidhani kama tatizo ni kusomesha mke; bali ni nini hasa kinachotembea kichwani mwake mnapojenga uhusiano wa mapenzi na hata kuoana. Nafikiri mke wa kukukimbia utamfahamu hata kabla hajaongezekewa na elimu au kipato.
Tatizo wengi wetu hupata wenza (mke/girlfriend) kwa kutumia kivutio cha ukwasi na/au wadhfa mkubwa hata kama ni illusion tu. Mke wa aina hiyo values zake zinakuwa finyu sana; atakuwa anakupima wewe na watu wengine kwa vitu hivyo hivyo tu. Akipata ufunuo mpya (elimu zaidi) na soko kubwa zaidi, basi wewe unakuwa na thamani ndogo sana kwake.
Na ikitokea uelewa wako (kielimu) ni mdogo zaidi na yeye sasa ndio yuko katika kiwango cha kuchangia mada na "maprofesa" na "vigogo" wengine, basi umeliwa.
Nafikiri somo kubwa kwa mwanaume ni kujiamini na kujijengea uwezo (kisaikolojia) wa kukabiliana na mabadiliko yoyote ya maisha. Ukikimbiwa na mke mwenye mtazamo finyu, thank God; it's GOOD RIDDANCE! Tena huenda huko mbele ya njia akajuta kurahisisha maisha na kujikuta akitafuta njia ya kurudi (baada ya kupata "elimu dunia").
By the way, mimi mwenyewe nasomesha mke digrii ya kwanza na huwa na-enjoy sana kuona excitement yake tunapopata muda wa kujadili dhana na njia mbalimbali za kutatua mafumbo katika masomo yake. Atanikimbia au la? Hainiumizi kichwa sana.