Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Kama kuna kitu ambacho Serikali ya Tanzania inasifika kwa usiri, ni kuficha kwa kipato cha viongozi na usiri wa mali zao.
Tumeonelea kwa muda mrefu ni jinsi gani kila kitu kinafanyika kwa siri na kila mtu akidai kuwa keshawasilisha taarifa zake kwa tume ya maadili.
Lakini tume hii ya maadili, si inafanya kazi kwa ridhaa wa Serikali na si Wananchi, na hivyo kuficha ukweli kuhusu mapato ya watumishi wa Serikali walioko katika nafasi za uongozi kama vile Rais, baraza la mawaziri, Wabunge na mpaka wakuu wa wilaya?
Iweje kila kitu ni siri na kitafahamika kwa Umma pindi Raisi atakapoamua na isiwe ni jambo la kawaida?
Wenzetu Wamarekani, kila mwezi wa nne wa mwaka mpya, kila raia na mkazi anayefanya kazi Marekani , huwasilisha ripoti za mapato yao ya mwaka wa fedha uliopita kwa Mamlaka ya kodi ili kupimwa kama wamelipa kodi ilivyotakikana au la.
Hata Rais wa Marekani, hutoa ripoti kamili inayoonyesha mapato yake na mali zake iwe ni mshahara, rasilimali za soko la mitaji (hisa), mauzo ya mali kama vitabu na mali zingine anazomiliki kama nyumba, mashamba na hata magari na boti.
Sasa nashangaa kwa nini Tanzania mambo haya ni siri na huku tunajitapa kuwa tunataka tuwe wazi na tuna demokrasia.
Wakati wa Ujamaa, ilieleweka kwa nini Viongozi walikuwa wakificha ukweli kuhusu mali walizonazo, kwa kuwa miiko ya uongozi ilikataza kwa wao viongozi kuhodhi na kumiliki mali zaidi ya kipato chao cha mshahara.
Hivi sasa, kila mwanasiasa aliyeko Bungeni au ngazi yeyote ya uongozi na uwakilishi, hudai kuwa ameshafanya wajibu wake kutaja mali zake kwa Mwenyekiti wa tume ya Maadili na hivyo tusimsumbue kujua ana mali kiasi gani.
Sasa kama sisi tungekuwa kama Marekani;
Leo hii hakuna aliyediriki kuuliza swali alilouliza mwalimu Nyerere kwa Lowassa kuwa alipata wapi fedha za kujenga jumba kubwa la kuikodishia Ubalozi wa Afrika Kusini!
Hivyo basi, safari yetu ya kupigana na ufisadi, haianzi na Manji, Lukaza au Mengi pekee, inaanza na Kikwete, Shein, Pinda, Sitta, Karume, Mwamnyange, Manumba, Jaji Ramadhani. Othman, Lowassa, Nahodha, Zitto, Slaa, Kimbisa na wengine wengi ambao ni viongozi.
Tunataka tujue mapato yenu ya mshahara kwa mwaka, mapato mengine ambayo si mshahara na thamani na orodha za mali zenu! Haya ya siri na kutuficha yana lea ufisadi na ukosefu wa uadilifu na nidhamu kati yenu.
Aidha kila pato (mshahara, masurufu, bakshishi, bonasi) ni lazima likatwe kodi! Hii mambo ya kujilipa masurufu na kutafuta safari kila kutwa kuchwa ni wizi wa mchana!
Naambatanisha habari ya mapato ya Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama kama kithibitisho cha nchio iliyojijenga Kidemokrasia na uwazi kutoka kwa viongozi wake. Sitakubali kisingizi kuwa sisi ni bado nchi changa kufikia hatua kama Marekani kuwa wazi katika kujua mapato ya Viongozi wetu!

- Ingekuwa rahisi sana kujua mali za Chenge na hata kumtia mashakani kwa uharaka tuliposikia kuwa ana akaunti ya fedha za kigeni kule Cayman Island.
- Tungeshituka mapema na kumhoji Mkapa alipopata uwezo wa kununua Kiwira na hata kupata mkopo ule wa Dola Laki 5.
- Tusingepagawa kusikia kwamba Mwakyembe ana hisa za thamani kubwa kwa kampuni ya kufua Umeme.
- Karamagi asingeangaliwa kwa mashaka na kampuni yake ya Makontena.
- Alipoibiwa Kapuya mitambo ya kuchimba madini tusingejiuliza katoa wapi pesa.
- Tungejua mapato halisi ya Rostam na mahusiano yake na Kagoda na Dowans.