Mchekechoni
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 279
- 19
Tatizo la usiri wa mapato na matumizi katika makanisa ya 'walokole' limechukua sura mpya baada ya kujitokeza vilio vya baadhi ya waumini toka makanisa mbalimbali ya madhehebu hayo wakitaka uwazi juu ya matoleo yao. Hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na viongozi wakuu wa makanisa hayo kutokuweka bayana mahesabu ya mwaka ya Mapato na Matumizi, kama inavyohitajika chini ya sheria ya usajili wa taasisi zisizo za serikali (makanisa yakiwemo). Sasa ni muda mwafaka wa mambo kuwekwa hadharani mbele ya washarika wa makanisa hayo ili kuweka sawa hali na kuondoa migogoro inayopelekea washirika na viongozi wao kufikishana mahakamani. Makanisa ya Katoliki, Lutheran, Anglikana, SDA, n.k yana utaratibu wa kutangaza mapato mara kwa mara na pia huwasilisha mahesabu ya mwaka tofauti na 'makanisa ya walokole', ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe ili kuepusha janga la kitaifa hasa ikizingatiwa kwamba 'makanisa ya walokole' yametapakaa nchi nzima!