Mapapai :- utamu ,faida na matumizi yake!!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
papaya-in-bangladesh1.jpg

Hapa ni mti wa papai, leo nimekumbuka faida mbili za majani ya mipapai moja ni dawa ya tumbo hasa kama una tatizo la choo kubwa . Unachukua hayo majanai na unachemsha na halafu unakunywa yale maji yake. Pili ni sabuni unaweza au niseme mimi nimewahi kufulia nguo ila usifulie nguo nyeupe basi itakuwa kijani. Nguo nyingine zote sawa kabisa.

i-papaya-half.jpg

Na hapa ni tunda lenyewe nalo lina faida zake kwanza ni kwa ajili ya kula ni tamu sana na pia nalo kama una tatizo la choo kubwa ni nzuri. Halafu jambo jinginge papai ni kilainisho kizuri sana cha chama hasa nyama ya ngómbe. Toa hizo mbege weka kwenye chombo, pondaponda papai na uchanganya na hizo mbegu koroga taratibu katakata nyama vipande vidogovodogo weka humu kwenye mpondo na subiri masaa kadhaa. Hakika utaifaidi nyama yako mno itakuwa lainiiii. Ila kusema kweli nimetamani kweli papai ni muda sasa sijala
 
Mkuu hueleweki! Maana hujaeleza kama hilo papai unalo pondaponda kwaajili ya kulainisha hiyo nyama lazima liwe bivu au la? zaidi ya hapo, pia hujaeleza iwapo nyama hiyo ni lazima ioshwe kwanza kuondoa hilo papai au la? /
 
unapondaponda man kwani nani asiyejua kwamba kabla hujala kitu lazima uoshe
Mkuu hueleweki! Maana hujaeleza kama hilo papai unalo pondaponda kwaajili ya kulainisha hiyo nyama lazima liwe bivu au la? zaidi ya hapo, pia hujaeleza iwapo nyama hiyo ni lazima ioshwe kwanza kuondoa hilo papai au la? /
 
Majani yake pia ni dawa ya kutuliza athma! Kausha majani, changanya na majani makavu ya athma weed (mziwaziwa), then sokota na vuta kama sigara. Ukishondwa basi choma chumbani mwa Mgonjwa ambaye kabanwa na hiyo pumu.
 
Kule indonesia na malaysia utonvu wake huvunwa na kuwekwa kusindikwa kwa ajili hiyo ya kulainisha nyama. Majani na mti wake vikaukia shambani ni mbolea nzuri sana. Matunda yake ni chakula bora kwa ndege. Uchunguzi unafanyika kuangalia kama mti waweza kuwa na mbao nzui.
 
hivi tun gekua na viwanda vya madawa hii si ingekua raw material kwa kumodify madawa ya magonjwa yote hayo kwasababu mimi sidhani kama wazungu wana miti shamba ni kwamba raw materials hizo wanakuja kuchukua huku kwetu africa then madawa wanakuja kutuuzia wenyewe kwanini tusiwaibie ujuzi huo?
Kule indonesia na malaysia utonvu wake huvunwa na kuwekwa kusindikwa kwa ajili hiyo ya kulainisha nyama. Majani na mti wake vikaukia shambani ni mbolea nzuri sana. Matunda yake ni chakula bora kwa ndege. Uchunguzi unafanyika kuangalia kama mti waweza kuwa na mbao nzui.
 
Ponda ponda begu za Papai changanya na maji safi kidogo ni tiba nzuri ya minyoo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom